Napata Mshahara wa laki 3, nataka niache kazi nikajiajiri

Napata Mshahara wa laki 3, nataka niache kazi nikajiajiri

Wewe kwenye kujiajiri,vyote unavyo kasoro kimoja tu,uthubutu wa kuamua kuanza,
Unao mtaji,chombo Cha usafiri kukurahisishia mishemishe unayo,bado uthubutu wako na wazo la n nini ufanye ndo umekosa,
Unatakiwa usiogope kuamua ,watu wanaendesha biashara mtaji milioni,pesa inayozunguka kwenye uchuuzi Ni laki 4 tu na daily uhakika kukunja 15 Hadi 30
Asante changamoto kuna kazi moja ninaisubiria mpaka leo na sina uhakika itakuja lini na hiyo ndio iliyonipa million 3 kwa ajjili ya biashara.
 
Ukiona huwezi fanya maamuzi mwenyewe ya kuacha kazi na kujiajiri ujue mda bado na usiache, unachopaswa kuuliza ni, nimeacha kazi, nimeamua kufanya biashara ya machungwa, wajuzi wa biashara nipeni ushauri.
Hakuna siku muda utafika utasema uko tayari kwa kufanya jambo lolote kitu ambacho nauliza ni kutaka kujua tu
 
Kwa sababu una mke (familia); weka akiba/ fedha ya kutumia mwaka mzima, baada ya hapo acha kazi na uanze kujiajiri kwenye fani unayoiitaji
Nilitaka hii pikipiki nimkabidhi boda hesabu awe ananiletea halfu mimi niende nikafanye mchakato wa kuanza maisha mapya
 
Acha ujinga wewe kitoto.
Tuliza akili kusanya kidogo kidogo uwe na capital ya kutosha kujiajiri sio matako kuwa kila mtu anayo

Jichunguze utaweza na je una passion n hayo mambo sio badae uanze kutupa story za mikono ya watu kwenye mikono yako
Kwanza usinitukane kitoto unanijua
 
Nataka nikafanye mkoa issue za umachinga mkuu
Umachinga bora Dar Mkuu, mkoani utateseka sana kutoboa. Mzunguko wa mkoani huwa ni jau sana kaka na mbaya zaidi saa za biashara mkoani ni chache sana yaani saa mbili hadi saa kumi na mbili jioni, ukiforce sana saa mbili usiku tena napo miyeyusho.

Sikushauri kwenda mkoa kufanya umachinga Mkuu.
 
Wakuu,

Mimi nikijana ninafanya kazi kwenye taasisi moja nchini kama Volunteer kwa muda wa miezi sita sasa.

Mwanzo nilikuwa nafanya kazi kwenye moja la shirika kubwa na mshahara mzuri sema mkataba uliwahi kuisha.

Hivyo Sehemu nayofanyia kazi kwa sasa nalipwa laki 3 ambayo hiyo hela nikijumlisha na mahitaji yote ni ndogo sana.

Juzi NSSF wamenilipa million 3. Na nina pikipiki nilinunua bodaboda wangu kairudisha so niko nayo.

Nimepata wazo la kuacha kazi nikajiajiri kwa hii Hela niliyoipata ya mafao.

Niliwaza mkoa wa Morogoro au Dodoma.

Ushauri wakuu.
kuacha kazi sio kazi kazi kupata kazi tafuta kazi ukiwa bado unafanya kazi hiyo
 
Kwani ukiendelea na ajira huko na biashara huku utashindwa kusimamia? Biashara sijui ni upande wangu lkn kwasasa naona ni nzito sana! Usiache kazi kwanza fikiria namna bora ya kuendesha biashara huku ukiwa kazini.
Ni kazi sana kufanya Biashara uku unafanya kazi kwa mtu, izo wanawezaga wanasiasa tu mana wao waga wana weka ela tu kwny biashara kutoka kwny mikeka yao hawaoni asara kwny biashara
 
Asije kusema hatukumwambiaa yani ni jambo hatari sana.
Usinitishe mkuu.

Nikwambie kitu kazi niliyotoka nilikuwa nalipwa laki 8.

Kabla ya hii kazi nishapata kazi mbili sema sikuwa nimejiandaa kwenda mkoanj.

Hivyo sio muoga sana kiivyo kimaisha.

Na nishawahi kufanya biashara nyingi tu.

So sio mjinga kiivyo kisa nimeomba kazi
 
Back
Top Bottom