Kwa kupitia serikali za mitaa / vijiji (local government) , wajumbe wa nyumba 10 wapewe fomu za sensa na wapite kwenye nyumba zilizochini yao, wapewe wiki moja tu wawe wameshazitembelea nyumba zote zilizochini yao na kuzijaza fomu zote kwa kila nyumba, wakazikabidhi fomu hizo kwenye ofisi za serikali ya mtaa/kijiji, ofcourse wapewe na posho kidogo.
Afisa mtendaji akusanye zote na kuziwasilisha ofisi ya wilaya/mkoa ya sensa kwa ajili ya majumuisho na uchakataji wa taarifa.
Pesa zitakazookolewa ziende zikajenge flyover pale TAZARA, foleni ya malorry pale imesababisha hali kuwa mbaya sana.