Nape: Sina kinyongo na uamuzi wa Rais Magufuli; Akasirishwa na aliyemtishia Bastola

Nape: Sina kinyongo na uamuzi wa Rais Magufuli; Akasirishwa na aliyemtishia Bastola

Kuna watu wamewafumania wapenzi/wenza wao laivu bila chenga lakini bado wakawasamehe na maisha yanaendelea wakiwa pamoja. Ajabu leo watu hawataki tumpongeze Nape kwa ushujaa na kusimamia haki kisa aliunga mkono kufutwa kwa bunge laivu na kuhusika kwa bao la mkono.

Kama Mungu anasamehe, sisi ni nani mpaka tumkane mwana aliyeamua kurudi zizini? Ni sawa na chadema eti wasingemtoa Zitto kwa sababu tu alisaidia kukijenga chama na tulimpenda hata kama amebadilika na kuwa profesa ndumilakuwili. [HASHTAG]#Redemption[/HASHTAG] [HASHTAG]#BornAgainPolitician[/HASHTAG]
 
​

Heshima Kwenu wakuu,

Leo nmeamua kuwaletea update kutoka kwenye mkutano wa aliyekuwa Waziri wa Michezo wa awamu ya tano Nape Nnauye.

Karibuni.

=======

UPDATES;


=======

13:08hrs: Nipo hapa Protea hotel, Mheshimiwa Nape bado hajafika. Ntamsubiri hapa hapa.

Ametokea mtu anayeitwa Iddi Suleiman ambae ni meneja wa Protea na kudai mkutano hautakuwepo na waandishi walipombana nani kazuia, alisema akaulizwe RPC wa Kinondoni.

1415hrs: Nape amekuja lakini akazuiliwa na Askari(Wanausalama(?) ili asifike sehemu ya tukio, akaamua kushuka ili aje kwa mguu, wakaanza kumvuta kumrudisha kwenye gari. Walikua maasikari kama wanne. Ilikuwa sio mbali kutoka Sehemu waandishi wa habari walipokuwa, Sema walikuwa kwa ndani.

Aliyewajulisha wandishi wa habari kwamba Nape kazuiliwa nje ni dereva wa Nape aliyeanza kupiga honi ya gari kwa nguvu kitu kilichowastua waandishi wa habari na kuwafanya watoke nje. Walipotoka nje wakakuta nape anavutwa aingie ndani ya gari ila Waandishi walipofika Askari wakapunguza kasi

1428hrs: Nape anaongea na waandishi wa habari nje ya Hoteli akiwa juu ya gari.

Nape: Wapuuzi, nimekuja hapa wananitolea bastola eti rudi kwenye gari, nimepigana kuiweka CCM madarakani anakuja mpuuzi eti usishuke kwenye gari, mimi nape sina kinyongo na uamzi wa rais wangu, kama sikumshawishikunichagua hivyo hata kuniacha ni sawa.

Nimejitahidikutimiza wajibu wangu, tusihangaike na Nape tuhangaike na Tanzania inapokwenda nimekuwa mzalendo na muungwana, nimekuwa ninatimiza wajibu wangu

Mimi ndo nimekuwa mzalendo kwa CCM, ambayo niliikuta ikiingia kwenye shimo inakwenda, nitasemakweli daima na fitina kwangu mwiko, na nilichokisiamamia juzi ni kusema kweli, kinachotukutanisha sio magwanda ya kijani, ni imani, nimefundisha na mzee Nnauye kusema kweli na kusimamia ninachokiamini, kamaninachokiamini kitaleta matatizo mimi nlishawahikufukuzwa CCM

Usipopita kwenye matatizoya kisiasa hutakomaa, Ili mbegu iote shuti ioze, nimepanda mbegu ya kupigania haki hakika itaota, Tanzania ni yetu nchini yetu. Vijana hamna la kuogopa simamieni mnachokiamini Mwalimu, Kawawa waliondoka na sisi tutaondoka.

