Nape Nnauye: Tukosoane kwa hoja na lugha za staha. Kutukanwa kwa mama mmoja ni kutukanwa kwa kina mama wote Tanzania

TUSHINDANE KWA HOJA BILA KUPIGANA

Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amewasihi Wananchi kutumia maneno ya staha pale wanapowasilisha hoja zao au kukosoa.

Waziri Nape ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam alipokuwa akizungumza katika Kongamano la majadiliano ya Ripoti ya Tume ya Haki Jinai lililohudhuriwa na Wataalamu, Viongozi Wastaafu, Watumishi wa Serikali na Wanafunzi.

Amesisitiza utamaduni wa Taifa la Tanzania ni kuheshimiana huku akitaka kukosoa kufanyike na maoni yatolewe bila ya kutoa lugha za matusi.

Waziri Nape amekumbusha maneno ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
kuwa watu washindane kwa hoja bila ya kupigana.

Pia amekumbusha kuwa mijadala ya Haki Jinai inapoendelea Watanzania wakumbuke kuwa Moyo wa Rais Samia Suluhu Hassan unataka Haki hivyo msingi wa yote ni watu watendewe haki.

Aidha, Waziri huyo wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari amesema tayari amezielekeza taasisi zilizo chini ya wizara yake kuandaa majukwaa mbalimbali kwa ajili ya kujadili na kuchambua mapendekezo hayo ya Tume ya Hali Jinai kwa lengo la kupata maoni ya Wananchi ili ubora upatikane.

View attachment 2692527
Alimuita Magufuli mshamba, je alitukana wababa wote? Au wakati huo kukosoa kwa staha haikuwa lazima?
 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknoloji ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) amewataka watanzania kutotumia lugha za matusi kukosoa jitihada mbalimbali zinazofanywa nchini na Rais wa Serikali ya Awamu ya Sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Waziri Nape ameyasema hayo leo Julai 18 Mkoani Dar es Salaam alipokuwa akizungumza Katika Kongamano la Majadiliano ya Ripoti ya Tume ya Haki Jinai lililohudhuriwa na Wataalamu, Viongozi Wastaafu, Watumishi wa Serikali na Wanafunzi.

Nape amesema kuwa Rais Samia alipowaapisha Viongozi wa Wizara ya Mipango na Uwekezaji amewataka Viongozi hao wawasikilize wakosoaji wote na ikiwezekana wawajumuishe kwenye michakato mbalimbali ya kuboresha mambo mbalimbali katika nchi yetu na kusema kuwa kitendo cha baadhi ya wananchi wakiwemo wanasiasa kutumia lugha zisizofaa wanapotoa maoni yao sio sawa.

“Tukosoane, turekebishe, tutoe maoni bila ya kutukanana. Baba wa Taifa Mwalimu Nyerer alitufundisha tukosoane kwa hoja bila ya kutukanana. Kosoeni, toeni maoni, msidhalilishane na wala msitukanane na hasa inapokuwa ni Rais wa Nchi yetu mana yeye ni sura yetu sote”. Amesema Nape

“Kutukanwa kwa Mama ni kosa na hata kama hajakuzaa moja kwa moja unapomtukana basi ni sawa na kutukanwa kwa wazaza wote, tunao wajibu wa kuwaadhibu wote wanaotukana wazazi wa Nchi hii, kwani wazazi hawa wametulea, wametutunza, wametufikisha hapa tulipo salama na tusisahau kuwa utamaduni wa nchi yetu ni kuheshimiana” Ameongeza Waziri Nape.

Waziri Nape pia amempongeza Rais Samia kwa nia yake ya dhati kutaka kuona haki ikitendeka nchini na kusema kuwa mageuzi anayofanya katika kuboresha na kukusanya maoni ya watanzania kuhusu maboresho ya taasisi zinatoa haki nchini.

“Tunaposhuhulika na Haki Jinai, moyo wa Rais unataka haki. Haki italiinua Taifa letu,” amesema Nape.

Huyu kiribatumbo amesahau kuwa alimuita Magufuli mshamba?
 
Nape wewe sio kijana tena na ukielewa Hilo itakuwa umejitambua
 
Ni kweli Matusi yamekuwa mengi sana mitandaoni FB Twtt na kwingineko

Na hii imetokana na utamaduni mpya wa kutoa maoni nyuma ya Avatar, ufunguaji wa nchi na kupewa uhuru wa kutoa maoni bila shuruti.

