Nape Nnauye atishishiwa Bastola na kusukumizwa kwenye gari

Shujaa wa leo ni kitenge sasa ajiandae kusingiziwa madawa ya kulevya na mapacha wawili.
Jamaa kafanya kazi kubwa sana, Nape alikuwa anasukumizwa ndani ya gari kama tenga la nyanya vile. Kitenge kaokoa jahazi.
 
Shujaa wa CCM aliyekataliwa na kudhalilishwa na wa chama chake! Iwe fundisho!
 
Aibu kubwa sana kwa maafisa usalama wote, kamanda siro muangalie kijana wako laa sivyo itakuwa zamu yako kutumbuliwa.
 
Na wakamshikia bastola katika nchi yenye democrasia kama Tanzania

Na bado tunaimba nchi ya amani!!! Watu wanatishiana kwa bastola; Nape alimwambia ajitambulishe akakaa kimya, je angekuwa jambazi anataka kumteka? Kitendo hiki chote kinahitaji investigation ya kujua kwanini kimetokea kwa waziri aliyetumbuliwa ambae alikuwa hata bado kukabidhi ofisi!!
 
Sometimes hawa ndugu zangu wanausalama wanakuwa kama wameshikiliwa akili
 
CCM mlizani ni kina Lema tu ndiyo wataburuzwa na mtutu wa bunduki.

Shime wana CCM jioneeni mwenyekiti wenu anavyowafanya bila huruma na mlimpigania kweli leo anawageuka wakati mnatenda haki
 
Siku hizi haombi tumuombee!
 
Ujasiri aliouonyesha Maulidi Kitenge katika sakata la Mh Nauye ni wa ajabu. Waandishi wote na mamia ya watu waliokuwepo waliufyata huku wakishuhudia Mh Nauye akirudishwa garini kibabe na vijana wanaodhaniwa ni Usalama wa taifa tena wakiwa tayari walishaonyesha wazi kuwa wana bastola ila Kitenge akiwa ndani ya Suti alitumia nguvu na busara kuzuia jaribio lile akoshirikiana na mlinzi mmoja wa Nape

Source; Video za tukio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…