Kwa miaka yote tangu ateuliwe kuwa IGP , Mtukufu Sirro amejipambanua kuwa upande wa ccm , huyu ndio chanzo cha vurugu kwenye harakati zote za kisiasa za vyama vya upinzani , ameshiriki kuvuruga , kuumiza na kuua Raia wasio na hatia kwenye mikutano na maandamano ya amani ya vyama vya siasa yasiyo na vurugu zozote , Ametumika sana na Serikali ya ccm kudanganya raia ili kunufaisha chama chake cha ccm , NENDENI TUNDUMA MKAJIONEE UNYAMA WALIOFANYIWA CHADEMA , Mauaji ya Akwilina na utekaji wa MO ni ushahidi wa uongo wa wazi na wa kishamba sana wa Simon Sirro , kama yeye mwenyewe au mpambe wake anabisha ajitokeze hadharani .
Mtesaji mkuu wa Wanasiasa wa Tanzania kwa awamu ya 5 na hii ya 6 ni Simon Sirro kupitia Jeshi analoliongoza la polisi , kwa kadri ya kumbukumbu zangu sijawahi kuona vurugu zozote za kisiasa zilizoanzishwa na upinzani , bali nimeshuhudia utesaji , manyanyaso , wizi wa kura wa aibu sana na utekaji wa viongozi wa upinzani ukisimamiwa na Jeshi la polisi lililo chini ya Sirro .
Mtu wa namna hii hana uwezo wa kuitisha kikao na vyama vya siasa vya upinzani kwa namna yoyote ile si tu kwa vile hana MAMLAKA YA KISHERIA YA KUFANYA HIVYO , Bali pia haaminiki na anao upande wake wa yule aliyemteua ambaye ni Mwenyekiti wa ccm .
NASHAURI CHAMA CHANGU CHA CHADEMA KUTOHUDHURIA KIKAO CHOCHOTE KITAKACHOITISHWA NA SIMON SIRRO akiwa yeye binafsi ama akivaa cheo cha IGP
NAKALA :
John Mnyika