Ilhali mheshimiwa Waziri Nape alipokuwa akizungumza hayo katika Kongamano la Majadiliano ya Ripoti ya Tume ya Haki Jinai lililohudhuriwa na Wataalamu, Viongozi Wastaafu, Watumishi wa Serikali na Wanafunzi naamini akiwa amesimama kwenye msingi wa mila na desturi za Mtanzania na haki- Mheshimiwa Raisi Samia Suluhu Hassan siku ya wanawake duniani mbele ya baraza la wanawake wa CHADEMA na Dunia aligusia Upayukaji mitandaoni na athari zake "Kutunishiana misuli" na Kadhalika alisema "huwa naingia Jamiiforums, nawasoma nacheka, lakini nasema huu ni Utamaduni mpya"

Msikikize hapa chini dakika ya 12+

Mheshimiwa Waziri Nape, akubali kuwa huu ni Utamaduni mpya, Raisi alishakubali haya na ni suala la Mda tu kwa Watanzania kukubali matusi kama sehemu ya Utamaduni wa kujibishiana hoja. Hakika haizoeleki lakini ndipo tulipofikia.

Mama kila siku anazidi kwenda shimoni
 
Tatizo hizo hoja hazijibiwa kwa uzito wake, zinajibiwa kwa vihoja, matokeo yake ndio anaishiwa kupewa zawadi yake ya maneno makali, msaliti aliyetuuza watanganyika ndani ya mipaka yetu, hatufai.
 
Stahaa👇🤡🤡🤡
ZPSd.jpeg
 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknoloji ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) amewataka watanzania kutotumia lugha za matusi kukosoa jitihada mbalimbali zinazofanywa nchini na Rais wa Serikali ya Awamu ya Sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Waziri Nape ameyasema hayo leo Julai 18 Mkoani Dar es Salaam alipokuwa akizungumza Katika Kongamano la Majadiliano ya Ripoti ya Tume ya Haki Jinai lililohudhuriwa na Wataalamu, Viongozi Wastaafu, Watumishi wa Serikali na Wanafunzi.

Nape amesema kuwa Rais Samia alipowaapisha Viongozi wa Wizara ya Mipango na Uwekezaji amewataka Viongozi hao wawasikilize wakosoaji wote na ikiwezekana wawajumuishe kwenye michakato mbalimbali ya kuboresha mambo mbalimbali katika nchi yetu na kusema kuwa kitendo cha baadhi ya wananchi wakiwemo wanasiasa kutumia lugha zisizofaa wanapotoa maoni yao sio sawa.

“Tukosoane, turekebishe, tutoe maoni bila ya kutukanana. Baba wa Taifa Mwalimu Nyerer alitufundisha tukosoane kwa hoja bila ya kutukanana. Kosoeni, toeni maoni, msidhalilishane na wala msitukanane na hasa inapokuwa ni Rais wa Nchi yetu mana yeye ni sura yetu sote”. Amesema Nape

“Kutukanwa kwa Mama ni kosa na hata kama hajakuzaa moja kwa moja unapomtukana basi ni sawa na kutukanwa kwa wazaza wote, tunao wajibu wa kuwaadhibu wote wanaotukana wazazi wa Nchi hii, kwani wazazi hawa wametulea, wametutunza, wametufikisha hapa tulipo salama na tusisahau kuwa utamaduni wa nchi yetu ni kuheshimiana” Ameongeza Waziri Nape.

Waziri Nape pia amempongeza Rais Samia kwa nia yake ya dhati kutaka kuona haki ikitendeka nchini na kusema kuwa mageuzi anayofanya katika kuboresha na kukusanya maoni ya watanzania kuhusu maboresho ya taasisi zinatoa haki nchini.

“Tunaposhuhulika na Haki Jinai, moyo wa Rais unataka haki. Haki italiinua Taifa letu,” amesema Nape.

Nape Wewe ulimtukana Edward Lowassa kuwa ni Oil Chafu, mara mgonjwa, wewe huyu huyu uliwahi kurekediwa ukimtukana Rais aliyepita Hayati Magufuli kuwa ni Mshamba na maneno mengi ya kihaini, huwezi leo kusimama na kujipa uadilifu wa kukemea wengine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa....

