Wana jamvi salama. Poleni na majukumu ya kazi katika kipindi hiki kigumu cha kujenga uchumi wetu binafsi.
Katika hali ya kawaida, hakuna mtu asiyejua nn kinaendelea katika nchi ni mvutano wa nguvu mbili zinazopingana na hali halisi jinsi ilivyo.
Tangu mchakato wa kumteua mgombea ktk kile chama cha kijani unaanza, hiyo ilikuwa ni 2015. Ile nguvu ya wapi itakuwa mshindi ilikuwa inajionyesha katika kila dalili.
Maana ukweli ulikuwa unaoneka kuwa yupi anaweza kuja kuwa mgombea halisi. Ila ikaja kuwa ambvyo haikutegemewa, mtu aliyedhani hakuwa yeye ila akaja yule ambaye wala hakudhani.
Hapa nafsi za watu ziliumia sana mana haikuwa kama ilivyokuwa, lakini haikuwa shida mana ikategemea ingekuwa kuja uoande wa pili na huku upande wa pili ikatokea ndivyosivyo. Hapa nafsi za watu wengi zaidi ziliumia mana zile nafsi za watu wa mwanzo na hizi pia kwa ujumla haikuwapendeza wananchi. Lakini kwa shingo upande tu wakakubali iwehivyohivyo tu.
Sasa ikaja wale walioamua kuwa vile wanavyotaka wao kwa kweli ikawa hivyohivyo.
Kwa wale ambao nafsi zao ziliridhia kuwa wanavyotaka wakaanza kuona huyu waliyemuweka amekuwa sivyo wanavyotaka akaanza kuvuruga vile walivyoweka wao. Ikawa hivyo kwa muda kdg ikaendelea hadi wakajiuliza huyu kweli ni MWENZETU au sio yule.
Kumbe wamesahau kuwa hivyo walivyooanga haikuwa hivyo. Zile nafsi za watu kuumia wao wakifurahi kwa sherehe ile laana ya kinyongo inawarudia wao sasa.
Kwa kweli laana imeanza kuwatafuna hadi kwenye kiini sasa mana kila mmoja wao inauma kwa vile sivyo ilivyozoeleka kabisa.
Niwape pole kwa haya maumivu mana ndio yapo katikati kabisa.
Hii ni laana ya mamvi tu. Hakuna ambaye hajui jinsi walivyomfanya kule ndani.