Napagawa na Bati: ALAF, ANDO, DRAGON - uchaguzi mgumu. Watu wa mauzo saundi kibao!

Napagawa na Bati: ALAF, ANDO, DRAGON - uchaguzi mgumu. Watu wa mauzo saundi kibao!

Nahitaji pc 279 ila changamoto niliyokutana nayo ni kama yako mkuu!

Hata sijui yupi mkweli yupi mpigaji kabla sijafanya uamzi
 
Mwenye ufahamu au uzoefu na haya mabati ya rangi atupe elimu
 
Nimemaliza Kupiga Mbao, site yangu wameshakuja watu wa sales wa makampuni mbalimbali, na wamenipiga saundi za kutosha.

Mafundi nao waliopiga mbao wamenishauri ila walivyoona nimepagawa sielewi nitumie bati kampuni Gani wakaniambia wewe Bosi leta bati yeyote sisi tutapiga mana sijui tukushaurije.

Katika watu na makampuni niliongea nao Kila mmoja anavutia kwao, nimeamua Sasa nibaki na choises tatu tu ANDO, ALAF na Dragon mana nisije kuchizika.

Katika bei ukipanga Kwa namba 1, 2 ,3 wakwanza na wapili tofauti ya bei ni 2800 , wapili na watatu tofauti ya bei ni 3000, na wakwanza na watatu tofauti ya bei ni 5300 Kwa Kila MITA ya bati, Mimi nahitaji mita 600.

Sasa mabati yote ni mazuri, ila kati ya Ando, ALAF na Dragon nani Bora zaidi, hapa ndo mtego umejificha, makampuni mengi yanasema hiyo kampuni bei yao IPO juu c Kwa sababu ya ubora Bali ni kwasababu Wana brand kubwa.

Naombeni mnishauri, nichukue bati Gani ambayo itakuwa ni Bora zaidi kati ya hizo tatu hapo

Site ipo mkoa Gani?? Mi nimetumia Dragon ila niliagiza kiwandani sio kununua madukani na haijapauka hata kidogo.
 
Mwenye ufahamu au uzoefu na haya mabati ya rangi atupe

Upo mkoa Gani na choice Yako rangi gani maana Kuna rangi nyingine majanga na zinapauka sana kulingana na Hali ya hewa. Charcoal grain ni nzuri ila isiwe nyeusi Wala blue hizo rangi ni tatizo. Utanishukuru panapo majaliwa kwa huo ushauri
 
Nahitaji pc 279 ila changamoto niliyokutana nayo ni kama yako mkuu!

Hata sijui yupi mkweli yupi mpigaji kabla sijafanya uamzi
Nenda ALAF. Kuna house niipaua 1994 hadisasa bati zake ni Imara na hazina kutu.
Kuhusu za rangi bado nashauri nenda ALAF ni miaka 15 nimepauwa na bati za rangi still paa lina vutia
 
Nenda ALAF. Kuna house niipaua 1994 hadisasa bati zake ni Imara na hazina kutu.
Kuhusu za rangi bado nashauri nenda ALAF ni miaka 15 nimepauwa na bati za rangi still paa lina vutia
ALAF nimewacheki bei Yao imesimama hatari. Hivi hakuna kampuni nyingine inayozalisha mabati Bora Kwa bei ya kitanzania zaidi ya hao ALAF ?
 
Mkuu acha kupata shida njooo sunbank nikuuzie bati Bora kwa gharama nafuu kuhusu ubora tunazo evidence za project ambazo tumeezeka nazo nyingi Zina 5yrs +
No kupauka
Kabla ujanunua fanya research za izo project
Mfno kwa moja ya project zetu Kati ya nyingi apa dar tumeezeka maktaba kuu ya taifa

0685572320
Huwa mnatabia tenda kubwa zinazonekana mnaongeza wingi wa aluminium materiaal kwenye coating. Ila mass production kwa wanannch wa kawaida mnaweka rangi za ukumbini ambazo hazidumu 3years
 
Dragon ondoa kwenye list. Mwaka tu linakuwa limepauka
 
ALAF nimewacheki bei Yao imesimama hatari. Hivi hakuna kampuni nyingine inayozalisha mabati Bora Kwa bei ya kitanzania zaidi ya hao ALAF ?
Bei yakitanzania na Bati litakua lakitanzania

Price = Quality
 
1. Alaf
2. Sun share
3. Kiboko
4. Kinglion
Kikubwa zingatia uchukue gauge 28, kama upo karibu na bahari usijaribu kuchukua gauge 30 bati litapauka utaichukia nyumba yako
 
ALAF nimewacheki bei Yao imesimama hatari. Hivi hakuna kampuni nyingine inayozalisha mabati Bora Kwa bei ya kitanzania zaidi ya hao ALAF ?
Bei imesimama bati ya elfu 27 kwingine kule ni 41 elfu lakini nimkataba
 
Back
Top Bottom