Nape Nnauye: Rais Samia Suluhu aendelee mpaka 2030

Kwa Mujibu wa katiba iliyopo haiwezekani kwenda hadi 2030.

Awamu yake hii ya kwanza ,endapo chama kitampitisha 2025 basi ndio itakuwa term ya mwisho ya pili.
 
Legacy hailiwi. Unadhani familia yake itakula legacy. Kumbuka siasa ni ajira na huwezi kuchezea ajira. Hata upinzani hawatafuti legacy bali ajira, wanapoipata ajira kama ubunge wanatakiwa kuishikilia vizuri.
 
Jamani Nchi yetu ina matatizo sana ina Viongozi ambao hawatumii akili zao kupata wanachotaka badala yake wanatumia tabia iliyojengeka Awamu hii ya sifu unufaike au pinga upotee. Huyu ni Mbunge na aliwahi kuwa Waziri anamsifu na kushauri, kwa maneno tu ya Rais, aongezewe Kipindi kingine Kiongozi ambaye hata mwezi mmoja wa Kipindi hiki alichopo madarakani hajamaliza. Mtu hatathiminiwi kwa maneno anayotamka bali kwa matokeo ya mchango wa maneno yaliyotamkwa, lazima kuwe na muda wa kutosha kufuatilia utekelezaji wa yaliyosemwa. Mnauye angeeleweka kama angependekeza mwezi mmoja kabla ya Mheshimiwa Rais kumaliza Kipindi hiki cha uongozi wake maana sote tungekuwa tumeona matokeo ya maneno ya Rais. Kipindi cha Kwanza cha Awamu ya Tano, Mwendazake na mrithi wake walitamka na kuagiza mengi sana ya kuleta Tanzania Mpya itakayokuwa kama Ulaya na MaCCM yakaimba sana "mi5 tena" na mbinu mbalimbali zikatumika kuhakikisha hilo linatokea na matokeo yake tumeona Mwendazake anaenda zake akituacha na Tanzania yetu ileile na watu wake hali mbaya zaidi.
 
Sifia sana lakini cheo hupati,ulishaharibu kabla.Rekodi zipo.
 
[emoji3516] Hii ni dalili wazi kwamba wote walikuwa wanaimba pambio wakijua wazi.kabisa yanayofanywa na Mungu mtu sio halali! Lakini hapkuwa na wakusemea lolote.
Nadhani huko.aliko Huyo Mungu anayasikia !!
 
Kweli CCM ni ile ile! Unafiki kwa kwenda mbele!
 
Samia asipokuwa makini na Wana siasa wa nchi hii atapoteana mapema Sana.

Kuwa Rais sio kitu Cha kitoto.


Aamini tu kwamba hadi Sasa Kuna watu hawaamini kama yeye Ndio Rais ama wao wataweza kuongoza nchi wakiwa nje ya mfumo.

Unataka Rais aongoze hadi 2030 kwani Katiba hajaisoma huyu Nape?

Viongozi wetu wengi wanajipendekeza Sana hadi Aibu.
 
Wazee wa mapambio wameanza
 
Mbona wanamnanga marehemu hata kabla hajaoza huko aliko? Si wangesubiri hata tumalize maombolezo?
 
Nape amesahau hana tena Godfather.

Sidhani atamrubuni SSH,Lakini ajikite kwenye Chama,yawezekana akasikika na kulamba nyadhifa za serikali.
 
Goli la mkono linamtesa huyu ndugu wa kijani

Unafiki unamtesa huyu mganga njaa. Huyu akiwa Waziri ndio alifungia television zisioneshe shuhuri za Bunge!! Leo hii ukimuuliza sababu ya sera ile na faida yake kwa wananchi hawezi kujibu kwasababu alifanya kwa kujipendekeza kwa mwendazake!!
 
Unafiki unamtesa huyu mganga njaa. Huyu akiwa Waziri ndio alifungia television zisioneshe shuhuri za Bunge!! Leo hii ukimuuliza sababu ya sera ile na faida yake kwa wananchi hawezi kujibu kwasababu alifanya kwa kujipendekeza kwa mwendazake!!
Malipo hapa hapa duniani
 
Tunapoelekea Tanzania tutakua na chawa wengisana kwasababu kila siku wanaongezeka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…