mama D
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 19,981
- 35,581
mama D unaweza ishi bila kutenda dhambii? Unaamini kwamba dhambii zote ni sawa?
Hata Mungu anajua ndio maana tuna kibali cha toba
Dhambi zote ni makosa yaliyosawa mbele za Mungu lakini zipo dhambi zinazozalisha majanga mengi kwetu zaidi ya nyingine
Ulishawahi kujiuliza madhara ya dhambi ya ZINAA?
ZINAA ni chanzo cha magonjwa mengi na vifo vingi kuliko dhambi zingine
ZINAA ina hatari kubwa sana kwetu maana ukishanajisi mwili inamoishi roho yako huna sehemu ya kukutana na Mungu wala malaika
1 WAKORINTO 6:18-20
Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.
Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.