Napitia changamoto kubwa, mke wangu anachanganyikiwa!

Napitia changamoto kubwa, mke wangu anachanganyikiwa!

Yaani inasikitisha na inahitaji uvumilivu,Tumeowana kama miaka 20 iliyopita tuna mtoto mmoja na mmoja alifariki.

Kama miaka 4 iliyopita hivi ndivyo mwenzangu alipoanza kupitia changamoto za kuchanganyikiwa, anaweza akaazisha zogo bila sababu kunituhumu namroga au mimi malaya,kila mtu kwake ni mchawi,yaani yeye ni mtu wa kulalamika tu, tuachane nimpe taraka na mambo chungu nzima
Anaweza anzisha zogo sehemu yoyote ile iwe kwenye gari sokoni au sehemu yoyote ile
Kwa kweli inahitaji moyo ukitegemea wakati namuowa alikuwa vizuri tu
Au aliambiwa umemtoa mtoto kafara
 
Jua hiloo mkuu ilimradi anakuzalia hanywi dawa basi lea watoto wako ukiingia ulizia watoto wako woi ukihitaji kubarikiwa anza na wazazi , ndugu , watoto wako . Basi .... mana mwanadamu ambaye hata hamjazaliwa naye ningumu kuweka asilimia 100 kumwamini
Ana mtoto mmoja tu wa miaka 18
 
Kipato kipo vizuri tu,ila inaitaji moyo sana,mfano anaweza kukuchenjia ndani ya basi akakunyan'ganya simu kukutuhumu unachati na wanawake na likawa zogo kubwa, au mko nyumbani ukachelewa kurudi sababu ya mihangaiko akaanzisha zogo,kuna wakati kama binadamu huwa najikuta nashindwa kuvumilia,
Pole sana. na wakati mgumu kweli kweli. Lakini hata mimi sishauri umwache. Usiishie kwenda hospital moja au kwa dr mmoja. Zunguka usichoke. Kama upo Tanzania ndiyo inakuwa tena ngumu zaidi kwa sababu hospital nyingi magonjwa kama haya hayana madaktari wazuri.
 
Kuboma una mchepuko ndio kamuamulia mkeo halafu mnapurukushiana kila wakati ni.kweli wanaume wa jf ni wachawi wengi wao hata mume wangu Tate Mkuu ni mchawi 🤣🤣🤣🤣 natania eh nampenda babe wangu .
Na mimi ni mganga mashuhuri wa kienyeji huku Kwa Msisi Tanga! Akitokea kijana akakumendea, namgeuza msukule mara moja. Sitaki utani hata kidogo. Na kama huamini, jiulize holoholo yuko wapi!
 
Pole sana mkuu.....kuhusu kurogwa inawezekana mkeo ana paranoid thoughts mpeleke hospitali hata pale mloganzila wana kitengo cha psychiatry nenda kapate msaada...

Kuhusu kuanzisha zogo na kukutuhumu unachat na wanawake wengine...mkeo ana insecurities, ushawahi kumcheat before??Epuka vitu/mazingira yote yanayoweza kumfanya suspicious....more importantly anahitaji reassuring...

Je akianzisha zogo wewe unaonyesha kuogopa? Don't feed her character..akianzisha zogo next time usionyeshhe kuwa intimidated wala usiwe aggressive subiri akitulia uongee nae firmly kuwa hupendi anachofanya, nini kinasababisha awe hivyo muulize na jinsi anavyodhani unaweza kumsaidia asirudie??? Take a note ..this is if she is mentally capable na anafanya makusudi...

Mwisho avoid vitu vote vinavyom trigger jaribu kuanzia sasa kuobserve hizo outbursts kama kuna patterns, ukishamsoma utajua kumkwepa...
 
Yaani inasikitisha na inahitaji uvumilivu,Tumeowana kama miaka 20 iliyopita tuna mtoto mmoja na mmoja alifariki.

