Kitenge katoa wapi ile OVER CONFIDENCE? Anaonekana kama anampiga mabit jamaa wa Usalama!Jamaa kafanya kazi kubwa sana, Nape alikuwa anasukumizwa ndani ya gari kama tenga la nyanya vile. Kitenge kaokoa jahazi.
Kwa mazingira hayo huyo hawajibiki kwa Kamanda Sirro kabisa na wala hapokei command ya kamanda Sirro.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]Nani asiyejua uaskari ni kazi ya kina Bashite huwezi kushangaa hilo
Hii haiko sawa kabisa!! Huyo ni nani mwenye pistol??
Haapa alivyotolewa bastola, Msanii Harmorapa naye alikuwepo hapo ila alitimua mbiop baada ya Bastola kuonyeshwa
Ni maisha ya Kisiasa ila la leo ni ubabe wa hadharani MAGUFULI NI DIKTETA MKUU NA MSAIDIZI WAKE MAKONDA[emoji21]Mzee wa goli la mkono limemrudi!!!.....Malipo ni hapahapa!!!
Nafikiri umepata jibu la swali ulilouliza kutoka kwa wadau hapo juu.
Mie hoja yangu ni hii... Mbona leo umeweza kuhukumu kabla hata ujajua ni nini kilichopelekea yote haya? Ni ajabu sana leo eti hujapendezwa kuona hiyo bastola (tena kamoja tu) ikitolewa nje nje... wakati juzi hapa tuliona sote askari wa aina tofauti wasio na magwanda na wenye magwanda ya kijeshi wameshika silaa kubwa kubwa za kivita wakiongozwa na rc saa nne usiku wakiingia kwenye private premises, wewe mwenzetu ukatuambia kuwa huoni uvamizi wala shari yoyote ya lile tukio, kana kwamba kungeweza kukawa na explanation nyingine ya kawaida kabisa ya lile tukio...ambayo sijui ni ipi kwa mfano... Hueleweki ndugu.
Hawa ni askari polisi upelelezi siyo wa TISS. Wale wa TISS wanafundishwa vyema na wana adabu na wala hawawezi kutumwa kwenye mission ya wazi namna hiyo.Mara zote nimekuwa na mashaka sana na maaskari wetu hasa waliofuzu katika kipindi cha miaka kumi iliyopita. Sina hakika kama ni sababu ya nyadhifa na nafasi walizokuwa nazo wazazi wao au ni kiburi tu binafsi.
Miaka iliyopita mpaka ukamjue fulani ni askar wa Usalama wa Taifa ilikuwa ni shughuli pevu ila ikaja kuwa kinyume kwa kipindi cha miaka kumi na miwili, mtu alikuwa na uwezo wa kuanza kujigamba tu mkiwa bar au pahala popote penye mkusanyiko wa watu kuwa yeye ni usalama wa taifa au akaitoa kabisa silaha aliyonayo kwenye hadhar, binafsi simshangai huyu askari mpumbavu.