Nape: Sina kinyongo na uamuzi wa Rais Magufuli; Akasirishwa na aliyemtishia Bastola


Hizo hadithi zenu hujashtukia tu kuwa hazina nafasi? Najua mnatunga tuhuma na kila aina ya hadithi wakati huu ili kujaribu kuhalalisha ukatili na uharibifu wa mkuu wenu. Hamtofanikiwa.

Atakuja Sizonje na kutoa vijembe na vitisho vyake kama kawaida; lakini subirini tu kidogo mtajua ngoma ya watoto haikeshi. Kutambazuka na tutakuwa na nchi nyingine na majira mengine.
 
Nape anajua kuwa ccm inatambua mchango wako, kilichotokea na wajib kitokeee, kisingetokea kwake kingetokea kwa mwingine,

Nimeona busara kwa nape, ila ajue kuwa hao waandishi ni wanafiki kupindukia wao ndio ulipochaguliwa waliponda balaaa... Leo umekuwa shujaaa..

Ndivyo siasa ilivyo
 
Nafikiri kuondoka kwa Nape akuwezi kubadilisha ukweli na akuwezi kumsafisha Makonda bali ukweli utabaki pale pale
 
Nchi inaongozwa hovyo hovyo.... Huyu Rais wetu kwanini ana kigugumizi kuchukua hatua kwa Makonda? Kuna nini hasa?
 
It is the wearer who knows where shoe pinches! We suffered a great deal bro...Wacha Nape aonje dhuluma ya dola labda itasaidia kuliponya Taifa hili!
 
Mdogo wangu Nape, Acha unafiki wa kisiasa, Kusema huna kinyongo na Rais kwa kukuondoa kwenye nafasi yako ya uwaziri kwa mazingira hayo, si kweli kabisa. Tuko kwenye kipindi cha Kwaresma, hatupaswi kusema uongo. Unaweza kusema umemsamehe, lakn lazima iwe imekukasilisha. Hakuna mtu anayependa kuonewa. Ni hulka ya kawaida ya binadamu. Baada ya hapo, unaweza kusema umemsamehe, hapo tutakuelewa...
 
Ndio ccm sasa inaenda yenyewe kaburini na Nape huyoo cdm
Sasa wewe unadhani mtu mmoja akiondoka ndo anaua chama.. Akishaondoka lowasa.. CCM ni kubwa Sana ipo mwanza, Dodoma, kote mtu mmoja hawezi kubadili mitizamo ya wanachama wengi ambao wapo kwenye MTANDAO Mpana wa vijana, wazee, wa mama na Wazazi
 
Mchapakazi ataonekana tu wananchi tunajua, haijalishi mnatulisha maneno gani, tutampa kura anayetetea maslahi yetu kwa ujumla.
Kwa sasa tumekuwa waelewa sana msidhani hatuelewi tuendako.
Matukio yoooote " tunawaona tunawaonaaaa"
Hatujatupa vichinjio.
 
Wasiyoweza speed ya magufuli watupishe.. Hili ALISHASEMA Nashangaa hakutaka kusoma alama za nyakati
 
Alhamis hii jua limechomoza likiambatana na mshtuko mkubwa kwa wananchi wengi wa Tanzania.



Mshtuko huo umetokana na taarifa ya mheshimiwa Nape Nnauye kupokonywa nafasi ya uwaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Hii imekuwa habari yenye mpasuko mkubwa hasa katika kipindi hiki ambacho Nape ameonekana kuwa mtetezi muhimu wa vyombo vya habari kufuatia kitendo kilichofanywa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuvamia studio za Clouds Media Group akiwa na askari wenye silaha nzito.

Ikiwa ni siku moja tu baada ya kupokea ripoti toka kwenye kamati aliyokuwa ameiteua kufanya uchunguzi wa tukio hilo, Nape ameondolewa na kuacha sintofahamu kubwa kwenye mkasa huo.

