Napinga IGP Sirro kukutana na Vyama vya Upinzani kwasababu hana hadhi ya kuwa mpatanishi

Wewe kwa akili zako nyingi unavyoona,hawa watawala wanaipeleka wapi ili Taifa?
Na wewe kwa akili zako nyingi unadhani Lema, Mbowe, Sugu, Msigwa, Mnyika na Pambalu watalipeleka wapi hili taifa wakipewa nchi?
 
Samia anakosea mno kutowasikiliza wapinzani atajutia baadaye.
 
I >100% support you.
 
Hatutashiriki vikao vya shetani

..Nadhani huu ni MTEGO kwa Chadema.

..Wanajua kwamba kutokana na waliyowatendea mtakataa kuonana na IGP na Msajili wa Vyama.

..Mnachotakiwa kufanya ni kukubali wito huo, na mkifika kwenye kikao muwashinde IGP na Msajili kwa hoja.

..Nina wasiwasi mkubwa sana kama kweli Msajili anataka kuitisha kikao hicho.

..Mnachotakiwa kukikataa na kusitisha makongamano bila kuwa mmepewa tarehe ambayo kikao kitafanyika.
 
Vyama vinavyo jitambua haviwezi kushiriki, hiki ni kiini macho.
Ila vyama mamluki vitajihimu napema tu.
Polisi ni nguvu za CCM, unategemea kuna la maana hapo.
CCM bila polisi imekufa.
 
Wakakae na maccm yao wawaeleze kuwa hawako tayari kuwatumikia kinyume na katiba

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Umenikumbusha watu wasiojulikana
 
Naunga mkono 100%
 
Msiposhiriki maana yake kila mkiandaa chochote mtatwangwa, amueni kusuka au kunyoa
Kwani miaka yoye si ndiyo kazi ambayo amekuwa akiifanya? Ambao amekuwa anawatwanga, bado wanaishi, ambao amekuwa anawakumbatia, baadhi hawapo.

Ulinzi wa anayeonewa hutoka kwa Mungu, na huo ni ulinzi mkubwa kuliko ulinzi wa vifaru 1,000 vilivyosheheni mabomu.

Mwenyezi Mungu, wakati tukishuhudia ukuu wako na kukunyenyekea kwa kila ambalo kwalo unatupitisha, hatukomi kuendelea kuomba ulinzi wako. Wafunike waja wako, wakae katika ulinzi upitao ulinzi wote, huku ukiwaonesha mawakala wa shetani jinsi ulivyo mkuu. Mapigo yako makubwa yawakumbushe na kuwafundisha kweli yako.
 
Mshiriki msishiriki hakuna athari yeyote Kwa nchi hi[emoji23][emoji1787]
Kwa kuwa mnajua hakuna athari, mnahangaika na kuandaa hiyo mikutano kwaajili ya nini? Si lengo ilikuwa kumtesa Mbowe? Tayari yupo mahabusu. Bado hamjaridhika tu?

Mna uwezo wote kwenye utawala wa shetani, lakini hamna chochote wala nguvu yoyote mbele ya utawala wa Mungu. Tukio la TAL vs JPM, kama mngekuwa na akili hata ndogo sana sawa na chembe ya haladali, mngekuwa mmejifunza, lakini shetani amewapofusha ili awapitisha kwenye uovu wote kabla ya kutambua kuwa mwisho wa waovu wote ni jehanamu.
 
Dua la kuku halimpati mwewe [emoji23][emoji1787]
 
Hakuna adhari kwa nchi? Unahisi mpaka wakaitisha kikao ni jambo dogo ee? Ukikua utaelewa nguvu ya upinzani ndani ya nchi.
Mnachezewa shere tu muingie kwenye 18, Tanzania hakuna upinzani kuna waropokaji tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…