Nape: Sina kinyongo na uamuzi wa Rais Magufuli; Akasirishwa na aliyemtishia Bastola

Kabisa mkuu
 
Una matatizo ya akili wewe
 
Wanachumia tumbo...kuwa mama shujaa sio mchezo.

Ni lazima uache unafiki, uzandiki na kujipendekeza.

Serikali imekufa ganzi. Sterling mmoja na yeye hajielewi anarudia episodes!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Point ya msingi sana ila nani atathubutu...
Wenzao Kenya akina CORD/NASA wakipanga kwenda uwanjani kamkunji lazima waende hata kama watatimuliwa na polisi/mwagiwa maji lakini hawarudi nyuma kutekeleza azma zao.sasa UkUTA unasubiri mpaka leo viongozi wa dini waongee na Rais! Rais hapangiwi mtu wa kuongea naye/mda wa kukutana.
 
Acheni unafiki nyie CCM mtaungua wore.. Mnataka kusema nape ndo kawa jasiri kuliko kina Lema, Lisu na Mbowe? Acheni undakindaki, tena angekua Lema pale asingesukumwa sukumwa tu angekula virungu vya kutosha na kubebwa mzobemzobe. Nyie vipi bwana
Mimi sina unasaba na CCM soma.post zangu zote utanielewa.ila upinzani bila kujiongeza watanzania wote tutaangamizwa.lazima viongozi watoe mfano.ili sisi tufuate.nchi hakabidhiwi mtu Mwoga kama kunguru.
 
Huyo askari ni bwege kabisa,unatolea watu bastola,ww kama nani nchi hii?
 
Utawatafutia wewe kazi nyingine?
 
Hao hawana principle,wamejaa unafiki tu,
kairuki alikuwa mzuri mwanzoni lakini katika awamu hii kwisha kazi,
 
katika nchi hii watu wanao ongoza kwa unafki ni hao walio soma sana kuanzia prof na dr wengi wao wanawaza kuchumia tumbo
 
Binafsi mimi kama mpiga kura wako na mwananchi wa jimbo la Mtama nampongeza Mh. Rais kwa maamuzi ya kutengua nafasi yako kama waziri, Na sisi wanajimbo la Mtama tutakuunga mkono kama wananchi ambao tumekupa kura za kuwa mwakalishi wetu na tunafikiri itakuwa nafasi mzuri kwako kuja kutuhudumia sisi wapiga kura wako ambao kwa kiasi kikubwa ni kama umetutenga kutokana na kivuli cha “UWAZIRI”

Nasema hii kwa kuwa niliona kila dalili za kumfuata mtangulizi wako Bw. Membe ambaye na yeye alikuwa anajificha kwenye kivuli cha “UWAZIRI” na yeye alikula pesa za marehemu na akala zile za kiwanda. Nawe pia nilikuwa nakuona pia upo kwenye kasi ya ajabu kumfuata mtangulizi wako ulikuwa upo busy kuipigania Singida Utd na kumfunga ndg Selemani Methew ambaye alikuwa anaipigania Kariakoo ya Lindi na timu zingine za mkoa wa Lindi. Nafikiri unatambua ni kwa kiasi gani wananchi wa Mtama jinsi wanavyokuchukia na bado yale maneno yako ya kipindi cha kampeni yapo kwa wananchi wa Mtama, si unakumbuka kipindi cha kampeni wananchi walikuzomea mpaka ukatoa Bastola na kuipiga hewani risasi kadhaa..? Na lile tukio la kuzomewa mpaka ukalia ndani ya gari pale PHAISHA LODGE si unakumbuka pia na mpaka wananchi inafikia hatua wanakuombea dua mbaya mpaka unapata ajali haujajifunza tu..? haujui ni kiasi gani wananchi umewakwaza…!

Unakumbuka ahadi zako kupitia “SMS” yako ya Oktoba 11, 2015 kwa wapiga kura wako..? nakukumbusha kwa sababu najua unapita humu kwa Id fake ya __, Ulisema MAJI, BARABARA ZA VIJIJINI, UMEME, MTANDAO WA SIMU, HUDUMA ZA AFYA & SUALA LA ELIMU vitakua historia.

Kuhusu “MAJI” hapa mtangulizi wako afadhali kidogo alianza na mradi wa maji CHIUE kupitia Nyangao na wananchi tulijitolea nguvu zetu kuchimba mitaro, Lakini tangu Utawala wako mbunge wangu umebadili uelekeo sasa unataka kuchukulia maji RONDO ili mradi upitie unakojenga nyumba yako kule Makasini na hakuna dalili yoyote ile ya mradi kuanza, wananchi wako huku wanakunywa maji ya mto Lukuledi ambayo si masafi na si salama achilia mbali wale wa kata za Nyangamara na Mandwanga ambao wanakunywa maji yaliyotuama.

Kuhusu “BARABARA ZA VIJIJINI” hapa ndio mbaya kwa kweli barabara hazipitiki na hakuna halmashauri ambayo ina barabara mbovu kama ya Lindi ikiongozwa na jimbo la Mtama na hata ile barabara ambayo umeichonga ili uweze kwenda kijiji cha SHUKA ambako umenunua zaidi ya ekari 200 nayo sasa hivi haipitiki kabisa na hata watumishi wanapata shida kwa kweli. Uliahidi na umeshindwa kutekeleza.

