Nafikiri umepata jibu la swali ulilouliza kutoka kwa wadau hapo juu.
Mie hoja yangu ni hii... Mbona leo umeweza kuhukumu kabla hata ujajua ni nini kilichopelekea yote haya? Ni ajabu sana leo eti hujapendezwa kuona hiyo bastola (tena kamoja tu) ikitolewa nje nje... wakati juzi hapa tuliona sote askari wa aina tofauti wasio na magwanda na wenye magwanda ya kijeshi wameshika silaa kubwa kubwa za kivita wakiongozwa na rc saa nne usiku wakiingia kwenye private premises, wewe mwenzetu ukatuambia kuwa huoni uvamizi wala shari yoyote ya lile tukio, kana kwamba kungeweza kukawa na explanation nyingine ya kawaida kabisa ya lile tukio...ambayo sijui ni ipi kwa mfano... Hueleweki ndugu.