Nape: CCM itashinda tu uchaguzi mkuu ujao hata kwa goli la mkono


Nape atakuwa anatafuta pa kutokea kuelekea kwenye chama chake cha ccj,hivyo anataka ahakikishe anaibomoa ccm
 
hata mi nawalaumu ukawa na upinzani kwa ujumla wapo kama vile hawapo wamepokea 230m wamegeuka viziwi na mabubu ghafla ila najaribu kujiaminisha ukimya wao wanautumia kupanga mashambulizi mazito kama walivyosema wahenga kimya kikuu kina mshindo mkuu

Walau Godbless Lema amejaribu kuonesha kuwa bado yupo kwenye game anaendeleza harakati za kuuza uhai wake Arusha! Sina ugomvi naye mtu huyu!
 

Wewe mleta uzi huu uombe nape hasikujue kwani akikujua lzm atakunyang'anya kadi ya uanachama
 
Huu ni ukweli mchungu sana. ccm ndio chama kinachoongelewa sana na wananchi kuwa na wagombea urais wanaopimika, wanaoweza kuongoza nchi, wenye record safi na wenye uzalendo na mapenzi kwa tanzania.

in fact wapinzani ni wasindikizaji.

Mkuu ni CCM yenye wagombea safi au ni woga tu wa mabadiliko!?
 
hata mi nawalaumu ukawa na upinzani kwa ujumla wapo kama vile hawapo wamepokea 230m wamegeuka viziwi na mabubu ghafla ila najaribu kujiaminisha ukimya wao wanautumia kupanga mashambulizi mazito kama walivyosema wahenga kimya kikuu kina mshindo mkuu

unaelewa maana ya KIMYA KINGI KINA MSHINDO MKUU? maana yake ni kwamba UKAWA wapo kimya lakini watakapoanza kuongea magamba watajuta kwanini walikuwa wanatoa kauli za KICHOCHEZI kama hizi.
 
Huu ni ukweli mchungu sana. ccm ndio chama kinachoongelewa sana na wananchi kuwa na wagombea urais wanaopimika, wanaoweza kuongoza nchi, wenye record safi na wenye uzalendo na mapenzi kwa tanzania.

in fact wapinzani ni wasindikizaji.

mknd wako! hz kauli za kichochezi za Nape Nnauye zikiingiza nchi kwenye umwagaji wa damu, mtafute mahali pa kukimbilia.
 
Last edited by a moderator:
"CCM itashinda tu hata kwa Goli la Mkono" Nape

Kauli hii ni hatari mno tena katika wakati kama huu tunajiandaa na uchaguzi mkuu. Lakini hapana shaka kuwa hii ni kauli ya Chama Cha Mapinduzi. Kwa tunaofahamu kazi ya "Katibu wa itikadi na uenezi" ni kueneza anayoagizwa na chama chake, hivyo yote anayoyasema Nape ni kwa niaba ya chama chake.

Ushauri wangu; Watanzania tunahitaji sana kubaki na amani yetu iliyojengwa katika misingi imara na waasisi wetu, vyama ni taasisi za muda, huzaliwa na kufa, lakini ardhi hii itadumu milele. Japo hata mimi naona kila dalili ya siku za CCM kuhesabika, basi watambue hii ni siasa na siasa ni mchezo wa namba, ukiona namba haitoshi wapishe wenzako, CCM inapaswa kujiandaa kisaikolojia. Nasema haya kwa sababu naamini, Tanzania ya leo si Tanzania ya jana, kama CCM wataamua kufunga Goli kwa mkono hapana shaka watanzania hawa ninaowafahamu hawatauacha mkono huo salama, lazima wataukata.

Tafadhali, CCM msituvurugie Nchi
 

Kazi ipo mwaka huu
 
kauli ya nape huenda imetoka kwa mwenyekiti wa tume. huwezi jua. maana majaji wengi ni wanaccm...

Na ndiyo maana wananchi wakilalamika kuhusiana na zoezi zima anakuja juu kama moto wa kifuu.

Nina wasiwasi hizi vurugu za uchaguzi zitaanza hata kabla ya uchaguzi
 
Nape(Nepi) ni kiongozi wa hovyo sana. Huwezi kutoa kauli chafu kama hiyo. Halafu JK hamkemei si ndio maana tunajua anamtuma. Kama hamtumi basi kwa kauli hiyo ajitokeze hadharani kukanusha hii italeta balaa siku za usoni.
 
unaelewa maana ya KIMYA KINGI KINA MSHINDO MKUU? maana yake ni kwamba UKAWA wapo kimya lakini watakapoanza kuongea magamba watajuta kwanini walikuwa wanatoa kauli za KICHOCHEZI kama hizi.

sasa reply yako na komenti yangu vina tofauti gani??
 
Yes sasa nimekubali patakuwa na vurugu....kama kweli Nape kaongea hivyo basi amani hakuna tena.Nani anakumbuka mwaka 64 pale mapipa jinsi ile nyumba ya Mwarabu ilivyopigwa mabomu.
 
Mfunge goli la mkono wakat washabiki tunaona?? Hakika tutaingia uwanjan kulikataa goli hilo, tunajua kua refa ni wenu lakin washabiki tutaamua mshind wa halali ni nan. Tukutane Oktoba
 
CCM iko madarakaani kwa wizi wa kura, Nape ametuthibitishia hili, kweli Mungu hamfichi mnafiki.
Chama ambacho msemaji wake ni aina ya Nape kina kila dalili ya kufa...kwa kauli hii ya Nape nitamshangaa mwenyekiti, katibu, makamu wasipokemea kaluli hii... nitaamini kuwa kweli magamba ni sikio lakufa.
 
CCM imesema kuwa itahakikisha inarudi Ikulu hata “kwa bao la mkono” wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 25.



Katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye alisema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana kwenye viwanja vya Nyehunge wilayani hapa.



Neno “bao la mkono” hutumiwa kama goli lililofungwa kwa kuupiga mpira kwa mkono kinyume cha taratibu za mpira, lakini hukubaliwa kwa kuwa mwamuzi anakuwa hajaona kitendo hicho.
“Rangi inayoenda Ikulu ni hii (anaonyesha shati lake la kijani ambayo hutumiwa na chama hicho).


Tuna uhakika na ushindi wa Rais. Kwa namna yoyote ile, CCM itarudi Ikulu hata kama ni kwa bao la mkono... bao ni bao tu ili mradi refa hajaona,” alisema Nape.


Chanzo : Mwananchi



My take: Naona imefikia hatua ccm hawaogopi tena na kuthubutu kutamka hadharani kwamba wizi wa kura ndiyo tegemeo lao litakalowapa ushindi.
 
EmmaGMangwela

bora goli LA mkono utasawazisha na kuongeza LA ushindi kuliko ushindi WA mezani wakati timu zote zipo uwanjani
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…