Nape na ombi la CAG kukagua mikopo; kuna watu wamepanic!

Si unaona wanavyopanic?

Hapo kaka ni zoezi la kukomoana tu, ningeona ni kitu cha maana sana chenye tija ningekua na uhakika endapo uchunguzi utagusa kila aliyehusika na hatua kali kuchukuliwa bila kuangalia mtu usoni, SIONI HILO LIKITOKEA.
 
Ukaguzi ulishafanyika serikali mpya ilipoingia kifuatacho ni kurahisha watu tu.
 
Hapo kaka ni zoezi la kukomoana tu, ningeona ni kitu cha maana sana chenye tija ningekua na uhakika endapo uchunguzi utagusa kila aliyehusika na hatua kali kuchukuliwa bila kuangalia mtu usoni, SIONI HILO LIKITOKEA.
Mkuu kuishi kwingi kuona mengi.
Mwalimu aliwahi kutufundisha kuwa, kuna wakati mwingine mkubwa akikosea na huna la kumfanya. Hapo basi kumzomea tu ni adhabu tosha!
 
Mkuu kuishi kwingi kuona mengi.
Mwalimu aliwahi kutufundisha kuwa, kuna wakati mwingine mkubwa akikosea na huna la kumfanya. Hapo basi kumzomea tu ni adhabu tosha!

Nakuelewa na tuko pamoja sana. Shida ni hata hiyo kuzomewa, wako wanaotakiwa wazomewe lakini hawatazomewa. Itaangaluwa huyu ni nani na tukimzomea itakuaje? Wengine hawatatajwa hata kuwa kwenye orodha ya kuzomewa.

Wakati huohuo wako watakaoachwa ila siku wakileta ukorofi, watakumbushwa wanatakiwa wazomewe.

Ndiomaana nikasema, zoezi ni jema lenye nia ovu. Huyo anaepiga kelele ni kwa vile hakupata vizuri sehem yake au hakuridhika. Sio kwamba ana uchungu na nchi

Si ni huyo huyo aliyetuletea msamiati wa goli la mkono kwenye chaguzi?
 
Hata kama hamdanganyiki, hata kama mnajua kila ovu; then mnavyojua mnafanya nini?
 
SUKUMA -GANG na MATAGA ndio wamepanic .,
 
NAPE ameokoka, anatubu kijanja; ila ili aende mbinguni , aachie ubunge maana ameingia kwa UCHAFUZI na si UCHAGUZI, kistaarabu tu aachie jimbo, hivi vitu anajikusanyia hatokwenda navyo peponi, atacha watu wakigombea kwenye miradhi.
 
Na Kuna mambo hayaonekani kwa macho na ndio mabaya zaidi. Utakuja kuelewa pale utakapokuja staafu na kukuta mfuko wa pensheni Magufuli alishaukwanguaga siku nyingi.

Utakuja kujua Mjamaaa alikuwa sio kabisa pale utakapolipwa 25% ya mafao yako na kuambiwa nyingine uje kuchukua baada ya miaka 12
 
Hili litawafanya MATAGA wafiche sura zao na kuacha kuiandama Serikali ya Samia

Pia ni jambo zuri pia kwa Wananchi walioaminishwa kuwa Marehemu Magufuli alikuwa Malaika mtakatifu kumbe alikuwa ni Shetani la kutisha.

All in all CAG Kichere aongezewe walinzi binafsi kwa maana akina Polepole bado wapo.
 
U$€nge Tu Bora wasifanye huo ukaguzi. Kupeana pesa za vikao vya ukaguzi halaf hamna kitu.
Unakumbuka Muheshimiwa Samia alisema ukaguzi ufanyike katika Ile miezi mwendazake alikua anaumwa. Haya nambie ile report imeenda wapi. Full ushuzzi tu.
 
Kwani kunashida gani huo upepo ukapita? Sisi ni matajiri, tunajenga kwa fedha zetu za ndani. Mbona lilipita pia, jamaa alikuwa mwongo sana sema wafuasi wake wengi walikuwa wale waliotajwa na Twaweza. Huwezi kuta mtu anayejielewa akishabikia ujinga kama ule.
 
Nape amuulize mpango sio kubwabwaja tu
 
Labda lengo lake ni fisadi kuu aliyekuwa kwenye kichaka cha unyonge ajulikane
 
Mkuu hakuna watu wa ajabu ajabu kama baadhi ya watanzania, hawana kizuri yaani mtu akiiba fedha ya umma utawasikia vijiweni wengine wakimsifu kuwa fulani ni mwanaume aisee amepewa nafasi hajafanya kosa na sasa hivi ni tajiri. Wengine utasikia oooh jamaa anajidai na mali za wizi alizokwapua kwenye mradi wetu wa maji au barabara vijijini. Sasa kimbembe jamaa huyo huyo akikamatwa ukimwambia njoo utoe ushahidi anakataa kata kata ila muite sasa kutoa ushahidi wa uongo yaani atakuja fasta.
 
Hao waliopita lini waliwahi kusema wao ni wasafi na wasema kweli? Huyo aliyekuwa Rais wa wanyonge ndiyo alikuwa anasema yeye anachukia ufisadi na ni msema kweli. Sasa akichunguzwa kuna shida gani? Wanyonge mnatakiwa mjue ukweli kuhusu aliyekuwa Rais wenu ili mjue ni jinsi gani aliwapambania.
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…