Sisi pia tutaondoka suala la kujiuliza tutaawaachia watoto wetu nchi ya aina gani, hilo ndio kubwa,uamuzi ni wa kwetu wenyewe

Lengo la kuja hapa ni kumshukuru Rais kwa alichokifanya, namshukuru kwa kuniamini kwa mwaka mmoja, nampongeza Mwakyembe naye ni mwanahabari.

Nimefurahi kufanya kazi na nyie, muungeni mkono Mwakyembe na Rais Magufuli ndiye rais tuliyenaye na kudumisha umoja na mshikamano.

Tumefanya kazi pamoja na nimefurahi sana kufanya kazi na nyie
Tudumishe amani na upendo wa nchi yetu, Nape ni mdogo kuliko nchi, wakati wa aliyeniteua ameniondoa mimi nitaendelea kuwatumikia.

Niliomba kazi ya Ubunge na sio uwaziri, sasa narudi kuwatumikia wananchi wangu wa Mtama

Polisi wamezuia gari ya Nape isiondoke, ameshuka kwenye gari anamsikiliza kamanda wa polisi Kinondoni

Nape anawataka waandishi wa habari waondoke, anadai hakuna la kuwaambia tena

​


View attachment 485542

View attachment 485512



Kumbe mchezo ulianza hivi, Nimekutana na hii. Tizama chini

 
Nape mdogo wangu, kuikuta CCM inachungulia shimoni haikupi leseni ya kukiuka taratibu za utumishi au kiutawala.

Ulitakiwa ureport kwa Mamlaka yake ya uteuzi na uwaachie. Ulilofanya ni kudhalilisha Rais, Makamu wake pia Waziri mkuu. Ulikuwa na lengo zuri sana ila hukuwa na weledi wa kudeal nalo. RC ulimchukulia kama Paul Makonda na si Mkuu wa Mkoa. Ulikosea Mkuu wangu. Pumzika ufikirie upya.

Ila kauli za CCM ulikuta inachungulia shimoni ukainyanyua naona ndizo zilizokusukuma hata ukafanya uliyoyafanya. Si kweli kama ulinyanyua CCM mdogo wangu bali kuna mchango wako.

Wewe wakati huo hukuaminika mpaka na hawa wanaokupaka uji kwenye lips sasa. Mzee Kinana ndiye mwenye haki ya kunena hayo na si wewe.

Pole dogo. Lakini pia, ulikuwa na motive ya kumuondoa RC ambe pia hakuwa chini yako wewe. Ni kama mtu na mdogo wake. Hukuwahi kuhisi haya maumivu uliyonayo angeyapata kwa move uliyokuwa nayo? Nafahamu unaumia sana. Haya ni maisha tuu. Maisha ni mchakato na kujifunza pia.

Naamini hutorudia kufanya makosa makubwa kama haya eti kwa kuwa tu ulipigania chama. You are wrong mdogo wangu.

Cha mwisho, usichopenda kufanyiwa usimfanyie mtu mwingine Nape. Kazi njema.
Mkuu hapa ni umemaliza mjadala mzima. Huyu alihisi yeye ndio CCM. Aisee hii ni dharau kwa wanaCCM. Nenda tu kwa kweli mwanakwenda.
 
Kikwete :wauza madawa wana nguvu wamo wanasiasa pia maaskofu nikiwataja nchi hii inatikisika
Magufuli :vita hii hakuna kuangalia brand wala Jina wala Sura
Nape :Jamani ZOEZI hili litaua brand za watu
Magufuli :hata akiwa mke wangu akamatwe tu
Makonda :tumeamua kuanza hii vita ni kama kumwagia mafuta kwenye shimo kila nyoka atatoa kichwa
Makonda :na mimi ukitoa shimo nakugonga tu kichwa
Magufuli :makonda wewe chapa kazi
Nape :kazi hii ina gharama
Magufuli :MIMI NDIO RAIS LIA GARAGARA MIMI NDIO RAISI
NDEGE JOHN :UNGANISHA DOTS, ISHU SIO UHURU WA HABARI ISHU NI WAUZA NGADA KUBANWA VILIVYO
TANESCO :TUNAWAPA SIKU TANO MLIPE MADENI SUGU
WA PENDA UDAKU MATAPELI WAONGO :TWAFAAAA
WAZALENDO :HAPA KAZI TU

ndege JOHN: umehitimisha kila kitu.

