Nape: Sina kinyongo na uamuzi wa Rais Magufuli; Akasirishwa na aliyemtishia Bastola

Nape: Sina kinyongo na uamuzi wa Rais Magufuli; Akasirishwa na aliyemtishia Bastola

Dah nimejisikia vibaya sana kweli hivi huyu ndio nape yule wa kipindi cha Kampeni nape wa kusukumwa na polisi dah Mungu amjalie sana Nape
Tulia mkuu-karma inatabia ya kukurudishia sawasawa na ulivyotoa.
....ukinisoma kwenye mistari utanielewa.
 
Hakika hotuba fupi aliyoitoa Mh Nape ni ya kishujaa.Hakuna asiyejua mlikoitoa CCM wewe Na Kamanda Kinana.CCM ilikuwa imekufa mkaifufua lakini Leo shukurani yao tumeiona Bravo Nape Bravo Nape wewe ni Shujaa utabaki kuwa Shujaa
 
viongozi wa dini baada ya kutuambia tumuombee sasa hivi wako kimya ila yatawafika tu nao,yataanza kwa gwajima halafu watasema ah huyo achana naye mjeuri huyo halafu yatawafika nao pia kwani hata clouds walitarajia yaliyowafika?
 
Nimemuona Gwajima kwenye sauti ya Nape kuwatukana Usalama wa Taifa Letu. Hii ni hatari kuvunja amani. Usalama wa Taifa tusiwatukane.
 
Kampeni ya kwanza tususie kwenda uwanjani taifa stars ikicheza uwanjani, waende TFF
Msituletee siasa kwenye mpira, pambaneni huko huko hatupendi ujinga.
 
Aliyeuliza season 2 ndo hii sasa, hakuna tena vyeti, hakuna tena Daudi Bashite, Hakuna tena Njaa, hakuna tena kuvamiwa kwa CLOUDS MEDIA hakuna tena sijui nini..... wiki nzima itakuwa ni kuachishwa uwaziri NAPE MOSES NNAWIE. Baada ya hapo itakuta season three...... itakayotupeleka mbali kabisa na BASHITE
Kwel wew ni son of man [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16]
 
​

Heshima Kwenu wakuu,

Leo nmeamua kuwaletea update kutoka kwenye mkutano wa aliyekuwa Waziri wa Michezo wa awamu ya tano Nape Nnauye.

Karibuni.

=======

UPDATES;


=======

13:08hrs: Nipo hapa Protea hotel, Mheshimiwa Nape bado hajafika. Ntamsubiri hapa hapa.

Ametokea mtu anayeitwa Iddi Suleiman ambae ni meneja wa Protea na kudai mkutano hautakuwepo na waandishi walipombana nani kazuia, alisema akaulizwe RPC wa Kinondoni.

1415hrs: Nape amekuja lakini akazuiliwa na Askari(Wanausalama(?) ili asifike sehemu ya tukio, akaamua kushuka ili aje kwa mguu, wakaanza kumvuta kumrudisha kwenye gari. Walikua maasikari kama wanne. Ilikuwa sio mbali kutoka Sehemu waandishi wa habari walipokuwa, Sema walikuwa kwa ndani.

Aliyewajulisha wandishi wa habari kwamba Nape kazuiliwa nje ni dereva wa Nape aliyeanza kupiga honi ya gari kwa nguvu kitu kilichowastua waandishi wa habari na kuwafanya watoke nje. Walipotoka nje wakakuta nape anavutwa aingie ndani ya gari ila Waandishi walipofika Askari wakapunguza kasi

1428hrs: Nape anaongea na waandishi wa habari nje ya Hoteli akiwa juu ya gari.

Nape: Wapuuzi, nimekuja hapa wananitolea bastola eti rudi kwenye gari, nimepigana kuiweka CCM madarakani anakuja mpuuzi eti usishuke kwenye gari, mimi nape sina kinyongo na uamzi wa rais wangu, kama sikumshawishikunichagua hivyo hata kuniacha ni sawa.

Nimejitahidikutimiza wajibu wangu, tusihangaike na Nape tuhangaike na Tanzania inapokwenda nimekuwa mzalendo na muungwana, nimekuwa ninatimiza wajibu wangu

Mimi ndo nimekuwa mzalendo kwa CCM, ambayo niliikuta ikiingia kwenye shimo inakwenda, nitasemakweli daima na fitina kwangu mwiko, na nilichokisiamamia juzi ni kusema kweli, kinachotukutanisha sio magwanda ya kijani, ni imani, nimefundisha na mzee Nnauye kusema kweli na kusimamia ninachokiamini, kamaninachokiamini kitaleta matatizo mimi nlishawahikufukuzwa CCM

Usipopita kwenye matatizoya kisiasa hutakomaa, Ili mbegu iote shuti ioze, nimepanda mbegu ya kupigania haki hakika itaota, Tanzania ni yetu nchini yetu. Vijana hamna la kuogopa simamieni mnachokiamini Mwalimu, Kawawa waliondoka na sisi tutaondoka.

