Nape Nnauye atishishiwa Bastola na kusukumizwa kwenye gari

Nape Nnauye atishishiwa Bastola na kusukumizwa kwenye gari

Mara nyingi sana tumezomea kuona Jeshi la Polisi wakitumia nguvu kubwa sana kupambana na upinzani kuliko kutumia akili au njia sahihi katika kutimiza wajibu wao huo.
Kitendo ambacho kimefanywa leo na Afisa wa Jeshi la Polisi kuonyesha bastola hadharani kinatakiwa kulaani na kupingwa kwa nguvu zote.
Aliyekuwa Waziri wa Habari na Utamaduni na michezo Nape Mnauye akifika maeneo ya hotel kwa ajili kufanya mkutano na waandishi wa habari jambo la kushangaza baada ya hapo Afisa wa Jeshi la Polisi alimfuata na kuzuia wakati Nape Nnauye anamwambia Afisa wa Jeshi la Polisi atoe kitambulisho chake yeye Afisa badala ya kutoa kitambulisho ndo akatoa bastola.
Ni tukio la kulaani sana kwenye nchi kwani ni muda wiki sasa baada ya tumeshuhudia tukio la kituo cha Clouds kuvamiwa na Rc akiwa na ulinzi na askari wenye silaha .
Anaruhusiwa na sheria, kama unaona wivu kaajiliwe huko nawe!
 
Makada wa ccm ndio mjifunze sasa kwa tukio la leo.msijifanye muda wowote ccm inawageuka.
 
Hivi kabisa hii ya leo Nape kunyooshewa bastola kwa namna ile unaweza kulinganisha na jinsi Makonda alivyoingia casually pale Clouds na wale askari?

Kabisa unaweza kulinganisha?

Nani pale Clouds alinyooshewa mtutu wa bunduki kama ilivyotokea kwa Nape?

Nani pale Clouds alikuwa roughed up kama ilivokuwa kwa Nape leo?

Nani?

Utakuwa zuzu kabisa wewe kama utayalinganisha haya matukio mawili.

Wengi wenu nyie mna akili duni sana aisee.

Dumb like a bucket of rocks.

Halafu wala sijahukumu na ndo maana nikauliza hayo maswali niliyouliza kama nilivyouliza kwenye ishu ya Clouds.

But again if you are dumb as a bucket of rocks you wouldn't see any difference.
Chaaaa... Mbona mapovu yakheee! Kwa hiyo ukiniita dumb, sijui akili duni, sijui nini automatically inakufanya wewe mwerevu sana kwa mfano... Pathetic!
 
Ni aibu kwa taaluma nzima ya usalama,kwa mwanausalama kumvamia kiongozi bila ya kujitambulisha na kuonyesha kitambulisho na kuanza kumtisha kwa bastola ili atii amri yako.
Nakushauri kamanda Sirro umrudishe uyu kijana akasome vizuri sheria za usalama kuliko kulitia aibu jeshi la polisi.



Haapa alivyotolewa bastola, Msanii Harmorapa naye alikuwepo hapo ila alitimua mbiop baada ya Bastola kuonyeshwa


Aah, Maulid Kitenge the negotiator namuona ndani ya koti jekundu.
Ila kiukweli hii haiko sawa, sina uhakika kama hawa jamaa wanajua ethics za kazi zao. Huwezi toa tu bastoli mbele za watu tena ukiwa na lengo la kumuonyesha aliyekuwaga waziri hata masaa kumi hayajapita, haiko sawa kabisa!!
 
Dah hii siku ya leo nimeumia sana nlvyomsikia nape anaongea lakini harmorapa kaniacha hoi ikanibidi tu nicheke daah
 
Hawa ni askari polisi upelelezi siyo wa TISS. Wale wa TISS wanafundishwa vyema na wana adabu na wala hawawezi kutumwa kwenye mission ya wazi namna hiyo.
Soma unielewe kaka, wapo wa TISS ni wajinga huwez kufikiria kama ni wao ingawa ni wachache, walisumbua sana kipindi cha katikati hapo
 
Hawa ni askari polisi upelelezi siyo wa TISS. Wale wa TISS wanafundishwa vyema na wana adabu na wala hawawezi kutumwa kwenye mission ya wazi namna hiyo.
nani kakudangany.hao tss
 
Inanipa wasiwasi mkubwa kumuelewa kama yule ni usalama au ni mamluki ya usalama.

1. Kwanini amekuwa short tempered ndani ya sekunde mpaka kutoa silaha?
2. Nape nI hatari kiasi gani pale?, mpaka kuwe na usalama zaidi ya watatu ambao silaha zao zote zinaonekana kiunoni?
3. Kama ingetokea Nape kugoma, angeweza kutimiza lengo lililomfanya kutoa silaha?
4. kama ilikuwa ni lazima Nape asifike pale, wameshindwa nini kumzuia toka huko barabarani?
 
Afisa usalama yule hakika ametushtua kwa kiasi kikubwa nakumbuka mwaka juzi mitaa flani Mwanza walirushia risasi kati ya askari polisi na afisa usalama mmoja ila wengi nahisi ni "vichaa"
 
Back
Top Bottom