Nape: Bando ni huduma ya ziada, ukitaka lisiishe tumia salio la kawaida. Mbunge ataka liwe kisheria

Nape: Bando ni huduma ya ziada, ukitaka lisiishe tumia salio la kawaida. Mbunge ataka liwe kisheria

Safi Nape. Kipindi Kile Mlikuwa amnaambiana kuwa Nape ni shujaa. Si kila ambaye alipishana na Magufuli alikuwa na akili. Wengine walikuwa vilaza sana. Nape Sijawahi mwona ana akili toka wakati wa Kikwete. Wapinzani walikuwa wanamwona Nape na Makamba ni mashujaa... Sasa wanaona rangi kamili. Mtu ambaye aligombana na Magufuli lakini alikuwa na akili alikuwa Tundu Lissu.
 
... Nape kwa hili yuko sahihi. Bando ni added service yenye masharti nafuu ili kuvutia wateja na mojawapo ya masharti hayo ni kikomo cha matumizi.

Ukiifanya huduma hiyo iwe ya lazima kwa kuitungia sheria sio kivutio tena bali ni takwa la kisheria which is not right. Itadumaza ubunifu na kuondoa ushindani.
Ushindani gani unao uongelea? Hivi miaka yote umeshawahi sikia kelele za watu kulalamika bando kuwa juu zaidi ya mwaka huu?!
 
Sijawahi ona nchi yoyote dunia hii, eti wakupe bando alafu isiwe na kikomo cha muda.. Hilo halipo, ila ukiwa hutaki bando, baki na hela yako unatumia bila kununua bando, which is very expensive..!!

Uwizi mkubwa unafanyika kwenye bando kuisha, yaani GB 2 au 3 say, unakuta within 3 hours haipo, kwa kuperuzi tu, huja download au upload chochote..!!
Kama bundle liwe na kikomo basi mfano nimenunua GB 40 na kila siku natumia 500MB then ikifika mwisho wa bundle ikate nikiunga kile kifurushi changu kiendelee kuwapo kijaziwe na hiki kipya.
 
Sijajua kwann Yule jamaa aliye mnyanyulia bastola hajamalizana nae jumla jumla
Mungu ana makusudi yake. Kipindi kile alikuwa na angeonekana shujaa sana. Na pengine mngesema anafaa Kuwa RAIS. ila haya yote ni kwamba watu mjifunze kitu pia.
 
Hicho ndio kinachofanyika. Hizo hela, zote ni serikali inachukua ndio maana Nape anajibu kwa Nyodo. Wananchi tungekuwa na umoja tugomee hata siku tatu kununua huduma toka kwenye hiyo mitandao tutaheshimiana.
Wanachi wa bongo ubinafsi wetu ndio unatuponza. Na ndio maana tunapata watu wabinafsi katika uongozi.
 
Ushindani gani unao uongelea? Hivi miaka yote umeshawahi sikia kelele za watu kulalamika bando kuwa juu zaidi ya mwaka huu?!
... bando ni matokeo ya ubunifu na ushindani; haipo kwenye huduma za msingi. Kesho na keshokutwa wakija na ubunifu mwingine nao mtataka muutungie sheria kisa wananchi wanalalamika. Anayelalamikia bando si arudi kwenye huduma ya msingi?
 
Walamba asali mnateteana.

Yani mtu anunua bando la GB 1 apate mb800 na wewe unatetea uozo huo?
... bando ni matokeo ya ubunifu na ushindani; haipo kwenye huduma za msingi. Kesho na keshokutwa wakija na ubunifu mwingine nao mtataka muutungie sheria kisa wananchi wanalalamika. Anayelalamikia bando si arudi kwenye huduma ya msingi?
 
... bando ni matokeo ya ubunifu na ushindani; haipo kwenye huduma za msingi. Kesho na keshokutwa wakija na ubunifu mwingine nao mtataka muutungie sheria kisa wananchi wanalalamika. Anayelalamikia bando si arudi kwenye huduma ya msingi?
Ndio watuibie?
 
Waziri wa habari, Nape Nnauye amewataka wabunge kuacha kutuhumu wizi kwenye mitandao ya simu kwa ujumla.

Nape amesema bando ni huduma ya ziada ambayo ina masharti ya muda, mtu akitaka lisiishe uko utaratibu wa kutumia 'Main Tarrif' akitolea mfano tiketi za kusafiria za mwezi ambayo hauwezi ukadai hata ukitumia mara moja.

Nape amesema hofu yake ni kutumia Bunge kushutumu uwekezaji mkubwa kuna wizi inakwenda kuharibu huduma ya mawasiliano.

Spika Tulia akifafanua swali la mbunge, alimtaka Nape aeleze kama ni sheria au utaratibu na kama Bunge linao uwezo wa kubadilisha au haliwezekani.

Nape amesema ni utaratibu wa kibiashara ndio maana bei yake ni ndogo kulinganisha na kutumia salio na sio suala la sheria.

====

Akitoa hoja, mbunge Franscis Mtinga ametaka bando ziwe kisheria na Nape kama ambavyo alileta muswada wa kulinda habari binafsi, alete muswada wa kulinda haki kwani mashirika ya simu yanaibia wananchi sana. Mbunge ametaka kutopangiwa jinsi ya kutumia bando alilonunua.

