Nape: Sina kinyongo na uamuzi wa Rais Magufuli; Akasirishwa na aliyemtishia Bastola

Hii series imefikia sehemu ya fitna sasa leo nyuzi zilizojaa fitna kwa Nape zinatiririshwa tu humu
 
Dear.. tunamwita Nape shujaa kwa sababu tunaamini hakuna mtanzania mwenye akili timamu, jasiri na asiyesimamia unafiki na njaa anayeweza kupenda style ya uongozi ya Pombe.... hata mawaziri wengine nao pia hawaridhiki na mwenendo huo ila kwa sababu ya uwoga wa kutumbuliwa ambao Nape hana, tabia ya kuendekeza njaa ambayo Nape hana, tabia ya kukosa ujasiri ambayo Nape hana na tabia za kinafiki ambazo Nape hana ndizo zinazowafanya kuendelea kuwepo kwenye serikali ya baba na mwana mpaka leo....
 
Unaishi Tanzania hii hii au we mwenzetu upo Burundi?
 
 
Tatizo lako kila habari ya Bashite unatetea kila post kwa wenye akili tunawaza yawezekana mmoja wao kama sio ikulu anakutafua sio bure. Usikasirike kutafuna ama kutafunwa ni mambo ya kawaida yapo katika real life cycle
Huyo sio kutafunwa ni kukanyagwa. Mijadala ya maana anaiharibu kama wadada wa kona bar wanavyo haribu ndoa za watu
 
weka vyeti tutambue uwezo wako wa kufikiri
 
Mtasema sana lakini kwangu Nape ni zaidi ya kijana shujaa. Na vijana tusiogope hii ni nchi yetu sote
 
Aisee kumbe jpm anaangalia ukawa wanasema nini ndiyo anafanya maamuzi, tunashukuru kwa Taarifa ingawa huu uzi ni duplicate
 
Juzi kwenye mkutano na waandishi wa habari Nape alisema ye alikipigania chama maana kilikuwa kinaanguka..

Ukiangalia kwa umakini yale ni maneno ya kijeuri tu..maana chama kilitaka kufa kutokana na figisufigisu walizokuwa wakiziendesha yeye na mwenyekiti dhidi ya lowasa..

Lakini Nape alikuwa na hiyari ya kukipigania chama cha mapinduzi sababu yeye ni mnufaika wa chama hicho..kwa upande mwingine yeye amenufaika zaidi na chama kuliko chama kunufaika na yeye sababu hata kabla ya yeye chama kilikuwa na watu waliokibeba..isipokuwa ye tunaweza kumsifia kwa kumfubaza lowasa ndani ya chama alipokuwa akishirikiana kufanya kazi hiyo na chadema Nje ya chama..kwa hili anastahili pongezi..

Nape ametajirika sana na kutembea kifua mbele kupitia ccm..nakumbuka juzi nilikuwa naangalia clip alipokuwa kwenye kampeni za urais iringa..
Katika ile clip nape anasema aliingia kwenye mgahawa akakuta wanacheck kampeni za chadema kwenye TV.

Akabet kwa mill 5 kuwa lowasa akiongea dk 15 anawapa hiyo pesa hapo hapo..na akatoa 1 mill kabisa.

Swali; hizi pesa zote za pocket money alikuwa anatoa wapi?? Nje ya ccm au ndani ya ccm..??
Kama pesa zote hizo alikuwa anazipata ndani ya ccm, je kulikuwa na haja ya kulalamika amekisaidia chama?? Maana alipata ujira mwingi na hata kujenga ghorofa ya kisasa kule salasala..

Hiyo ni sawa na wema kujiita kada wa ccm wakati alikuwa anafanya biashara na ccm na alilipwa pesa..
Kwa hili nape akiombe radhi chama.
 
Unataka Nape awe na moyo wa malaika kwa uongozi huu wa kina Bashite ??.

Nakumbuka siku Nape alipounda tume hii iliyompa Shida, Makonda aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook. Kuwa lazima Nape awe wa kwanza kung'oka. Je huoni nguvu ya Makonda kuendelea kuwakalia mawaziri wengine vibaya ?!

Kufanya madudu ya wazi lakini anaambiwa chapa kazi !!! Kwamba kughushi vyeti ni umbeya, kulazimishwa kurusha kipindi haramu kwa mtutu wa chuma eti nako ni embea

Hiki kipindi nacho kitapita na WaTz watasahau aina hii ya uswahiba ktk uendeshaji wa serikali
 
Mkuu, shooting ya hotuba na shooting za music/kwaya ni tofauti sana. Kwenye hotuba huwezi kariri kila kitu ulicho kirekodi huko studio halafu uje ufatishe vile vile wakati unahutubia, kua na akili walau kidogo.
But anyway, moral of your story:- Hakuna rafiki wala adui wa kudumu kwenye siasa, hata nyie wa kumfanyia hivyo Nape?
 
Ukweli kabisa Nape usisikilize mihemuko ya watu mitandaoni. Wengi wanaokupush wanataka udidimie kisiasa maana ukienda CHADEMA umekwishaaa. We kaa kimya muda si mrefu JPM akiona umetulia atakupa kiti kingine maana ni ukweli ulio wazi JPM anajua mchango wako mkubwa kwake na kwa CCM. Ona mama Anne alikaa kimya si kampa ubunge. Nchimbi pia si yuko ubalozi? we tulia ni muda tu. Kakuondoa sababu anajua waliokuwa wanakushinikiza kwa hili sio wema. Ampe ushindi gwajima we................................... labda sio JPM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…