Kama miaka 4 iliyopita hivi ndivyo mwenzangu alipoanza kupitia changamoto za kuchanganyikiwa, anaweza akaazisha zogo bila sababu kunituhumu namroga au mimi malaya,kila mtu kwake ni mchawi,yaani yeye ni mtu wa kulalamika tu, tuachane nimpe taraka na mambo chungu nzima
Anaweza anzisha zogo sehemu yoyote ile iwe kwenye gari sokoni au sehemu yoyote ile
Kwa kweli inahitaji moyo ukitegemea wakati namuowa alikuwa vizuri tu
Anakwenda makanisa yetu yale?
 
Pole sana mkuu.....kuhusu kurogwa inawezekana mkeo ana paranoid thoughts mpeleke hospitali hata pale mloganzila wana kitengo cha psychiatry nenda kapate msaada...

Kuhusu kuanzisha zogo na kukutuhumu unachat na wanawake wengine...mkeo ana insecurities, ushawahi kumcheat before??Epuka vitu/mazingira yote yanayoweza kumfanya suspicious....more importantly anahitaji reassuring...

Je akianzisha zogo wewe unaonyesha kuogopa? Don't feed her character..akianzisha zogo next time usionyeshhe kuwa intimidated wala usiwe aggressive subiri akitulia uongee nae firmly kuwa hupendi anachofanya, nini kinasababisha awe hivyo muulize na jinsi anavyodhani unaweza kumsaidia asirudie??? Take a note ..this is if she is mentally capable na anafanya makusudi...

Mwisho avoid vitu vote vinavyom trigger jaribu kuanzia sasa kuobserve hizo outbursts kama kuna patterns, ukishamsoma utajua kumkwepa...
Menopause inampa uchizi dada
 
Kwa maelekezo yako mafupi,binafsi naona ana kitu kinachoitwa sonono,hali ya kutokubaliana na jambo lililotokea ile simanzi ya kumpoteza mtoto bado inamuumiza na Ndio inayomfanya hawe mtu wa jaziba,lawama, anahisi dunia imemkatili ni vyema kama ukimtafuta daktari wa akili
 
Wah sasa umeoa mke mwingine au unaishije
Sijaoa, bado niko na huyu mke wangu,yaani siyo kwamba mda wote kachanganyikiwa hapana mda mwingi anakuwa vizuri tu na anasimamia majukumu yake kama mke,lakini ndiyo hivyo kuna wakati anabadilika yaani anaweza anzisha zogo bila sababu
 
Pole sana. na wakati mgumu kweli kweli. Lakini hata mimi sishauri umwache. Usiishie kwenda hospital moja au kwa dr mmoja. Zunguka usichoke. Kama upo Tanzania ndiyo inakuwa tena ngumu zaidi kwa sababu hospital nyingi magonjwa kama haya hayana madaktari wazuri.
yeah huo ugonjwa anatakiwa kutumia muda vizuri kwa mfano kama anaanza kumpeleka hospitali anatakiwa ahesabu muda vizuri yaani ndani ya miezi 3 hadi 6 awe ameshaanza kuona matokeo na dalili za mgonjwa kupata nafuu kutokana na dawa anazotumia,ukiona hii miezi yote ya tiba bado yuko vilevile jiongeze utafute njia mbadala hapa inabidi utumie skili yako maana hakuna atakayekwambia,daktari atafanya kazi yake aliyotumwa vitu vingine yeye havimuhusu na hatokwambia.
Kumbuka huu ugonjwa hospitali hawana vifaa vya kupima na kutoa majibu ya asilimia 100 kuonyesha chanzo cha tatizo isipokuwa daktari anatumia njia ya kumuhoji maswali ya kisaikolojia kisha anakwambia ni kweli huyu anaumwa ugonjwa wa akili na kwa kiwango chake cha kuvurugwa anastahili akae wodini au ukaishi naye nyumbani kisha uwe unakuja naye siku za kuhudhuria kliniki(haya nimeyashuhudia kwa macho yangu maana nilishawahi kuuguza wagonjwa wa aina hii).
 
Back
Top Bottom