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Nchi za kiafrica kuendelea ni ngumu sana ofice za umma zinageuzwa kama mali ya familia hadi watuhumiwa anataka haki ya kukosolewe kwa staha badala ya kujiuzulu.
 
Huyu waziri wa habari siku zote huongelea mambo kijuujuu tu akiwa kama kada mtiifu wa chama chake, na wala siyo kama waziri mwenye dhamana. Yeye kupitia wizara yake ndiyo hupaswa kuwa mfano bora katika kutokutoa habari kabla ya kufanya utafiti wa kina na hatimaye kujiridhisha kuhusu "contents & material facts"
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknoloji ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) amewataka watanzania kutotumia lugha za matusi kukosoa jitihada mbalimbali zinazofanywa nchini na Rais wa Serikali ya Awamu ya Sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Waziri Nape ameyasema hayo leo Julai 18 Mkoani Dar es Salaam alipokuwa akizungumza Katika Kongamano la Majadiliano ya Ripoti ya Tume ya Haki Jinai lililohudhuriwa na Wataalamu, Viongozi Wastaafu, Watumishi wa Serikali na Wanafunzi.

Nape amesema kuwa Rais Samia alipowaapisha Viongozi wa Wizara ya Mipango na Uwekezaji amewataka Viongozi hao wawasikilize wakosoaji wote na ikiwezekana wawajumuishe kwenye michakato mbalimbali ya kuboresha mambo mbalimbali katika nchi yetu na kusema kuwa kitendo cha baadhi ya wananchi wakiwemo wanasiasa kutumia lugha zisizofaa wanapotoa maoni yao sio sawa.

“Tukosoane, turekebishe, tutoe maoni bila ya kutukanana. Baba wa Taifa Mwalimu Nyerer alitufundisha tukosoane kwa hoja bila ya kutukanana. Kosoeni, toeni maoni, msidhalilishane na wala msitukanane na hasa inapokuwa ni Rais wa Nchi yetu mana yeye ni sura yetu sote”. Amesema Nape

“Kutukanwa kwa Mama ni kosa na hata kama hajakuzaa moja kwa moja unapomtukana basi ni sawa na kutukanwa kwa wazaza wote, tunao wajibu wa kuwaadhibu wote wanaotukana wazazi wa Nchi hii, kwani wazazi hawa wametulea, wametutunza, wametufikisha hapa tulipo salama na tusisahau kuwa utamaduni wa nchi yetu ni kuheshimiana” Ameongeza Waziri Nape.

Waziri Nape pia amempongeza Rais Samia kwa nia yake ya dhati kutaka kuona haki ikitendeka nchini na kusema kuwa mageuzi anayofanya katika kuboresha na kukusanya maoni ya watanzania kuhusu maboresho ya taasisi zinatoa haki nchini.

“Tunaposhuhulika na Haki Jinai, moyo wa Rais unataka haki. Haki italiinua Taifa letu,” amesema Nape.

Yeye toka sakata hili la DPW lilipoanza alionyesha dhahiri kuwa kachagua upande wa kuusimamia. Hata mchango wake bungeni katika mjadala wa kuridhia IGA, hakuangaishwa kabisa na baadhi ya vipenge ambavyo watu wengi wanavikosoa, isipokuwa yeye alijikita katika kuwananga, kuwabagaza, kuwatisha na kuwakejeli watu wote wenye mitazamo tofauti kwa vigezo na mtizamo wa chama chake.

Yeye kwake mtu kutoridhika na baadhi ya vipengele vilivyomo katika makubaliano na mkataba wa DPW ni matusi dhidi ya Rais SSH, hizo kauli zake tata ni kificho cha kutaka kujumuisha kuwa ni matusi dhidi ya wanawake wote, hii ni njia dhaifu ya kutaka kutafuta "political miliage" ndani ya sakata hili kupitia huruma za wanawake. Kwanza ni lazima atambue kuwa ni kosa kutaka kujumuisha makosa ya mtu mmoja ama ya kikundi fulani na kisha kuyahusisha na jumuiya nzima ya watu wote bila ya kujali kuhusika wala kutokuhusika kwao.

