Napendekeza Serikali ya Tanzania ichapishe Noti za Shilingi Elfu (50,000) na Laki moja (100,000)

Zipo sababu za kiuchumi kabisa kwanini hakuna noti za gharama kubwa na ndio maana Marekani pamoja na uchumi wake mkubwa hadi sasa nadhani bado pesa ya noti iliyo kubwa ni usd 100. Sijui kama kuna ya zaid ya hapo ingawa zilikuwepo miaka ya nyuma sana zikafutwa baada ya kuona balaa lake

Sasa kwa kinchi kama tanzania ambacho uchumi wake unasuasua eti unaweka Tsh 100,000/= iwe noti moja mtakuja kulia kilio cha mbwa koko nadhan na nchi ndio itafia hapo hapo maana yake hiyo ni dalili mbaya sana tena kwenye mstari mwekundu kabisa kiuchumi

Ni afadhari tupambane Tsh 500 irudi kwenye noti.
 
Zikitengenezwa chache sana, sidhani kama zitakua na athari inayohofiwa.
Wakati wa kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru, kulitengenezwa sarafu ya elfu 50, ni wangapi waliweza kuiona au kuishika sembuse kuimiliki.
Tungekuwa tumeshazama kwenye digital economy kusingekuwa na sababu, lakini bado tumeganda kwenye cash economy.
Juzi kati nimepita ofisi moja ya TRA, nikakuta kwenye dirisha la Benki kuna mtu analipia Kodi za Customs, hayo mabulungutu niliyoyaona hapo nikaacha mdomo wazi.
Nikajisemea mbona tumeambiwa miamala kwa kutumia cash mwisho milioni 5 lakini hapa ukizihisabu kwa kukisia hazipungui milioni 100?
 
Ili kuonesha uchumi unaimarika hata noti za 10k zilipaswa zisiwepo kwenye mzunguko na shilingi 50 bado ingekuwa inalipa hata nauli ya mwanafunzi kwenye daladala.

More zeros inaonesha unafilisika.
Sikutegemea kulisikia hili kwa "meneja wa makampuni"

Exactly
Thamani ya pesa ingekua ndogo sana ku compare na pesa zingine kama dollar.
 
Note kubwa kwa Baadhi ya nchi
1. Kenya note kubwa n 1,000
2. Dubai note kubwa n 500
3. Marekani note kubwa n 100$
Kuwa na pesa kubwa ya note kama 50,000 au 100,000. Ndio kuanguka kwa uchumi cz pesa inakua haina Thamani.
Uganda kuna note ya 50,000 angalia uchumi wao ulivo chini.
 
Huna nia njema na uchumi wa tanzania... Ikifikia hatua hiyo manake fedha ya tanzania haina thamani.... Ilitakiwa shiring 1, 5, 10, 20, ndo ziendelee kuwa za coin kwenye mzunguko na 50, 100, 200, 500, 1000,2000, 5000 na 10000 ziwe za noti lakini kwenye mzunguko wa noti ziwe 50, 100, 200, 1000 na 2000 ziwe kwenye atm na 5000 na 10000 ziwe zinatumika pale ambapo kuna biashara kubwa ya mafedha mengi Ili kuepusha kubeba mizigo ya fedha....

KWa namna ninavyo fahamu hiyo ndo sera ya uchumi nchi ikitaka fedha yake iwe na nguvu...... SAsa wewe sijui umekula maharage ya wapi? Au umetumwa kuja kutesti raia?
 
Mrengo wako yaezekana upo sahihi but in reality uchumi lazima ukuzwe kwa vitendo! Kuhusu hizo noti faida ni kupungua kubeba maburungutu meeengi wakat yana thaman ndogo!!
 
Natamani sana mtu kama 'Covax' akusome wewe hapa.

Sijui kama na wewe umesoma kiasi kile kile kinachomfikia yeye, lakini umetumia lugha na mifano ambayo kila mtu anaelewa unazungumza kitu gani.
Tena hukutumia maneno mengi sana ya kueleza 'concept' yenyewe uliyoilenga.

Kama wewe ni 'msomi', natamani sana tuwe na wasomi wengi kama wewe.

Mkuu 'Meneja', naona huyu ndugu hapa hujamsoma kuhusu hoja yake hii, ambayo mimi naamini amegusa penyewe kabisa kwenye mada yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…