Kuna mawaziri ovyo watatu tz kama Nepi,kipara na waziri wa kwenye miamba hawa ni mawaziri ovyo Sana.
 
... hiyo sasa ni kazi ya regulator (TCRA) kutoa majibu na solution. Iko hivi, Serikali inamiliki kampuni ya mobile (TTCL) ni opportunity kwao kuweka bando bila expiry date ili wananchi tukimbilie huko then automatically na wengine hawatakuwa na options zaidi ya kuiga ili wabaki sokoni.

Hiyo ndio maana ya competion sio ushindani kutungiwa sheria za kijinga anazo propose huyo mbunge.
Uko sahihi ndugu yangu mradi TCRA isifanye kazi kama Idara ya Serikali. TCRA ni shirika la Umma ambalo limeundwa kisheria kulinda maslahi ya Serikali, Wawekezaji na Mlaji kwa uwazi kabisa.
Aidha, kwenye sheria zote za Mashirika ya Udhibiti kuna kipengele kinachohitaji kiwepo chombo cha kutetea maslahi ya mlaji. Kile chombo kikiundwa ipasavyo, kunakuwa na wajumbe ambao wanajua ndani na nje ya IT, kwa upande wa TCRA, ili kila jipya likijitokeza hiki chombo kiweze kuchambua pumba ni ipi na mchele ni upi kwa niaba ya Mlaji. Waziri Nape anatakiwa alielezee Bunge na Wananchi utaratibu huu kama umeundwa ipasavyo na kama unafanya kazi ipasavyo. Vyombo vyote viwili, TCRA na kile cha Utetezi wa Mlaji vinalipiwa na Serikali/wananchi. Ni vyombo vyetu, siyo wakubwa wetu! Kama utaratibu huo haupo au haufanyi kazi, ni jukumu la Waziri ama kuelekeza au kuwajibika Bungeni. Sheria hizi zilitungwa kiwango cha kimataifa, ingawa tumeanza kuvibadili baadhi ya vifungu vifanane na ulemavu wetu. Nimalize kwa kuomba msamaha andiko refu mno; ila kwa hapa petu Tanzania, dhamira na uwezo wa kufuatilia na kutekeleza masuala kwenye kiwango hicho cha kimataifa ndiyo tunashindwa, isipokuwa masuala machache binafsi ambayo uwezo wetu tunayashinda mataifa mengi!
 
Kama bando ni huduma ya ziada je kwenye huduma ya msingi tuseme 10k unapata mb ngapi
Hii huduma wanayoita ya ziada watu ndio wanaitumia sana na imeshakuwa ya msingi isiwe kigezo cha kuwazulumu wateja
 
Kwa hili ingawa tunaumia wananchi ila Nape yupo sahihi
Sasa nimeelewa ni kwanini mafuta soko la dunia yakipanda basi na agents wanapandisha hapo hapo ila yakishuka wanasubiri stock ya nyuma iishe. Waziri mwenye dhamana kazi ni kupambania wananchi siyo kutoa majibu dry, sawa ni ofa kwa hyo kupitia ofa ndo uwapige watu? Vipi nikienda kwenye matumizi ya kawaida ndo yana bei elekezi kuwa kila mtandao kwa dakika 1 ni sawa na kiasi fulani cha pesa?
 
Udanganyifu upi au tunaongea vitu tofauti? Unapewa bando unaambiwa bando hilo litatumika kwa kipindi cha mwezi mmoja. Mwezi mmoja ukiisha definitely hilo bando halitatumika tena, ni udanganyifu gani hapo.
Mbona kama vile wewe ni kichwa ngumu!! Umeelewa alichomaanisha kweli? Unaenda kununua bando promo yake ni 1GB, ila ukilinunua tu unajikuta unapewa mb 800 kwa bei ileile. Au umenunua sms 200, unatuma sms 10 tayari ujumbe wa kubakiza sms chini ya 7, ukituma 2 tu tayari zimeisha. Wizi huu upo hata kama wewe hujakutana nalo.
 
Kwa mfano makampuni yanatangaza kuanzia kesho hakuna bando hivi mtakuja hata jf kweli,unaweka 500 yako hata hujamaliza kusoma post moja imeshakwanyuka. Makampuni wana haki.
Na wao watumie huo mfano wako wafanye hivyo waone kama wataingiza hela mbwa hawa. Biashara ni kulindana kati ya mteja na mtoa huduma! Unafikiri kila mwenye kisimbuzi anaweka kifurushi bei zinapopanda? Wengine huishia kusema local channels zinatosha
 
Waziri anawatetea wenye kampuni kina rostam badal ya rostam kuja kujitetea
 
Kwa mfano makampuni yanatangaza kuanzia kesho hakuna bando hivi mtakuja hata jf kweli,unaweka 500 yako hata hujamaliza kusoma post moja imeshakwanyuka. Makampuni wana haki.
Kijan umesoma Burundi nn mnk burundi wanaanchi wenye smart phone hawafiki elf 50 nchi nzimaaa
 
Waziri anageuka kuwa msemaji na mtetezi wa makampuni.

Watu dizaini hii ni rahisi kuuza nchi

sasa wewe kodi unalipa? 😂 😂 😂 😂 hata ingekua mm, mtu anatoa mabilioni kila mwezi kwenye kodi peke yake alafu na wewe kutoa hata buku jero ya tozo unataka kwenda kufungua kesi mahakamani
 
Back
Top Bottom