Nape Nnauye: Tuhangaike kujenga mifumo imara na siyo kutumainia mtu mmoja

sio kweli sasa hivi utendaji serikalini uko juu mno vyombo vya habari havina cha kuandika sasa hivi kuhusu utendaji wa kizembe serikalini ni almost haupo

taja eneo walau moja lenye uzembe humu

Nenda polisi uone kama kuna tatizo lako litatuliwa bila kutoa rushwa na huna pa kushtaki. Nenda hospitalini kama rushwa zimeisha. Nenda mahakamani kama hakuna mlundikano wa kesi. Juzi hapa tume ya uchaguzi imeshiriki kimachomacho kuhujumu wagombea wa upinzani. Na ole wako ukathubu kusema hayo hadharani uone utakachofanyiwa ikiwemo kuhujumiwa shughuli zako za kujiingizia kipato.

Siku moja rais alifanya mkutano na wafanyabishara kusikiliza kero zao, kuna mzee mmoja wa Mbeya akafunguka kuhusu rushwa za TRA, nenda kamuulize leo hii ana hali gani baada ya kuweka ukweli ule hadharani. Nenda leo TRA ukaone barua za kufunga biashara kisha usikilize matatizo ya hao wafanya biashara kuhusu kubambikiziwa kodi. Funga kazi, unaweza kusema zile pesa zilizochukuliwa kwenye Bureau de change zikipelekwa wapi kama sasa hivi kuna utendaji wa weledi huko serikalini?
 
Shida ya sasa watanzania wanageuka kuwa mambumbumbu kisa hawapati taarifa sahihi ,zinazowafikia ni pambio kupitia redio,tv,magazeti na social media za utambulishi usio na kificho.

Exactly.
 
Wabunge wengi wa CCM wakisikia hoja ya kumuongezea mtu miaka wanasonya.
2025 ni muda wa akili mpya, haya ya flani aendelee ni maneno ya wajumbe tuu wanaolinda ugali wao.
 
JF bana, leo nape amekua mtuu wa maaana na kupongezwa na kila mtu,
 
Eti hapana watatoa wale 19 na 300 watasema ndiyo
 
Mchanganyiko wa pumba na mchele kwenye andiko. Ujumbe ni kwamba tujenge mifumo bora na sio kumtegemea mtu mmoja ambaye ukiangalia style yake ya uongozi pia ina mapungufu mengi
 
Naongelea kwenye kero za watu wengi sio wagombea ubunge wachache wa CHADEMA waliopigwa chini au wahalifu wachache wenye mikesi Polisi au Mahakamani au TRA naongelea utendaji wa serikali kuwa ni mzuri kwa majority ya wa Tanzania siongelei minority unaoongelea wewe
 
Nape CCM yenu ishawatema hamna chenu... yaani wewe na wenzako ni kama sisi tu...uliopokonywa form za uteuzi njiani.

tena shukuru mno bila kupiga magoti hata hako ka ubunge ungekasikia kwa radio.
 

Hiyo serikali inachagua maeneo ya kuhudumia? Polisi, hospitali, Tra nk zinahudumia minority? Nasema hivi, serikali kudhibiti vyombo vya habari na kuvifungia vinapotangaza ukweli isioupenda, hiyo haiondoi ukweli wa matatizo ya watu au utendaji duni wa serikali fullstop.
 
Sasa kama mifumo ipo kwanini mnataka Magufuli aongezewe muda?
 
Kumbe bila hata mguu wa mtoto anaongea points
 
sio kweli sasa hivi utendaji serikalini uko juu mno vyombo vya habari havina cha kuandika sasa hivi kuhusu utendaji wa kizembe serikalini ni almost haupo

taja eneo walau moja lenye uzembe humu
Hakuna tofauti kubwa ya ufanisi kati ya huyu na watangulizi wake. Ubunifu pekee alionao ni vitisho na kupambana na watoa habari. Rais ajaye akitokea kambi tofauti, itabidi kupanua magereza zetu kukabiliana na waliotenda makosa chini ya utawala huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…