Pre GE2025 Nape Nnauye: Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza, ili mradi ukimaliza unasema Mungu nisamehe!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wala usiogope! Muulize Mange Kimambi. Hana hamu nao hao. Mkwara mwingi mitandaoni, lakini D-Day ikifika, utacheka zaidi ya Standing Comedies za Kibongo!
Unamcheka nani? Waliotukanwa ng'ombe wakajificha kisa ni wengi au wachache walioandamana kupinga kuitwa ng'ombe?. Tumia akili kabla ya kuropoka.
 
Huyu asilete mambo ya kitoto kwenye uongozi wa nchi. Nakumbuka enzi za idi amin alisema jambo la uongo dhidi ya Tanzania. Alipobanwa kwenye mkutano na viongozi wengine akasema alikua anatania. Mwalimu nyerere akaonya nchi hua hazitanii. Kwa hivyo Nappe hakika haitendei sawa nafasi ya uwaziri.
 
chadema walichekelea kifo cha mzalendo mleta maendeleo... mimi niliwaambia haya yanayo kwenda kutokea ....ukweli ni kwamba samia anakwenda kuangamiza taifa
 
Hajawahi kuwa na akili hata siku moja
 
Naona jamaa kasikia anatemwa ndio maana ameona aropoke tu
Liwalo na liwe
Jamaa mshamba sana huyu
Kwa hiyo anakusudia dhambi halafu anatubu
Sijui anaamini Mungu gani huyu
Wengi huwa ni mkumbo kwenye dini ila wanaamini shetani
 
Daah....! Kila kitu mungu. Mungu ametupa afya njema, ametupa utashi wa kutambua baya na zuri, Haki na batili. Anyway Tanzania itakombolewa siku hiki kizazi Cha machawa na waoga kitakapofutika hapa duniani... Yaan hebu fikiria mtu amekuja akaanza kukutukana mbele ya mke wako na watoto wako... Utasema namwachia mungu...? Umelala nyumbani na wala hujishughulishi utasema mungu niletee chakula?...... Duuh...? Kazi kweli kweli. Watanzania tunazidiwa utashi hata na wanyama...! Hata paka ukimubana kwenye kona mwisho wa siku atakuvimbia. Sisi ni viumbe wa aina Gani...? Tunadharauliwa na kutukanwa waziwazi, tunakejeliwa hadharani. Ama kweli watanzania, sisi ni wafu na wala sio viumbe hai.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…