Kuhusu “MTANDAO WA SIMU” mkuu sana na mh. Mbunge wangu wa jimbo la Mtama hapa napo umefeli kwa kiasi kikubwa, si unakumbuka mwaka 2015 ulivyoenda kule kata ya Mandwanga ambako unasema ni chimbuko la mzee Mosses Nnauye…? Unakumbuka uliwaahidi nini wale ndugu zako kuhusu suala la mtandao wa Simu, achilia huko pia sehemu kubwa ya jimbo lako mawasiliano ni shida.

Kuhusu “HUDUMA ZA AFYA” hapa sitaongelea chochote kwani tangu utoe vile vitanda pale Sokoine mwaka juzi na Wana-CCM kindaki ndaki kutamba mtaani huku wakisema kuwa umeanza kutekeleza ahadi zako sijaona kingine chochote mpaka sasa hivi.

Kuhusu suala la ELIMU, hapa mbunge wangu unafeli na unafanya maamuzi yako kupitia mitandao, tangu kipindi kile ilivyosambaa video na picha ya S/M Msingi Litingi iliyopo Nyangao na ukaikarabati mpaka leo hakuna jambo linguine kuhusu shule. Kuhusu ELIMU kuna Organization inaitwa SEDO inafanya “INSPIRATIONAL VISIT” kwa shule za kusini umeombwa kushiriki umekataa katakata, nakuomba Mh. Sana mfuate jirani yako mbunge wa Nanyamba Mh. Chikotta muulize amewezaje kutembelea shule na kusaidia kupunguza changamoto zinazowakabili wanafunzi na pia kuwapa hamasa au haujamsikia Mh. Bashe alivyowaahidi wanafunzi wa kidato cha nne endapo watafaulu kwenda kidato cha Tano..?

Jambo la kushangaza kuliko yote ofisi yako ya jimbo mpaka leo haina Katibu wa


Jimbo


Njoo jimboni tufanye kazi.
 
Acheni unafiki nyie CCM mtaungua wore.. Mnataka kusema nape ndo kawa jasiri kuliko kina Lema, Lisu na Mbowe? Acheni undakindaki, tena angekua Lema pale asingesukumwa sukumwa tu angekula virungu vya kutosha na kubebwa mzobemzobe. Nyie vipi bwana
Hebu jielewe wewe. Ni Mara ngapi mikutano inaghailishwa kwa kuhofia policcm na ni Mara ngapi watu wanapigwa kisa mikusanyiko. Sababu ya kusema nani wa kuthubutu ni kwamba watu wakiona maaskari na magari yao washa huanza kuhofia ila kama tungekuwa na msimamo juu ya tunachokiamini na kukipigania tungekuwa radhi kuumua, kufungwa ama hata kuuliwa kwa maslahi ya wengi. Hebu jiulize kama UKUTA ungefanikiwa na watu wangejitolea kupigania haki ya kikatiba unafikiri police wangeweza kuwadhibiti ama kudhibiti Tanzania nzima mikutano na kama ingekuwa hivyo Rais angeonekana vipi kwa jamii inayomzunguka kwa kuwayima Raia haki zao kwa kutumia nguvu. Nchi za wenzetu wanamsimamo na hawaogopi polisi wala jeshi
 
unamtaarifu/unamsuta??? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

ujumbe umemfikia!!!
hivi ulanga upo?
 
Reactions: e2n
Hivi karibuni wakati sakata la Bashite likiendelea huku kituo cha radio clouds kikionekana kulifumbia macho, kituo cha radio cha E fm bila kupepesa kilijadili suala hilo kinagaubaga bila kuona aibu!

Itakumbukwa pia wakati huo aliyekuwa waziri Nape Nnauye alikitembelea kituo hicho na kusema kuwa atawapa sapoti ya kutosha na hivyo kuhakikisha kuwa hawatopata usumbufu!

Sasa Nape ametumbuliwa na wizara amepewa Mwakyembe!

Huyu Mwakyembe amekuwa ni mtu wa kuropoka na kutoa maamuzi ya hovyo sana, ikizingatiwa alipokuwa wizara ya katiba na sheria alitishia kuifuta TLS kwa maslahi yake anayojua na yamkini yawezekana alitumiwa kutamka hivyo!

Huyu Mwakyembe inavyoonekana kapewa hiyo wizara kwa ajili ya kazi maalum, naamini kuna mizengwe itachezeshwa na lazima mlengwa akamatike ili ashikishwe adabu!

Tukiunganisha dot ishu ya Majizo kuhusishwa na madawa ya kulevya, kutumbuliwa kwa Nape maana tayari Nape alishaonesha ukaribu na Majizo na ile kusemekana kuna mambo nape aliahidiwa na Majizo, inapelekea kabisa kuonekana picha halisi ya yatakayojiri baada ya Mwakyembe kupewa hii wizara!

Kuna kile kitendo Kitenge alichofanya cha kumzuia yule jamaa aliyetoa pisto, siyo ajabu movie ikaanzia hapo!!
 
Kwa upende alionao kwa bwana bashitee hata swala la vyeti tuliishashindwa ni amri tu mtu anaenda necta anaamuru futa records za bashiteee weka paul nani atabisha wakati mkulu kasema
 
Umesema Sawa, Ushauri: wanasheria wakadai haki ya kikatiba ya mikutano ya siasa mahakamani badala ya kuendelea kulalamika majukwaani na kutoa matamko ambayo hayatekelezeki kama UKUTA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…