UTAFITI MCHANA KWEUPE...
nimeitazama [HASHTAG]#clip[/HASHTAG] ya Mh. Nape Nnauye (MB wa Mtama) alipotishiwa [HASHTAG]#bastola[/HASHTAG]. Nimejifunza haya:
1. Nape amekomaa na ni kijana jasiri.
2. Nape ni mwanasiasa anayeijua siasa.
3. Nape amesimamia anachokiamini.
Hata hivyo, kwa upande mwingine nimepata nafasi ya kumuona mtu (aliyevaa jeans na kapelo) akimtolea bastola Nape. Mtu mwenye bastola anaonekana ni [HASHTAG]#mwoga[/HASHTAG] kwa kuwa Nape hakuwa [HASHTAG]#adui[/HASHTAG] wala hakuwa na silaha.
Nimejifunza kwamba, nchi hii kama Nape (ambaye aliwahi kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM) ametolewa bastola mbele ya watu mchana kweupe; kuna uwezekano mkubwa kwa watu wa kawaida kuuawa na kutupwa kama mbwa.
Nchi inaelekea kwenye [HASHTAG]#anarchy[/HASHTAG] na wanaoipeleka huko watakuja kuvuna [HASHTAG]#upumbavu[/HASHTAG] wao. Mwisho wa utafiti huu wa mchana kweupe. Nampongeza Nape kwa kutoogopa bastola na kutomuogopa aliyewatuma waliyekuja na silaha kuzuia #press_conference yake Protea Hotel.