Nape ataka Akaunti ya Deni la Taifa ichunguzwe na iwekwe bayana Fedha hizo zilikopwa na kupelekwa wapi?

Nape ataka Akaunti ya Deni la Taifa ichunguzwe na iwekwe bayana Fedha hizo zilikopwa na kupelekwa wapi?

Hiyo ndo inaonyesha kuna mengi mno yanafichwa.

Ile habari ya bunge lipitie mikataba yote ya nchi haipo tena.

sijui kwa nn hata bunge linafichwa mambo mengi lakini tena uwezo wa bunge hili la sasa kujadili hiyo hoja sioni kama litathubutu.
Hovyo sana nchi hii inavyoendeshwa na kwa kweli yule bora alitangulia awamu ya pili ndo kabisa mngetega mikono anye juu ya mikono
 
Trillioni sitini na nne
ohnoway.png
 
Usilete uchonganishi; Nape ametoa hoja ya msingi na uchunguzi huo lazima uanzie awamu zote za nyuma. Nakumbuka enzi za Kikwete na Waziri wake wa fedha Mustapha Mkullo walifloat bond in foreign currency na fedha zile hazikujulikana zilitumika kwa miradi gani!! Zitto alijaribu kuulizia akazibwa mdomo!!! Uchunguzi ukifanyika professionally tutajua mambo mengi yanayokwamisha maendeleo yetu.

Tanzania haijawahi ku issue bonds kwenye masoko ya mikopo ya kimataifa kama vile EuroBond.
 
Mbunge wa Mtama Nape Nnauye ametaka ufanyike uchunguzi wa akaunti ya deni la taifa na iwekwe bayana kila senti ilikwenda wapi na ilifanya nini?

Source: ITV habari
Haya ndiyo mambo ambayo mbunge makini anaweza kuhoji na kueleweka. Maelezo rahisi rahisi tu kuhusu ustahimilivu wa deni la Taifa na uwezo wetu wa kuzidi kukopesheka ni hoja isiyo kuwa na mashiko yoyote.

CAG na timu yake ni lazima wakague matumizi halisi yaendanayo na fedha zilizopatikana kupitia deni hili. Deni la ndani limekuwa kubwa sana hata kuathiri uwezo wa mifuko ya jamii kujiendesha yenyewe kiufanisi.

Tukiligeukia deni la nje nalo pia limegubikwa na usiri mkubwa sana. Waziri mwenye dhamana badala ya kutoa taarifa kwa uwazi juu matumizi ya deni hili, yeye hukimbilia kutoa taarifa za uhimilivu wake.

Mh. Nnauye umeamsha hoja makini sana ambayo hapa jukwaani naamini itatendewa haki kupitia mijadala yenye madini. Nashauri hata naye waziri mwenye dhamana, Mh. Mwigulu abadili ID yake hata muda hapa jukwaani ili awe huru kulizungumzia suala hili.
 
Mbunge wa MTAMA Nape Nnauye amesema deni la Taifa limekuwa kwa kasi sana ndani ya miaka 5 iliyopita na kusema japo Serikali inadai ni himilivu hali sio nzuri...
Yure mupe yure muruke. Zama za uwazi hizi katika kuhoji, wala si za kutekana, kupotezena ama kuumizana.
 
Ziwe zinafanyika press conference mara kwa mara kwa Vinara wa BOT na Wizara ya fedha,ila hao wana habari wajumuishe wanahabari wenye utaalamu wa uchumi,fedha,biashara .
Kuna uwezekano mkubwa tukaacha visingizio.
 
Nakuunga mkono hoja, amewaza kama tunavyo waza wengi
 
Nawaza kwa sauti tu:
[emoji830]︎Ujenzi wa Meli mpya na ukarabati wa meli za zamani kwenye Maziwa makubwa nchini kurahisisha usafiri wa mizigo (mazao ya wakulima) na abiria ukaboreshwa...
Hizo meli ni bei gani? Miradi ya SGR na SG respectively hakuna hata mmoja uliofika 1/3 ya mpango. Kama unabisha dhibitisha. Isitoshe kulikuwa na uongo mwingi wa kupotosha umma kuwa hiyo miradi ni ya fedha za ndani.

Tulikuwa tunasema serikali ya Magufuli ilibobea kwenye upikaji data. Fafanua ni miradi ipi imefikisha deni kuvuka 20t maana hata hizo hospitali na vituo vya afya havivuki 500b, na wala idadi inayotajwa sio ya kweli bali ilikuwa ni data za kupika ili kuhadaa umma.
 
Huyo alipaswa kua jela KWA Sasa,ni JPM tu alimstahi. In short hana Morality ya kuongea chochote na ndo Mana alichagua kukaa kimya.

Thread za maovu yake zimejaaa humu if,unaweza kusearch
Mtu hatakiwa kuwa jela au nje kwa hisani ya mtu yoyote bali kwa mujibu wa sheria ndani ya katiba. Na sisi polepole tutoke kwenye siasa za kutukuzana binadamu badala ya Mungu.
 
Mtu hatakiwa kuwa jela au nje kwa hisani ya mtu yoyote bali kwa mujibu wa sheria ndani ya katiba. Na sisi polepole tutoke kwenye siasa za kutukuzana binadamu badala ya Mungu.
Kweli mkuu
 
Back
Top Bottom