Naona wazazi wangu wamenichoka, ni muda sasa nami nianze kujitegemea

Naona wazazi wangu wamenichoka, ni muda sasa nami nianze kujitegemea

Hapana mkuu unajua kuna maneno mzazi akiyaongea unajua kabisa hapa mzazi anakunyanyasa hivi kweli mimi na umri wangu huu niachae mavi chooni hebu mkuu think twice, sikuwahi kuambiwa hivi hapo nyuma. Na suala la kuanza kupanga chumba tayari nimeshaweka mipango yangu fresh nina akiba yangu ya boom kama 200k nahisi itanitosha kabisa kuanzia maisha
hapo chomoka fasta utakula mihogo lakini utakaa sawa tu na ipo siku utaiona fursa ya unachofanyiwa sasa
 
Hapo lazima utoboe. Geto la 50K unalipa kuanzia miezi 4 au 6 kabisa. Unanunua godoro lako la tano kwa sita inches 6 linatosha unalitandika chini, pazia nunua zile za bei nafuu kabisa najua chumba kitakuwa na dirisha moja.

Then tafuta mama ntilie aliyekaribu na wewe kaweke bili ya chakula cha mchana na usiku kwa mwezi m'moja haitakuwa pesa nyingi inaweza kuwa hata 60,000. Halafu unaweza nunua hata mtungi wa gesi au jagi la umeme unakuwa unachemshia chai asubuhi kama unapenda kunywa chai asubuhi.

Life litaenda utazoea then utaendelea kujiimarisha as life inasonga mbele.
Kabisa mkuu apa nasubiria boom la awamu ya pili linatoka mwezi huu nikijumlisha na akiba yangu ya 200k natoboa kigheto kibishi yaani
 
Boom linakuchanganya dogo.
Wazazi hawapendezwi na tabia zako tangu umeanza chuo.
Vijana wa kariba yako huwa ni jeuri msiopenda kukosolewa(wasomi uchwara), kuna kazi mnahisi mnadhalilishwa, mahisi mmekua hivyo mzazi hapaswi kukukoromea( elewa kua baadhi ya wazaz mtoto hata awe na 50 yrs kwao bado ni mtoto tu)..

Timiza majukumu uliyopangiwa, bado upo kwao fuata yanayokupasa, jeuri haitokusaidia.

Maisha yakikukaba koo huko ulikopanga, utaandika uzi kua wazazi wako hawakujali.

Kama unaenda kupanga basi kapange mkiwa na hali nzuri wewe na wazee wako. Waambie mpango wako wa kupanga ukiwa tayari umejirekebisha.
 
Usitoke hapo Kwa hsira kupanga kugumu kwakuwa una boom jipanhe kidogokidogo angalia Nini unaweza kufanya muda huu tengeneza connection za kupata hata vibarua vitavyokuwezesha ukitoka nyumbani usihangaike ukimaliza chuo ndio ukapange
 
Usiombee uzaliwe kwenye familia ambazo historia ya wazazi wako nao walinyanyaswa na wazazi wao (bibi na babu) huwa wana revenges
Mohamedex121
🔧🔧🔧Yes umemaliza wanaona kulipa kisasi ndio kunawafanya nao wapate amani ya moyo na akili..mara nyingi hua ni Ugonjwa

Naomba wapende kwasababu ndio Wazazi wako uliojaaliwa na MWENYEZI MUNGU na ni Wagonjwa pia wanasumbuliwa na (PTSD) yaan POST STRESS TRAUMATIC DISORDER ni ugonjwa hatari sana🤦👋
 
Hamna maza sikuhizi kabadika mpaka mimi namshangaa sijui anataka nini kwangu kama anataka nijitegemee kwanini asinifukuze nijue moja sio kunifokea tena kwa sauti kubwa.
Sikiliza mdogo wangu,
Mzazi hawezi badilika bila Sababu za msingi,lazima Kuna sehemu utakuwa unamkwaza,kaa tafakari njia zako hapo nyuma na za sasa utajua tatizo Nini!
Kama mzazi anajaribu kukuweka kwenye njia iliyo sahihi,humu utashauriwa mengi,tafadhali yachuje Kabla hujafanya maamuzi.

Haya unakwenda kupanga chumba source of income ya kulipia Kodi na kula,kulipia bili za umeme na maji,vitanda na godoro ,vyombo unazitoa wapi?unafanya kazi?
 
Boom linakuchanganya dogo.
Wazazi hawapendezwi na tabia zako tangu umeanza chuo.
Vijana wa kariba yako huwa ni jeuri msiopenda kukosolewa(wasomi uchwara), kuna kazi mnahisi mnadhalilishwa, mahisi mmekua hivyo mzazi hapaswi kukukoromea( elewa kua baadhi ya wazaz mtoto hata awe na 50 yrs kwao bado ni mtoto tu)..

Timiza majukumu uliyopangiwa, bado upo kwao fuata yanayokupasa, jeuri haitokusaidia.

Maisha yakikukaba koo huko ulikopanga, utaandika uzi kua wazazi wako hawakujali.

Kama unaenda kupanga basi kapange mkiwa na hali nzuri wewe na wazee wako. Waambie mpango wako wa kupanga ukiwa tayari umejirekebisha.
Mkuu we unaongea tu ila mimi nimeshajitahidi kufanya kazi za nyumbani kama kuosha vyombo naosha deki pia napiga hata jana pia nilipiga deki na maza akafoka ananiambia napiga deki vibaya sijui maji niliopigia ni machafu wakati maji ni masafi tu hayana shida. Na mimi kwenda kupanga nimeamua ili niepuke na kero za bimkubwa maana yeye ni mtu wa kufokea fokea bila sababu za msingi sasa naona kama kanichoka
 
Usitoke hapo Kwa hsira kupanga kugumu kwakuwa una boom jipanhe kidogokidogo angalia Nini unaweza kufanya muda huu tengeneza connection za kupata hata vibarua vitavyokuwezesha ukitoka nyumbani usihangaike ukimaliza chuo ndio ukapange
Tatizo kuwa nyumbani kwa wakati huu naona sina amani wala furaha so nimeamua kwenda kupanga angalau niwe huru na maneno ya bimkubwa. Kuhusu connection za vibarau nitajuwa huko huko naimani Mungu ataniongoza mkuu
 
Sikiliza mdogo wangu,
Mzazi hawezi badilika bila Sababu za msingi,lazima Kuna sehemu utakuwa unamkwaza,kaa tafakari njia zako hapo nyuma na za sasa utajua tatizo Nini!
Kama mzazi anajaribu kukuweka kwenye njia iliyo sahihi,humu utashauriwa mengi,tafadhali yachuje Kabla hujafanya maamuzi.

Haya unakwenda kupanga chumba source of income ya kulipia Kodi na kula,kulipia bili za umeme na maji,vitanda na godoro ,vyombo unazitoa wapi?unafanya kazi?
Najua sikuhizi nimebadilika nahisi hata wazazi wanalijua hili na kubadilika kwangu nikutoka na majukumu niliyonayo sasa hasa ukizingatia masomo chuoni nakosa muda wa kufanya kazi hasa katikati ya wiki na pia kuchelewa kurudi nyumbani sio kwamba nimeanza uhuni??hapana ni majukumu tu ya chuo yananifanya nifanye hivi maana huwa na baki mpaka saa 4 usiku na muda huo nautumia kujisomea chuoni maana kusoma home jau sana ukizingatia kelele za bimkubwa uwezi kuwa na utulivu. Sasa ndugu yangu kwa mabadiliko haya hivi ni kweli maza aanzee kukuchukia bila sababu za msingi
 
Back
Top Bottom