Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
sio kweli sasa hivi utendaji serikalini uko juu mno vyombo vya habari havina cha kuandika sasa hivi kuhusu utendaji wa kizembe serikalini ni almost haupo
taja eneo walau moja lenye uzembe humu
Nenda polisi uone kama kuna tatizo lako litatuliwa bila kutoa rushwa na huna pa kushtaki. Nenda hospitalini kama rushwa zimeisha. Nenda mahakamani kama hakuna mlundikano wa kesi. Juzi hapa tume ya uchaguzi imeshiriki kimachomacho kuhujumu wagombea wa upinzani. Na ole wako ukathubu kusema hayo hadharani uone utakachofanyiwa ikiwemo kuhujumiwa shughuli zako za kujiingizia kipato.
Siku moja rais alifanya mkutano na wafanyabishara kusikiliza kero zao, kuna mzee mmoja wa Mbeya akafunguka kuhusu rushwa za TRA, nenda kamuulize leo hii ana hali gani baada ya kuweka ukweli ule hadharani. Nenda leo TRA ukaone barua za kufunga biashara kisha usikilize matatizo ya hao wafanya biashara kuhusu kubambikiziwa kodi. Funga kazi, unaweza kusema zile pesa zilizochukuliwa kwenye Bureau de change zikipelekwa wapi kama sasa hivi kuna utendaji wa weledi huko serikalini?