Napendekeza kazi za kuhesabu idadi ya watu (Sensa 2022) ifanywe na wajumbe wa nyumba 10 , pesa zitakazookolewa zikajenge flyover TAZARA

Napendekeza kazi za kuhesabu idadi ya watu (Sensa 2022) ifanywe na wajumbe wa nyumba 10 , pesa zitakazookolewa zikajenge flyover TAZARA

Mzee kiufupi ni wengine tunazisubiria hizo kazi za muda ili tupate hata vimtaji.
Hasa national cake tutashare vp na sisi.
Wakati mwingine mbn huwa wanajibana matumizi lakini matokeo kwa. Wananchi huwa 0.

Hiyo hela watu wapewe wapige kazi.
Kama uko ofisini na unaandika uzi huu jua mtaani vijana hali siyo nzuri.
Uko sahihi lakini angalia upande wa ajira zilivyo ngumu. Ila kwa kuwa ni ajira tu ya muda basic ilete ahueni kiduchu.
Kuliko kuchezea resources at such a heinous scale, ni bora wawape mikopo isiyo na riba, mara 100 wafanye hivyo kuliko ajira za mchongo, za kufoji, za kufosi, no way!
 
Kwa taarifa yako ni kwamba katika kuhesabu watu mwaka huu makaratasi hayatakuwepo.
Wahusika watapewa electronic devices . Hivyo serikali itaokoa pesa nyingi ambazo zingewalipa maaskari walinda makaratasi, pesa za printing and photocopy n.k
Je, wajumbe wote wanajua kutumia hivyo vifaa?
Kama wana sifa waombe watapewa hiyo kazi
Lakini pia kumbuka kuwa wajumbe ni wanasiasa waliozalishwa na vyama vyao.
Je, ni sahihi hii kazi kufanywa kisiasa?
 
Sio kweli, wajumbe wote wanajua kusoma na kuandika, na kama walimpa ujumbe asiejua kusoma na kuandika, basi mwenyekiti na mtendaji wake watawajibika kumjazia hizo fomu, maana wao ndio wamefanya huo uhuni
Kwani katiba yetu inataja sifa za wajumbe wa mashina?
Je, moja ya sifa ni kujua kusoma na kuandika?
 
Wajumbe wengi hawajui kutumia kishkwambi
Mimi napendekeza wajumbe wajaze fomu kwenye makaratasi kisha afisa mtendaji azifanyie digitization na kuzituma kwa mamlaka husika kwa ajili ya uchakataji. Kumbuka, tablet haiuzwi buku 5, hizo pesa ni bora tukaboreshe miundo mbinu ya barabara na kuondoa foleni TAZARA
 
Ni wazo zuri lakini zingetumika kwa kila Kata kutatua changamoto za mitaa katika Kata! Mfano angalau hata kurekebisha miundo mbinu.
 
La saba wale wanajua hata kutumia kishkwambai?

Kiujumla sensa itatumia bil.629 ,,Aisee pesa nyingi sana hii Serikali iangalie nna ya kupunguza gharama.
Hizo tablet kwani zinauzwa buku 5, naoendekeza wajumbe wajaze kwenye fomu za karatasi kisha wampe afisa mtendaji azifanyie digitization na kuzituma kwa mamlaka husika kwa ajili ya uchakataji. Hizo pesa za kununualia Tablets ziende zikajenge flyover pale Tazara, hali ya foleni za malorry ni mbaya sana
 
Kiongozi wa 'malaika' alishajenga flyover TAZARA. Au unataka kufuta 'legacy' kwa kujenga nyingine?

Unawachokoza sukumagengi
 
Kiongozi wa 'malaika' alishajenga flyover TAZARA. Au unataka kufuta 'legacy' kwa kujenga nyingine?

Unawachokoza sukumagengi
 
Sensa ni zoezi kubwa na nyeti. Ndio maana shughuli zote nchini zitasimama kwa hiyo siku ya kuhesabu.

Kila mtu atahesabiwa sehemu ambapo zoezi litamkuta. Haya mambo yapo juu sana ya uwezo wa hao wajumbe.

Logistics zake ni zaidi ya hapo unapoona.

Ingekuwa ni rahisi hivyo hao wajumbe wangekuwa wanatuma taarifa kila mwisho wa mwaka, serikali ina update taarifa tu.

Isitoshe serikali ina hela nyingi sana, waache jobless wenzako wakapate hela hata ya vocha. Manake hata hiyo hela unayoiwazia inaweza isifanye kitu watu wakaipiga vilevile. Unawanyima masikini wenzako hela.
Kabisa mkuu.
Serikali Ina hela...
Jamaa anataka kuwazibia rizki graduates kibao walio mtaani na wana uhitaji wa hiyo hela.
 
Kwa lile zoezi la sensa lilivyo,linahitaji usmart Kwa sehemu Fulani ambao huo usmart sidhani kama wajumbe wanao.
Huo uwezo hawana,hata kama wanawajua vizuri watu Wao.

Acha graduate wapate hela,,,hii nchi siyo kila siku wanaokula hela ni walewale tu..the rest wanasota.
 
