Kwanza niseme tu wazi mimi sio mtaalam wa mambo hayo, hivyo yeyote anayeona zaidi ya mimi, please come up!
NAPE AKISUKUMWA NA KUTOLEWA BASTOLA NA 'jamaa '
Yule kijana wa shati jeupe aliyemfungulia Nape mlango wa gari hayuko sawa.
Amefungua mlango kama mlinzi, halafu within seconds akawa mtalii.
Akaja yule tall mwenye kofia, kaombwa kitambulisho akapiga hatua tatu nyuma na kuchomoa bastola.
HUYU TALL
Hatua za nyuma kazipiga kifala, I can do better.
Inaonekana mkono wake wa nguvu ni wa kulia ila bastola na pingu, vyote kaviweka upande wa kushoto.
Ametoa bastola kijinga kweli, na bila sababu, maana hata baada ya kuitoa hakuitumia.
Baadae akaanza kumsukuma Nape aingie kwenye gari, hakuwa na intent maana alikuwa upande dhaifu wa Nape na bado hakufanikiwa.
Akaja mtu aliyeonekana kama Maulid Kitenge, alimzidi nguvu na hoja yule tall ndani ya sekunde chache mno.
Yule tall anaonekana kama one of the dark vampire, KUMBUKA ULIMBOKA, maana baada ya kuona watu na magari yanazidi akavanish into the masses.
Back kwa 'mlinzi' wa Nape ,the guy sio mlinzi kabisa
Kwenye kiuno alionekana kama ' kabeba ' ,kuna wakati nilimsikia Nape akimruhusu afanye fujo lakini jamaa anacheka tu!
Otherwise kwenye clip ya pili Nape aliperform vizuri. Jazba haikumchukua kiivyo!
Wewe umeonaje.