Sisi pia tutaondoka suala la kujiuliza tutaawaachia watoto wetu nchi ya aina gani, hilo ndio kubwa,uamuzi ni wa kwetu wenyewe

Lengo la kuja hapa ni kumshukuru Rais kwa alichokifanya, namshukuru kwa kuniamini kwa mwaka mmoja, nampongeza Mwakyembe naye ni mwanahabari.

Nimefurahi kufanya kazi na nyie, muungeni mkono Mwakyembe na Rais Magufuli ndiye rais tuliyenaye na kudumisha umoja na mshikamano.

Tumefanya kazi pamoja na nimefurahi sana kufanya kazi na nyie
Tudumishe amani na upendo wa nchi yetu, Nape ni mdogo kuliko nchi, wakati wa aliyeniteua ameniondoa mimi nitaendelea kuwatumikia.

Niliomba kazi ya Ubunge na sio uwaziri, sasa narudi kuwatumikia wananchi wangu wa Mtama

Polisi wamezuia gari ya Nape isiondoke, ameshuka kwenye gari anamsikiliza kamanda wa polisi Kinondoni

Nape anawataka waandishi wa habari waondoke, anadai hakuna la kuwaambia tena

​


View attachment 485542

View attachment 485512

Tulishasema kuwa ukimfuga nyoka ukae na rungu sasa nyoka ameanza kuwauma watoto wa jirani wakiisha ataanza kuwauma wa aliye mfuga,ewe mungu tuepushie hiki kikombe
 
RPC anatumika vibaya lakini Anatakiwa kukumbuka cheo ni dhamana
 
Mimi sio mpenzi wa sisiem lakini namshauri Nape atulize munkari, atafakari sana halafu arudi nyuma miaka iliyopita na kuwakumbuka kina Kombe, Kolimba na Kighoma Malima. Naamini familia yake bado inamhitaji sana. Anadai hii ni nchi huru, YES na ya kidemokrasia!!!? Nafikiri itategemea uko upande gani wa wakina Donald Trump wa Bongoland.
Hawana uwezo wa kumfanya lolote nape.si walitumwa leo kwani wamefanya nini mbona nape ameongea sasa
 
Kila siku tunasema humu, wengi mnasubiri mpaka muumizwe ndipo muanze kusema haki haki! Kila siku tunashauri kila mtu asimame kwenye haki, kila mtu apinge uonevu bila kujificha kwenye magwanda ya vyama vyetu.. You don't listen, leo kimemtokea Nape, who would have thought? Kesho kitarudi kwa baadhi ya lunatics ambao bado wanashabikia ujinga ujinga...
 
Nape mdogo wangu, kuikuta CCM inachungulia shimoni haikupi leseni ya kukiuka taratibu za utumishi au kiutawala.

Ulitakiwa ureport kwa Mamlaka yake ya uteuzi na uwaachie. Ulilofanya ni kudhalilisha Rais, Makamu wake pia Waziri mkuu. Ulikuwa na lengo zuri sana ila hukuwa na weledi wa kudeal nalo. RC ulimchukulia kama Paul Makonda na si Mkuu wa Mkoa. Ulikosea Mkuu wangu. Pumzika ufikirie upya.

Ila kauli za CCM ulikuta inachungulia shimoni ukainyanyua naona ndizo zilizokusukuma hata ukafanya uliyoyafanya. Si kweli kama ulinyanyua CCM mdogo wangu bali kuna mchango wako.

Wewe wakati huo hukuaminika mpaka na hawa wanaokupaka uji kwenye lips sasa. Mzee Kinana ndiye mwenye haki ya kunena hayo na si wewe.

Pole dogo. Lakini pia, ulikuwa na motive ya kumuondoa RC ambe pia hakuwa chini yako wewe. Ni kama mtu na mdogo wake. Hukuwahi kuhisi haya maumivu uliyonayo angeyapata kwa move uliyokuwa nayo? Nafahamu unaumia sana. Haya ni maisha tuu. Maisha ni mchakato na kujifunza pia.

Naamini hutorudia kufanya makosa makubwa kama haya eti kwa kuwa tu ulipigania chama. You are wrong mdogo wangu.

Cha mwisho, usichopenda kufanyiwa usimfanyie mtu mwingine Nape. Kazi njema.
 
Back
Top Bottom