Kwa kupitia serikali za mitaa / vijiji (local government) , wajumbe wa nyumba 10 wapewe fomu za sensa na wapite kwenye nyumba zilizochini yao, wapewe wiki moja tu wawe wameshazitembelea nyumba zote zilizochini yao na kuzijaza fomu zote kwa kila nyumba, wakazikabidhi fomu hizo kwenye ofisi za serikali ya mtaa/kijiji, ofcourse wapewe na posho kidogo.

Afisa mtendaji akusanye zote na kuziwasilisha ofisi ya wilaya/mkoa ya sensa kwa ajili ya majumuisho na uchakataji wa taarifa.

Pesa zitakazookolewa ziende zikajenge flyover pale TAZARA, foleni ya malorry pale imesababisha hali kuwa mbaya sana.
Pesa zitafutwe na watanzania ziende zikajenge fly over Dar, si bora watu walambe usali tu kuliko huu ujinga uliouwaza.
 
Tumeshavuka huko kwenye peni na karatasi.
Kwahiyo siku hizi madukani hakuna peni na karatasi? Kama mwisho wa siku taarifa zinabadilishwa kuwa za kidijitali na kuchakatwa kidijitali, bado hakuna shida...
 
Hizo tablet kwani zinauzwa buku 5, naoendekeza wajumbe wajaze kwenye fomu za karatasi kisha wampe afisa mtendaji azifanyie digitization na kuzituma kwa mamlaka husika kwa ajili ya uchakataji. Hizo pesa za kununualia Tablets ziende zikajenge flyover pale Tazara, hali ya foleni za malorry ni mbaya sana
Hiyo Kazi atafanya pek yake? Yaani watu wa kata au kijij kizima au mtaa atafanya afisa mtendaji peke yake?
 
Mimi napendekeza wajumbe wajaze fomu kwenye makaratasi kisha afisa mtendaji azifanyie digitization na kuzituma kwa mamlaka husika kwa ajili ya uchakataji. Kumbuka, tablet haiuzwi buku 5, hizo pesa ni bora tukaboreshe miundo mbinu ya barabara na kuondoa foleni TAZARA
Kufanya gitization za data za kila mtu kivyakevyake mkuu ni cost sana. Kumbuka kwny sensa kila taarfa ya mtu huwa separate. Asa kijiji kina wananchi 5000 kwa mfano atafanya siku ngapi na kumbuka huyo mjumbe au Mtendaji hana jukumu moja. Ana majukumu mengine ya kiserikali
 
Kijana uko nyuma sanaa ya wakati, sensa ya mwaka huu inatumia technology ya kishikwambi ,madodoso yamewekwa huko.

Naona bado uko kipindi cha nyerere cha makarani kutembea na makaratasi na kuanza kupika data wakiwa chini ya mti.

Nchi nyingi duniani kwa sasa zimehama kwenye mafumo yako zinaenda kutumia technology ya kishikwambi kwenye kufanya tafiti.

Wewe unataka kuturudisha nyuma.

Nchi inapambana kusambaza umeme kila kona ya nchi ili tuweze kutumia technology kufanya mambo mengi wewe una discourage haya mambo.

Dogo nenda na wakati. Tulishatoka huko
Digitization bado iko palepale, wajumbe watachukua data kwa peni na karatasi, kisha afisa mtendaji ndio atazi-digitize hizo taarifa centrally na kuzihuisha, kisha atazituma kwa mamlaka husika kwa ajili ya sorting na uchakataji, tablet haziuzwi buku5 ndugu. Hizo pesa tukajenge flyover Tazara. Trillion 1 ni nyingi sana jamani.
 
Kwa taarifa yako ni kwamba katika kuhesabu watu mwaka huu makaratasi hayatakuwepo.
Wahusika watapewa electronic devices . Hivyo serikali itaokoa pesa nyingi ambazo zingewalipa maaskari walinda makaratasi, pesa za printing and photocopy n.k
Je, wajumbe wote wanajua kutumia hivyo vifaa?
Kama wana sifa waombe watapewa hiyo kazi
Lakini pia kumbuka kuwa wajumbe ni wanasiasa waliozalishwa na vyama vyao.
Je, ni sahihi hii kazi kufanywa kisiasa?
Wewe unanipa taarifa na mimi nakupa pendekezo. Napendekeza wajaze kwenye fomu kwa peni, kisha digitization ifanyike ofisini na afisa mtendaji kisha itumwe kwenye ofisi husika kwa ajili ya uchakataji, tablet moja unaweza kununulia karatasi za za mitaa hata 1000, na bado utagharamika kuzilinda hizo tablet vilevile, pesa itayookokewa ikajenge flyover pale TAZARA
 
Ni wazo zuri lakini zingetumika kwa kila Kata kutatua changamoto za mitaa katika Kata! Mfano angalau hata kurekebisha miundo mbinu.
Sio mbaya, ngoja tuzipambanie zipatikane kwanza, naambiwa zinaweza zikasitishwa
 
Back
Top Bottom