Ni hulka ya binadamu kutumia maneno ye kuudhi akiwa kwenye mihemuko ama kughadhabika. Na hapo hujikuta akitumia maneno yasiyo ya staha, pengine ni vyema tumkumbushe mifano kadhaa,
1. Yesu alimfananisha mfalme Herode na mbweha.
2. Nyerere aliwafananisha wanasiasa kama yeye na malaya au "mercenaries"
3. Mkapa alimrusi Sumaye hadharani, na hata kuwatusi wapizani kuwa ni malofa.
4. Bosi wake alitumia lugha ya kuudhi kuhusu Lissu kupigwa risasi wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2020
5. Nape huyu huyu alijitapa hadharani kwa CCM kupiga bao la mkono katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Lugha ngumu hutumika ili kumaanisha uzito wa jambo. Lugha kama hizi hazikwepeki pale panapojidhihirisha kuwa wale waliopewa dhamana kikatiba wanakiuka kwa makusudi viapo vyao. Pale inapodhibitika kuwa uamuzi umefanywa kwa ajili ya maslahi binafsi ya kundi fulani la watu, na wala siyo kwa maslahi mapana ya taifa, kamwe haziwezi kutumika lugha laini kama zile za mahaba na za kutongozana.
 
Ukitaka kuheshimiwa, wewe uwe wa kwanza kuheshimu wengine.

Mimi nikitumia kauli kali, ni mimi ndiye niliyeitoa. Lakini kwa Rais, yeye binafsi, waziri mkuu, mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa vyombo vya ulinzi, na wateule wake wote, wakitukana, wakipuuza, wakitisha, wakiwaonea watu wasio na hatia, ni Rais amefanya hayo. Kama haungi mkono matamshi na matendo ya wateule wake, ni lazima baada ya matamshi na matendo ya watendaji hao dhidi ya wananchi, ajitenge nao kwa kuchukua hatua dhidi yao. Akinyamaza maana yake anaunga mkono matamshi na matendo yao.
 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknoloji ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) amewataka watanzania kutotumia lugha za matusi kukosoa jitihada mbalimbali zinazofanywa nchini na Rais wa Serikali ya Awamu ya Sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Waziri Nape ameyasema hayo leo Julai 18 Mkoani Dar es Salaam alipokuwa akizungumza Katika Kongamano la Majadiliano ya Ripoti ya Tume ya Haki Jinai lililohudhuriwa na Wataalamu, Viongozi Wastaafu, Watumishi wa Serikali na Wanafunzi.

Nape amesema kuwa Rais Samia alipowaapisha Viongozi wa Wizara ya Mipango na Uwekezaji amewataka Viongozi hao wawasikilize wakosoaji wote na ikiwezekana wawajumuishe kwenye michakato mbalimbali ya kuboresha mambo mbalimbali katika nchi yetu na kusema kuwa kitendo cha baadhi ya wananchi wakiwemo wanasiasa kutumia lugha zisizofaa wanapotoa maoni yao sio sawa.

“Tukosoane, turekebishe, tutoe maoni bila ya kutukanana. Baba wa Taifa Mwalimu Nyerer alitufundisha tukosoane kwa hoja bila ya kutukanana. Kosoeni, toeni maoni, msidhalilishane na wala msitukanane na hasa inapokuwa ni Rais wa Nchi yetu mana yeye ni sura yetu sote”. Amesema Nape

“Kutukanwa kwa Mama ni kosa na hata kama hajakuzaa moja kwa moja unapomtukana basi ni sawa na kutukanwa kwa wazaza wote, tunao wajibu wa kuwaadhibu wote wanaotukana wazazi wa Nchi hii, kwani wazazi hawa wametulea, wametutunza, wametufikisha hapa tulipo salama na tusisahau kuwa utamaduni wa nchi yetu ni kuheshimiana” Ameongeza Waziri Nape.

Waziri Nape pia amempongeza Rais Samia kwa nia yake ya dhati kutaka kuona haki ikitendeka nchini na kusema kuwa mageuzi anayofanya katika kuboresha na kukusanya maoni ya watanzania kuhusu maboresho ya taasisi zinatoa haki nchini.

“Tunaposhuhulika na Haki Jinai, moyo wa Rais unataka haki. Haki italiinua Taifa letu,” amesema Nape.

NAPE ni mavi matupu kichwani mwake yeye alimwita Rais 'Mshamba' Baba Magufuli , na akamsingizia Baba Lowasa kuwa 'Amejinyea ' Huyu mbwa asichokonoe hasira zetu ni choko tena Lina hulka ya kike. NAPE alifanya uhaini akiwa ndani ya chama ,
 
Back
Top Bottom