Siku mbili zilizopita gazeti la Mwananchi katika habari yake kuu liliandika na mimi nanukuu "CCM itashinda tu hata kwa goli la mkono" Mimi binafsi hii habari ilinistua sana kwamba huyu mtu anasimama jukwaani tena kwa kujiamini anatoa kauli kama hiyo bila woga hata kidogo. Kwa nchi yenye watu makini hili halikutakiwa kupita hivi hivi, ingekuwa ni skendo kubwa, lakini kwetu hapa limeonekana kama la kawaida.
Statement kama hiyo nilitegemea vyama vya upinzani vingekuja na kauli kali kuikemea au kulaani kwa nguvu zote, lakini nimefuatilia katika vyombo vya habari hakuna kiongozi yeyote aliyekemea. Kukaa kimya kwa watu hawa kunanitia shaka na uelewa wao wa mambo ya siasa, siasa kama shughuli nyingine inabidi ujue ni wapi pa kuchukulia point na kujenga publicity, hilo hawakulitambua na fursa imewapita.
Lakini pia kauli ya Nape inatoa taswira mbaya kwa nchi yetu, kwamba cheating katika nchi yetu imeota mizizi kiasi kwamba linaanza kuonekana kitu cha kawaida, kama hivyo ndo hivyo tutatoa wapi moral authority ya kuwaonya au kuwakemea watoto wetu wasifanye cheating katika mitihani yao kama mwanasiasa kama Nape anaweza kusimama jukwaani akashadadia wizi wa kura?
Kwa kauli hiyo ya Nape ni dhahili shahiri tunafanya uchaguzi siyo kwa nia ya dhati bali ni kuwafurahisha mataifa ya magharibi ili yaendelee kutoa misaada. wanahubiri Amani na utulivu midomoni huku chini kwa chini wanapanga mipango ya wizi wa kura, hii ni aibu kubwa na haiashirii mwisho mzuri. Ndo maana wananunua magari ya washawasha na kuajili polisi wapya kila ukifika uchaguzi.
Na vyama vya upinzani inabidi vijitambue la sivyo vitabaki upinzania mpaka yesu arudi.
Nawakilisha wanajanvi