Nape: Sina kinyongo na uamuzi wa Rais Magufuli; Akasirishwa na aliyemtishia Bastola

Hapo umenena vyema, hawa viongozi wetu wa kisiasa ni hatari sana kumpa madaraka makubwa.
 
Bashite ana nguvu kwenye hii serekali kuliko Nape Nauye. Hivi Magu na Bashite wana siri gani[emoji15] mpaka imefika kumfukuza kazi Nape.


Ndukiiiii[emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Sasa ni dhahiri ukiingia anga za Bashite unaenda na maji.
Swali kubwa,kuna siri gani kati yake na 'Mufalume' hadi amlinde kwa gharama iwayo yoyote ile?
 
Tangu vita ya. ngada imeanza Nnauye alionekana yupo against na kile serikali inachosimamia mara image mara sijui nikikutwa nna mahusiano na Msaniii najiuzuru haya sasa wenzie wamemuwahi...
 
Hijacking everything and create elite club from resources that were meant for all is a sin and crime. Acha wapambane mpaka wakae sawa
 
Slaa aliteleza bafuni akavunjika mkono.Pili toa ushahidi wa kikao kilichomfukuza Slaa Chadeam.Slaa aliondoka mwenyewe baada ya kuhitilafiana na wenzake na isitoshe alirudi kuwakandia Chadema.
 
Ni kweli tumpe pole, ila roho wa bwana ananionyesha ufa mkubwa kule kule chumbani kwao. Ngoja tuone!
 
Hivi karibuni mara baada ya Mh. Nape Nauye aliyekuwa waziri wa habari utamaduni na michezo kukerwa na kitendo kiovu alichofanya mkuu wa mkoa wa Dar e salaam Paul Makonda kuvamia kituo cha habari cha Clouds akiwa na polisi wenye siraha za moto, Mh. Rais kwa kushangaza umma wa watanzania amemfuta kazi. Mimi kama raia wa nchi hii mwenye uhuru wa kutoa mawazo kwa mujibu wa katiba ya nchi, kitendo cha kusimamia ukweli alichokifanya Mh. Nape ni cha kizalendo kinachofaa kuigwa na viongozi wote wa kisiasa; ukweli lazima usimame hata kama kuna hatari ya kupoteza kazi na hata ikibidi maisha. Mh. Nape watanzania wote wanakuunga mkono na kumbuka kuwa maisha yapo hata nje ya uwaziri na ikibidi hata nje ya CCM. Kitendo alichokifanya Rais mimi sikushangaa kwani hiyo ndiyo tabia ya viongozi wengi wa Afrika ambao hawataki kukosolewa. Rais anapaswa kufahamu kuwa hakuna binadamu ambaye fikra zake tu ndiyo sahihi na hali hii ya kufumbia macho ukiukwaji wa sheria ikiendelea taifa hili litapoteza mwelekeo. Watanzania hapo ndipo wanapaswa kujifunza kutafakari kwa kina kabla ya kupiga kura, na hii ndiyo hatari ya chama kimoja kukaa madarakani kwa muda mrefu. Hapa naweza kusema kuwa watanzania tukomae na tuendelee kuonja madhira ya makosa tuliyofanya wakati wa kupiga kura. Mh. Nape hongera umeonesha njia hata kwa wana-ccm wengine waliopewa madaraka na Rais.
Siku zote haki huinua taifa.


 

 
[emoji23][emoji23][emoji23] Nimecheka sana kwenye clip ya pili jinsi harmorapa alivokuja kwa mbwembwe af baada ya kuona bastola akala kubwa fastaaaaaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…