Igweeeeeeeeee,
Mambo vipi wakuu?
Nimekutana na comment hii hapa chini iliyojaa uzalendo, nikaona nii-copy na kui-paste hapa kama uzi unaojitegemea kulingana na umuhimu wake kwa nchi yetu.
Na kwa sababu sikumwomba ridhaa ya kufanya hiki nilichofanya, naomba anisamehe kwa sababu sitaweza kuweka hapa ID yake. Hivyo, ninaomba kuwajibika kwa huu uzi kama mmiliki wake kwa asilimia zote.
Sasa twende kazi......
Rais akifia Madarakani yapaswa baada ya kipindi kifupi cha siku 90 ufanyike uchaguzi, Makamu wa Rais anayekaimu ndani ya hizi siku 90 asiruhusiwe kugombea ndani ya awamu hiyo ya aliyefia madarakani, aruhusiwe kugombea awamu inayofuata baada ya ile ya kufiwa kwa kufuata demokrasi kama kawaida ya ndani ya chama chake cha siasa, na anayekaimu nafasi ya rais aliyeaga dunia ndani ya hizo siku 90 asiruhusiwe kufanya mabadiliko ya nyadhifa zozote ndani ya utawala uliokuwepo.
Pia asijulikane kama Rais wa awamu toauti na Rais aliyefariki, bali awe kiongozi wa mpito na awamu iendelee kuhesabika ni ya Rais aliyefariki akiwa madarakani kwa sababu ndiye aliyepewa ridhaa na wananchi.
Kingine, wakati wa kipindi hiki cha siku 90, Makamu wa Rais asiwe na ruhusa ya kusaini mikataba ya uwekezaji au ya aina yoyote mpaka uchaguzi ufanyike wa kumpata Rais wa awamu inayofuata.
Yeye Makamu wa Rais atumike kutuvusha tu kwa huo muda wa siku 90.
Tunatakiwa tuwe taifa lenye maono ya muda mrefu na kuwawekea kinga viongozi wetu ambao tunawapata kwa gharama kubwa sana hasa hasa wale wa nafasi ya Urais. Hivyo, inabidi tuwalinde kwa kadri inavyowezekana ili wasihujumiwe kwa hali yoyote ile.
Vinginevyo, nafasi ya Makamu wa Rais wa nchi yetu kwa fursa yake ilivyo inaendelea kuwa ni hatari ya wazi kabisa kwa Rais mchaguliwa endapo Makamu huyo akiingiwa na tamaa ya madaraka.
Naomba kuwasilisha.