Nape Nnauye: Tukosoane kwa hoja na lugha za staha. Kutukanwa kwa mama mmoja ni kutukanwa kwa kina mama wote Tanzania

Alimuita Magufuli mshamba, je alitukana wababa wote? Au wakati huo kukosoa kwa staha haikuwa lazima?
 
Huyu kiribatumbo amesahau kuwa alimuita Magufuli mshamba?
 
Nape wewe sio kijana tena na ukielewa Hilo itakuwa umejitambua
 

Mama kila siku anazidi kwenda shimoni
 
Tatizo hizo hoja hazijibiwa kwa uzito wake, zinajibiwa kwa vihoja, matokeo yake ndio anaishiwa kupewa zawadi yake ya maneno makali, msaliti aliyetuuza watanganyika ndani ya mipaka yetu, hatufai.
 
Nape Wewe ulimtukana Edward Lowassa kuwa ni Oil Chafu, mara mgonjwa, wewe huyu huyu uliwahi kurekediwa ukimtukana Rais aliyepita Hayati Magufuli kuwa ni Mshamba na maneno mengi ya kihaini, huwezi leo kusimama na kujipa uadilifu wa kukemea wengine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi za kiafrica kuendelea ni ngumu sana ofice za umma zinageuzwa kama mali ya familia hadi watuhumiwa anataka haki ya kukosolewe kwa staha badala ya kujiuzulu.
 
Huyu waziri wa habari siku zote huongelea mambo kijuujuu tu akiwa kama kada mtiifu wa chama chake, na wala siyo kama waziri mwenye dhamana. Yeye kupitia wizara yake ndiyo hupaswa kuwa mfano bora katika kutokutoa habari kabla ya kufanya utafiti wa kina na hatimaye kujiridhisha kuhusu "contents & material facts" Yeye toka sakata hili la DPW lilipoanza alionyesha dhahiri kuwa kachagua upande wa kuusimamia. Hata mchango wake bungeni katika mjadala wa kuridhia IGA, hakuangaishwa kabisa na baadhi ya vipenge ambavyo watu wengi wanavikosoa, isipokuwa yeye alijikita katika kuwananga, kuwabagaza, kuwatisha na kuwakejeli watu wote wenye mitazamo tofauti kwa vigezo na mtizamo wa chama chake.

Yeye kwake mtu kutoridhika na baadhi ya vipengele vilivyomo katika makubaliano na mkataba wa DPW ni matusi dhidi ya Rais SSH, hizo kauli zake tata ni kificho cha kutaka kujumuisha kuwa ni matusi dhidi ya wanawake wote, hii ni njia dhaifu ya kutaka kutafuta "political miliage" ndani ya sakata hili kupitia huruma za wanawake. Kwanza ni lazima atambue kuwa ni kosa kutaka kujumuisha makosa ya mtu mmoja ama ya kikundi fulani na kisha kuyahusisha na jumuiya nzima ya watu wote bila ya kujali kuhusika wala kutokuhusika kwao.

Ni hulka ya binadamu kutumia maneno ye kuudhi akiwa kwenye mihemuko ama kughadhabika. Na hapo hujikuta akitumia maneno yasiyo ya staha, pengine ni vyema tumkumbushe mifano kadhaa,
1. Yesu alimfananisha mfalme Herode na mbweha.
2. Nyerere aliwafananisha wanasiasa kama yeye na malaya au "mercenaries"
3. Mkapa alimrusi Sumaye hadharani, na hata kuwatusi wapizani kuwa ni malofa.
4. Bosi wake alitumia lugha ya kuudhi kuhusu Lissu kupigwa risasi wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2020
5. Nape huyu huyu alijitapa hadharani kwa CCM kupiga bao la mkono katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Lugha ngumu hutumika ili kumaanisha uzito wa jambo. Lugha kama hizi hazikwepeki pale panapojidhihirisha kuwa wale waliopewa dhamana kikatiba wanakiuka kwa makusudi viapo vyao. Pale inapodhibitika kuwa uamuzi umefanywa kwa ajili ya maslahi binafsi ya kundi fulani la watu, na wala siyo kwa maslahi mapana ya taifa, kamwe haziwezi kutumika lugha laini kama zile za mahaba na za kutongozana.
 
Ukitaka kuheshimiwa, wewe uwe wa kwanza kuheshimu wengine.

Mimi nikitumia kauli kali, ni mimi ndiye niliyeitoa. Lakini kwa Rais, yeye binafsi, waziri mkuu, mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa vyombo vya ulinzi, na wateule wake wote, wakitukana, wakipuuza, wakitisha, wakiwaonea watu wasio na hatia, ni Rais amefanya hayo. Kama haungi mkono matamshi na matendo ya wateule wake, ni lazima baada ya matamshi na matendo ya watendaji hao dhidi ya wananchi, ajitenge nao kwa kuchukua hatua dhidi yao. Akinyamaza maana yake anaunga mkono matamshi na matendo yao.
 
NAPE ni mavi matupu kichwani mwake yeye alimwita Rais 'Mshamba' Baba Magufuli , na akamsingizia Baba Lowasa kuwa 'Amejinyea ' Huyu mbwa asichokonoe hasira zetu ni choko tena Lina hulka ya kike. NAPE alifanya uhaini akiwa ndani ya chama ,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…