Mastaa, viongozi na wananchi wametoa maoni yao ambao mengi yanafanana – hawajependezwa na kilichotokea huku wengi wakimwelezea Nape kama shujaaa.
Haya ni baadhi yao:

Zitto Kabwe
Nimezungumza na mbunge wa Mchinga @Nnauye_Nape na kuthibitisha kuwa Ni Kweli ameondolewa kwenye Uwaziri. Nape ni Shujaa wa kizazi chetu

Irene Kiwia
The key resource of ordinary citizens is numbers. And justice will reign on earth and truly will the voice of the people be the voice of God. When there is true awakening of the people, in numbers, it forms the real and conscious public opinion.

B12
Nitakua naota eti……. Ngoja nilale tena then niamke! Maana hii si mara ya kwanza kukutana na ndoto mbaya ya kutisha!!

Nchakali
Kaka @Nnauye_Nape nakushukuru kwa kunipa mfano wa kutumia kumfundishia mwanangu zion somo la uzalendo! HISTORY will JUDGE you RIGHT!

Halima Mdee
Naamini ni UZUSHI!!

Edo Kumwembe
Sidhani kama Nape anajali…alilitafuta hili kwa nguvu zote…sidhani kama anajali

Bonge la Nyau

Huyu ni shujaa wangu……

Wema Sepetu
We will Surely Miss U as Our Minister… Tulishakuzoea. Such a way to start Your Morning.. Lets wait for what’s NEXT…. This Is Tooo Much Jamani. This Country Be Full of Surprises Nowadays…. Smh.. Never Knew Nchi ina MaRais wawili… Now I know…. Smh…

Idris Sultan
Raisi akashika Jiwe na Almasi akavipimaaaaaaaa akasema embu katupeni almasi ina’ngaa kijinga jinga tu nimeiambia ing’ae kwani.

Madee‏
Sad newz

Masoud Kipanya
Haya ni mawazo yangu… Ningekuwa @Nnauye_Nape ningekaa KIMYA kabisa

Diva
Nimepata mshtuko wa mwaka . Kama Kijana Mpenda Haki na Mpenda Maendeleo na Ninaejitegemea Nimepata Mshtuko wa Mwaka , Nimejiuliza maswal Kwa uchungu Chozi limetoka

Peter Msigwa
Kwa Magufuli bashite ni muhimu na ni bora kuliko Nape ndani ya chama na serikali! Hongera JPM!

Mwana FA
(Alitweet muda mfupi kabla ya habari za kuondolewa uwaziri (Toka mwanzo kabisa wa haya maswahibu, kaka yangu @Nnauye_Nape anaonesha ukomavu wa hali ya juu kabisa..kisiasa na kibinadamu. Anajua umuhimu wa kufanya ‘vita’ dhidi ya mambo yasiyo sahihi kwa jamii bila dhulma na ukiukwaji wa sheria,na hayumbi kwy kusimamia ukweli.
NA HARINGI ..SALUTE kaka @Nnauye_Nape …najivunia kusema nakujua,ubarikiwe ndugu yangu)

Baada ya habari hiyo kufahamika alitweet: Aisee..

Aika
Its not dictactorship its being a coward [HASHTAG]#JustSaying[/HASHTAG] running frm people challenging u

Quick Rocka

I don’t feel proud kuwa mtanzania anymore….Tunatangazaje na kusifia nchi ambayo viongozi wanaosimamia ukweli na sheria wanaondolewa…Huku wanaozingua wanaendelea kupeta…Nape alikuwa waziri sahihi kabisa kwetu wasanii,wanamichezo na wanahabari.
Source;Bongo 5
 
Amesau anyepitisha majina ya ubunge mwenyekiti ana kura ya veto.
Aendelee kujisahau ataenda kuomba kazi clouds
 
[emoji51] [emoji51] [emoji35] [emoji35] Nashukuru nimeweza kujizuia. Mwenyez mungu atupe uhai tuzidi kuona mengi.
 
Naona tuko North Korea ghafla, Ndugu yangu NAPE kwa maneno hayo ya ukweli kabisa wasije waka Kukolimba wanatangaza amani lakini wameshika majambia tazama sana. CCM tunakuhitaji sana
 
Tuombe uhai tushuhudie yatakayojiri kwenye anga hizi za Tanzania..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…