Nape Nnauye: Mwenyezi Mungu ameamua ugomvi

Kwani ni uongo? Si ndio ukweli wenyewe huo au? 😆😆
 
Kimaadili ya kiuongozi hili halipo sawa, inaonyesha Nape pia hakui pamoja na changamoto alizopitia, anasahau kwamba huyo Magu anayemtuhumu angeacha mpira udunde wenyewe kwenye uchaguzi uliopita hata yeye asingekuwa mbunge. kifupi hiyo mbegu wanayoipanda lazima wataivuna japo kwa sasa wanaona kama mzaha tu kukejeli wenzao.
 
Acha upuuzi,kusemana alianzisha Mwendazake acha asiginwe hadi akili zikae sawa.
 
Heee... Kama upo nje ya nchi hongera...

Mimi ni shuhuda wa haya... Na sio kesi za kisiasa....
Unaambiwa futa hii kesi hata kama umeonewa.. Ukileta ujeuri usitulalamikie.. YAMENIKUTA HAYO
😅😅duuh
 
Ni watu wa chama kile au watu wa Chama Chako?? Mbona unaongea kama vile ni chama cha ACT😅😅
 
Mkuu kama angeacha mpira udunde wenyewe asingekuwa mbunge.. Ni kweli..
Na kama unakumbuka mpinzani wa Nape aliswekwa rumande wiki nzima ili asirudishe fomu...
Je, huoni ni lazima Magufuli asemwe ili liwekwe kwenye kumbukumbu... Na vizazi vijavyo vijue na lisijirudie tena?
 
wabongo wengi waliotamani kuona Nyerere Dam na SGR vikiwa mzigoni bado hawaamini kama chuma Magufuli amekufa, bado hawaelewi Magu alikufa lini, bado hawaelewi kipi kilimuua? wanapenda kujua nani walikuwepo wakati Magu akifa? jitihada kiasi gani zilifanyika kuokoa uhai wake? haya maswali kuna siku moja hata ipite miaka mia majibu yatapatikana!!

Halafu ni ujinga kufurahi binadamu mwenzio kufa maana njia yetu ni moja tu!! hata kobe wanaotoboa miaka 200 nao one day wanadedi, hivi nani kati yetu anajua atakufaje? atafia wapi? je mnakumbuka wale wazungu ambao Islamic State kule Iraq walikuwa wakiwachinja hadharani kwa kurekodi video? je wale jamaa wakiwa huru walijua one day watachinjwa?

Unaposhiriki mazishi ya mtu ni muda wa kujiuliza nawe mazishi yako yatakuwaje!

Ni wakati sasa JPM aachwe apumzike
 

Nape Nnauye na Maza Lao ni moja kuhusu marehemu.​

Bora Nape ni mkweli Ana kibali kulisema la rohoni, Maza anapiga kimya.​

Kuna siku Dr Bashiru anasema ukweli kuhusu kifo cha JPM watanzania hawataamini.​

Hakuna mwenye akili timamu wa kumuamini Bashiru,ni mwizi tu yeye na polepole walipiga hela sana kwenye ile biashara haramu ya kununua wapinzani uchwara ni wahuni tu
 
Lazima tuwaze JANA ili kuifanya LEO na KESHO yetu kuwa BORA ZAIDI. Ikiwa hujui utokako (JANA) utafahamu vipi ulipo (LEO) na uendako (KESHO).Ikiwa hujui wapi tatizo lilipoanzia huwezi kupata utatuzi juu yake. Hatma bora huja kwa kurekebisha jana yetu.

Hivyo basi, mema husafiri POLEPOLE lakini hudumu vizazi, mabaya husafiri kwa KASI zaidi hufutika mapema moyoni.

Tujitathimi jinsi tunavyoishi na wengine,duniani sote tuko njiani.

MIAKA 80 IJAYO WATAKAOKUWA HAI HUMU JUKWAANI NI WACHACHE MNO,AU WASIWEPO KABISA.
 
Wakati magu anawashambulia kwa kejeli matusi na lugha za Kidhalilisha majukwaani watu, mlishangilia huku mkisema ni sawa tu...Leo watu wanatoa nyongo mnawaona wabaya tena. Wapuuzi.
 
Huu upuuzi si wa mbayuwayu Nape wa kulaumiwa ni viongozi wakuu wa nchi. Ndo wa kumwambia Nape afunge domo. Fitina zinawatafuna kiukweli ila zitawagharumu .system nzima iko against Magufuli its sickening wanavyopambana na marehemu kwa ajili tu ya vyeo .
 
Alimtembeza kwa miguu Ikulu ya DSM
 
Sio kila kitu unakihusisha na chama kwani huyo ndugu yako Nape ni msemaji wa chama?. Acha dhana jumuishi ndugu yake Nape.
 
Hakuna mtu nimewahi kusoma sehemu yoyote akikejeri kifo Cha Hitler Wala Idd Amin, HAKUNA!

Kwanza Hitler aliamini hawezi kuuliwa na ni vigumu Sana yet kufa, aliwahi hata kutaja hadharani kwamba yeye hawezi kufa,
Kwahio kama wewe hujawahi kusoma hio kejeli ya Hitler then tukusaidiaje?
 
Uzuri huyo marehemu yeye ndie alikua wa kwanza kuwananga wastaafu wenzake hadharani, kabla yake yeye wastaafu walikua hawasemi wenzao hadharani.Acha anyweshwe dawa aliyo itengeneza mwenyewe huko alipo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…