Napendekeza mfumo wa ‘Randomizer’ kwenye usajili wa ‘plate number’ za magari nchini

Nina yangu huu mwaka wa sita, siendeshi kiunyonge kabisa, bali opposite yake, naendesha nikijiamini, kuna gari namba mpya saiv zinauzwa scraper, nilishafatwa watu wakasambaza story kwamba natembelea gari haina usajili maana hawakuwa wakiamini condition ya gari na plate number haziendani. Mtu ataachagari ipo condition nzuri atanunua gari ina namba mpya halafu imsumbue
 
Daah, ila plate namba ikishakuwa namba A, B , C, inakuwa shida sana hasa kwa watu wasiojielewa, dawa ni ku-randomize namba za usajili wa magari, hii itainua sana sekta ya ‘car restoration’ nchini na kuokoa fedha nyingi za kigeni zinazotumika kuagiza magari ‘restored/used’ ya Japan wakati tungeweza kufanya ‘restoration’ ya magari hapa hapa nchini na vijana wakapata ajira
 
Watu watataka entry document kutizama imeingia lini nchini 😀
 
Itunze gari yako. Gari za zamani zilizotunzwa zina bei kuliko gari mpya.
 
Kupata gari lenye hali nzuri hapa bongo yataka uwe mzoefu kwa kweli, kuna kubambikiana kwingi sana aisee
 
Nchi za East africa zingekuwa na uniformity ya kusajili licence plates.

Tutumie za kwetu ila bendera inakuwa na EAC.

Ile herufi ya mwanzo inaonesha nchi husika kama T au K au U au R au B au S au C.
 

Utaratibu huu nadhani ulikuwepo miaka ya nyuma nakumbuka gari zilisajiliwa kimkoa mfano Tabota zilianzia TB xxx, Tanga zilikua TAUxxxx Arusha ARS nk baadae ndio tukahamia hapa tulipo miaka hii ya karibuni nadhani serikali ilifanya hivi kwa kusudi na naloliona mimi ni za kiusalama zaidi kama source ya kutoa namba ni moja na kwa mtiririko mmoja ni ngumu sana kujirudia namba na ni rahisi kucontrol.
 
Sina uhakika na wanachofanya mataifa mengine yanayofanana na sisi, lakini ninachoona mimi wazo lako litawaongezea matapeli uwanja mpana zaidi wa kupiga pesa za wanunuaji wasiokuwa makini.

Tanzania tayari siyo mahali pa kuaminika sana kwa ununuzi wa vitu kama magari sababu ya utapeli unaowezeshwa na misrepresentation of facts. Mfano wanaofanya restoration kwa lengo la kuuza, huipamba gari kwa nje huku wakificha madhaifu ya ndani ili kupata bei nzuri.

Tukiongeza mwanya wa kuficha umri wa gari tutazidi kuongeza matatizo kwenye hii biashara. Ni afadhali mtu awe na taarifa sahihi za anachotaka kununua, zikiwepo zile zinazoonekana wazi pamoja na zile zinazomtaka akasome kwenye documents.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…