Wewe unayesoma bandiko langu, kama unajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya au una ndugu, ione ishara ya kukamatwa. Ama ujisalimishe au ujiue.

TANZANIA BILA MADAWA YA KULEVYA INAWEZEKANA - huo ndiyo ujumbe
 
Nape Nnauye 'Katika maisha ya kisiasa usipopita kwenye migogoro bado haujakomaa na ili mbegu iote lazima ioze, sasa mbegu niliyopanda lazima iote'-
 
Haya maneno umezungmza kama mzee lowasa siku ile ngoja ntafatilia kitakachokuja
 
Hakuna wa kuitoa ccm madarakan labda waamue kupumzika,,,

Wanawachezesha mziki nasi tunaucheza vzri tu bila wasiwasi

Wanapokuja nanpropaganda sisi tunacheka tu kusikiliza na kukosoa
Hakika wamewaweza,,,habar za vyet inakwenda kufa kibudu
 
Nape anapaswa kujutia bao la mkono alilowafunga watanzania wenzake waliotaka kupita njia nyingine. Tanzania ni moja na watu ni wamoja wote mazuri tunayataka, tuache hila katika kuyatafuta. Nadhani Nape anahitaji couselling ya kutosha maana mchango wake kwwnye ushindi wa ccm ulikuwa mkubwa sana anaweza kupata sonona kwa jambo hili. Hata hivyo hajachelewa, yeye kama kijana bado anazo kesho nyingi aende amtafuta babu yake Kingunge ampe ushauri juu ya nini cha kufanya, maana hakuna mtu aliyewahi kuipenda CCM na kuitumikia kama mzee Kingunge.
 
nakuwataja wale wasiyousika mbona ujamalizia
Kuwataja mmekuja juu, wanakamatwa kimya kimya sasa. Wenye kiherehere kama Nape na makuhadi wake wa vyombo vya habari, km Clouds, wanatumbuliwa mchana kweupe.

Nape atakuja kwenye kuwapa mbinu za kukwepa vita ya biashara ya madawa ya kulevya
 
Upuuzi tu .. Hakunachamadawa wala unga niliwahikusema hapa kunajambo lililo jificha
 
Magufuli ni mwanaumeeeeee. Hakuna kuangalia sura, unachemsha basi unapisha wengine. Nape we ni nani kudindishiana kifua na Rais wetu?
 
Waandishi wa habari munabowa!!!! MBona habari za mauaji ya wafugaji hamushupai kiasi hichooo? Huyu siyo shujaa ni mtu mwenye kiburi hata kwa bosi wake. Ngoja aipate.

Kompyuta za kituo cha haki za binadamu ziliponyakuliwa na polisi, alikuwa wapi? Alikenua na kujifanya eti gori la mkono!



fungua kituo chako utangaze
 
Kwa wale mliobakia ofisini kuna la kujifunza hapa,

kama wanamfanyia mambo haya Nape basi hauko salama kamwe.

Kaa mkao wa ready mda wowote kinanuka,
 
Compared to Those 50 Years Lost in Darkness?

This is not too late

I think so!
Tanzania mpya sasa naiona. Wanasiasa wa majukwaani wanaanza kumomonyoka mmoja baada ya mwingine. Wote wanahamia CHADEMA, chama bingwa kwa siasa za majukwaani, vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.
 
Back
Top Bottom