Nape Nnauye atishishiwa Bastola na kusukumizwa kwenye gari

Nape Nnauye atishishiwa Bastola na kusukumizwa kwenye gari

Hawa ndio wale tunaopiga kelele kula siku kuwa wana ZERO ila wanabebwa.

Yaani Huyo jamaa akili zake ni chache kama za Bashite.

Ameshangaza Dunia.

Ni aibu kwa taaluma nzima ya usalama,kwa mwanausalama kumvamia kiongozi bila ya kujitambulisha na kuonyesha kitambulisho na kuanza kumtisha kwa bastola ili atii amri yako.

Nakushauri kamanda Sirro umrudishe uyu kijana akasome vizuri sheria za usalama kuliko kulitia aibu jeshi la polisi.
ae9d14574e3bbed226f3c2cf1d2f8bf7.jpg
217b388a8e7c271a658257fd2558bced.jpg
 
Nashauri kama kuna msanii wa bongo fleva anataka aachie ngoma yake kali kwelikweli, basi asubiri kwanza hii movie iishe ndio atoe.
ndio maana harmorapa ameamua kwenda sambamba na kasi ya hili tukio.
 
UTAFITI MCHANA KWEUPE...
nimeitazama [HASHTAG]#clip[/HASHTAG] ya Mh. Nape Nnauye (MB wa Mtama) alipotishiwa [HASHTAG]#bastola[/HASHTAG]. Nimejifunza haya:
1. Nape amekomaa na ni kijana jasiri.
2. Nape ni mwanasiasa anayeijua siasa.
3. Nape amesimamia anachokiamini.

Hata hivyo, kwa upande mwingine nimepata nafasi ya kumuona mtu (aliyevaa jeans na kapelo) akimtolea bastola Nape. Mtu mwenye bastola anaonekana ni [HASHTAG]#mwoga[/HASHTAG] kwa kuwa Nape hakuwa [HASHTAG]#adui[/HASHTAG] wala hakuwa na silaha.

Nimejifunza kwamba, nchi hii kama Nape (ambaye aliwahi kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM) ametolewa bastola mbele ya watu mchana kweupe; kuna uwezekano mkubwa kwa watu wa kawaida kuuawa na kutupwa kama mbwa.

Nchi inaelekea kwenye [HASHTAG]#anarchy[/HASHTAG] na wanaoipeleka huko watakuja kuvuna [HASHTAG]#upumbavu[/HASHTAG] wao. Mwisho wa utafiti huu wa mchana kweupe. Nampongeza Nape kwa kutoogopa bastola na kutomuogopa aliyewatuma waliyekuja na silaha kuzuia #press_conference yake Protea Hotel.
Endeleeni na talalila zenu sie tukipiga hatua.
 
Yule polisi kanzu ni mshamba wa bastola, ngoja Magufuli aione hiyo video kama hajamtumbua
 
Tusubiri mashtaka yake kwa kuzuia serikali kufanya majukumu yake... Hii ndio Tanzmania
 
Matumizi ya silaha za moto katika awamu hii hayabagui kabisa. Uwe CCM , uwe Clouds FM utalimwa risasi tu. Hii ndio awamu ya tano.

Wote tunashuhudia haya wanafanyiana wao kwa wao

Wana hamu ya kuzitumia silaha za moto
Wana hamu ya kupiga risasi wale wote wasiowataka
Wana hamu ya kuwapiga risasi marafiki zao
Wana hamu ya kushurutisha watu kwa mtutu wa bunduki
Wana hamu ya kuwapiga risasi wapinzani
Wana hamu ya kuwapiga risasi raia wasio na hatia

Wana hamu kwa sababu wamepewa jeuri ya kutumia risasi kuwapiga WANANCHI kwa kuwa hao watoa amri ndio WENYE NCHI

Nape siwezi kukupa pole wala kukuonea huruma hata chembe maana malezi mabaya ya mtoto wa kupewa lawama huwa ni mzazi. Na wewe Nape ni mzazi wa CCM haijalishi ujana wako wewe ni mzee tu umeshailea vya kutosha wewe ni mzazi wa CCM acha upigwe tu ndio ujue wenzako walikuwa wanaumia namna gani .
 
Yule police amefanya makosa sana na atafukuzwa kazi why amuonyeshe mtu bastola nini kitu alichofanya hapo NAPE??nadhani hatua za kinidhamu inabidi zichukuliwe kwa huyo kijana mara moja
 
Masikini Harmo rappa akawa kama Petro wa Biblia , bastola ilipotolewa na askari yule mjinga alikimbia, nasikia amekutwa Chalinze bado anachanja mbuga.
Jioni hii nilisikia East Africa Radio wakisema ameonekana Morogoro. Inaonekana huyu jamaa ni mkali wa Marathon.
 
Kwako unaona joto ya jiwe
Lakin hujui ina mana gani hilo tukio kwa nchi...
Ina maana kubwa sana.....nadhani iktokea raia wanauawa kwa silaha hakuna msaada labda aseme mkuu...otherwise nchi haina direction....no vision
 
Dah!

Mimi si mpenzi wa CCM na si shabiki wa Nape ila hicho nilichokiona kwenye hiyo video sijakifurahia.

Kwangu haki ni haki tu.

Ni nini hasa kilipelekea yote hayo?

Kuna anayejua humu anieleweshe zaidi?
Nafikiri umepata jibu la swali ulilouliza kutoka kwa wadau hapo juu.

Mie hoja yangu ni hii... Mbona leo umeweza kuhukumu kabla hata ujajua ni nini kilichopelekea yote haya? Ni ajabu sana leo eti hujapendezwa kuona hiyo bastola (tena kamoja tu) ikitolewa nje nje... wakati juzi hapa tuliona sote askari wa aina tofauti wasio na magwanda na wenye magwanda ya kijeshi wameshika silaa kubwa kubwa za kivita wakiongozwa na rc saa nne usiku wakiingia kwenye private premises, wewe mwenzetu ukatuambia kuwa huoni uvamizi wala shari yoyote ya lile tukio, kana kwamba kungeweza kukawa na explanation nyingine ya kawaida kabisa ya lile tukio...ambayo sijui ni ipi kwa mfano... Hueleweki ndugu.
 
nape angaamua hapo angemsukuma tu adondokee huko alafu tuone anafanya nini? anatoa bastola mchana kweupe mbele za watu hapa nchin tz? amefundishwa kweli huyo? hahaha. hivi wanafikiri hii nchi ni kampuni yao wanaweza kuifanya lolote?
Yani kaonekana fala tu bora hata angepiga juu basi tujue alikua anatawanya watu,

Yani katoa bastola halafu hajaitumia alafu nape anamuangalia kwa dharaaau huku kaweka mkono mifukoni yani bonge ya dharau.
 
Back
Top Bottom