Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 60,050
- 104,466
Watakapofariki Wazazi wako kabla hujasimama kimaisha ndio utakuja kuwakumbuka na kuelewa kwamba hawakuwa wanakunyanyasa Bali walikuwa wanakufundisha maisha.Acha tu hapa naishi na wazazi wangu tena wakunizaa ila naona manyanyaso yamekuwa mengi hapa nyumbani ngoja nichomoke mwisho wa mwezi huu
Nyinyi Watoto wa sasa hivi ni shida sana, hamuwezi kujituma Nyumbani kila kitu mpaka muambiwe.
Inasikitisha sana na hasa ukichukulia sisi Wazazi wetu hatukuwagharimu pesa tulisomeshwa bure na Nyerere na tulisoma wote shule za umma na Watoto wa mawaziri.
Kuna kijana wangu wa rika lako naye kila nikijaribu kumseti inaonekana ana akili za kitoto kama zako, inasikitisha kijana wa kiume hata kuamka tu asubuhi mpaka uamshwe kisa upo likizo, mtapata tabu sana kwenye maisha yenu am telling you.