Nape Nnauye: Mwenyezi Mungu ameamua ugomvi

Naungana na Nape kwenye hili, yuko sahihi kwa asilimia mia moja.
Mabaya ya mtu yanaporudiwa kusemwa mara kwa mara inakuwa ni somo/funzo kwa wengine ya kuwa mwisho wa ubaya ni aibu, hii aibu anayoipata pamoja na nguvu kubwa inayotimika na wanufaika wa utawala wake au wale waliofurahia kuuawa, kutekwa, kujeruhiwa na kuteswa kwa Watanzania wenzao kukingia kifua udhalimu wake usiwe unazungumzwa lakini daima watu hawatasahau madhila aliyowasababishia.
Mnaopigania mazuri yake yasemeni lakini pia muwaache na wanaokumbusha mara kwa mara kuhusu mabaya yake waseme pia, hiyo ndiyo demokrasia.
 
Acheni ujinga. Nyie mbona kila kukicha mnamsema vibaya Idd Amin au Hitler? Ukizuia watu wasikuseme ukiwa hai watakusema ukiwa mfu.

Kupanga ni kuchagua
Hii ndio Afrika kila uchao ni unafiki.
Watu waseme yaliyojaa mioyoni mwao.
Utamaduni wa kufungana midomo utazaa watu kuviziana na bunduki ili kuupa moyo ahueni.
 
Ni watu wa chama kile au watu wa Chama Chako?? Mbona unaongea kama vile ni chama cha ACT[emoji28][emoji28]
Lini mimi nikawa mwanachama wa chama cha siasa? Sijawahi na sitegemei! Vyama vina unafiki ambao siuwezi nitaporwa kadi siku hiyo hiyo.
 
Tunamsubiri huku Kanda ya Ziwa ili tumpopoe.
 
Uzuri huyo marehemu yeye ndie alikua wa kwanza kuwananga wastaafu wenzake hadharani, kabla yake yeye wastaafu walikua hawasemi wenzao hadharani.Acha anyweshwe dawa aliyo itengeneza mwenyewe huko alipo.
Hii habari itaipeleka sisiem jalalani 2025
 
Wacha asemwe alifanya nchi kama baba yake mjinga yule tulikuwa kama watumwa kwenye nchi yetu .wacha mungu aitwe mungu kafanya muujiza kukyekelea mbali kichaa
 
Shida kubwa ni kwamba Mwendazake alizuia watu wasimseme kwa mabaya yoyote na kulazmisha asifiwe na kila mtu, Hivyo watu walishaishiwa maneno ya kumsifu wakabakia na mabaya yake tu, ndo sasa wanayaongea!
Binafsi sijaona ubaya wa kauli ya Nape maana wapo hata waliosema kuwa Tanzania chini ya utawala wa mwendazake ilikuwa hatarini kukumbwa na mapinduzi dhidi ya serikali iliyokuwa madarakani, ni mapinduzi ambayo ambayo kama yangetokea lazima yangeambatana na athari mbalimali ikiwemo watu kupoteza maisha, uharibifu wa mali na kuvurugika kwa mifumo ya uzalishaji mali na hivyo kupelekea athari kubwa za kiuchumi. Hii ni kwasababu Binadamu hata siku moja hakuwahi kuzowea shida hivyo ukimlazimisha kuishi maisha ya dhiki, awali atakuvumilia lakini uvumilivu wake huwa una ukomo!
Hivyo kifo cha Mwendazake ni dhahiri kilitupitisha katika mapinduzi salama dhidi ya serikali iliyokuwepo!
 
Ndio tatizo la kujifanya Mungu mtu ukifa lazima watu watakusema vibaya tu. Sio vyema mtu kujifanya ndio mjuwaji kuliko wengine, ujeuri mwingi huku ukijimini kama hii dunia na vilivyomo vyote uliviumba wewe hivyo hakuna cha kukubaisha wakati wewe ni mpita njia tu kama viumbe vingine tena kwa bahati mbaya hujui siku yako ya kuondoka.
 
Ila kina Nape haya maneno ya shombo yatawacost ikitokea Rais Ajaye akawa na akili atawapiga chini wote

Ningekuwa Rais uchaguzi ujao Kuna majimbo Bora niwape wapinzani tu, Nape ni mropokaji
halina akili hilo bila kujua kuwa linawachongea wenzake
 
Mimi mwenyewe sitokaa nisimulie jema la huyu mwendazake maana katesa wengi nikiwemo Mimi! Huyu ingekuwa ni amri yangu sote tulioteswa nae iwepo siku maalum ya kwenda kulichapa viboko lile Kaburi lake.
Alinivunjia nyumba yangu kishenzi sana huku akijinasibu kuwa hatukumchagua...akaenda mbali zaidi kuwa wale wa kule kanda aliyotokea walipwe fidia hata kama wamejenga kwenye hifadhi ya barabara!!!!
Wewe unateseka ukiwa pande zipi kwa kauri hii ya Mh Nape?
 
Kwa hiyo mzee nape yale magoti uliyompigia na yale machozi kumbe ilikuwa fix eee aka funika kombe siyo !!!
 
Hatuwezi kumpunzisha Dikteta alikuwa anaharibu Nchi yetu kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Isingekuwa Mungu kuingilia kati pale 17 Machi, 2021 huyu Magufuli angeifanya Nchi yetu iwe kama Zimbabwe kiuchumi, au Somalia kijamii au Rwanda Burundi kisiasa.


Tutaandika mpaka Dunia ielewe kuwa mtu aliyedanganya wajinga kuwa ni mchukia ufisadi yeye ndiye alikuwa FISADI mkuu
 
Mungu fundi sana
 
Tena we mleta maada umeendelea kumuheshimu kumuita ndugu nape Yani huyo anapaswa umuite wewe nape wewe sio ndugu nape.
 
Mimi nilikuwa namaanisha ethics za uongozi, hutakiwi kuendelea kulalamikia mambo ya nyuma rather ni kutakiwa kuona namna ya kusonga mbele. Na la pili wote wawili ni zao la uongozi haramu na chama chao. Hivyo hana moral authority ya kumlaumu mwenda zake kwa kiwango hicho.
 

Nape Nnauye: Mwenyezi Mungu ameamua ugomvi ila alichofanyiwa JPM na CCM ni uhaini.​

 
Nape bwana, sometimes huwa ana make sense!
Marehemu hakuwa na chembe ya busara katika kumchana mtu, hope haya yatakuwa hayamuumizi huko aliko coz naye alikuwa typical tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…