BUNDUKI KUBWA
Member
- Feb 11, 2024
- 89
- 269
Huyo karogwa na mademu zako tu
Kuna wengine kama 2 walikuja kuniomba hela eti wanadaiwa kausha damu na waume zao hawajui. Na kausha damu wamekuja mtaani kwao wanawatafuta.Tunakopa kimya kimya hadi mkija kujua tushakuwa vichaa tunaokota makopo. Chukua hatua
Mhh ,huyo sio mzima kabisa. Ana matatizo🤣🤣🤣🤣 Afu ni kama ndivyo tulivyo
Kipenzi upo? Unaendeleaje mama?Mhh ,huyo sio mzima kabisa. Ana matatizo
Umri unaweza kuwq mdogo lakini akili zimeeka.Mimi Nina 41 yeye ana 39 hivi tumeshaanza kuzeeka eeh.
Salama za kwakoKipenzi upo? Unaendeleaje mama?
Njema tu namshukuru Mungu kwa kweliSalama za kwako
Watanzania wengi kila changamoto inahusishwa na kurogwa au mapepo. Ndio maana kutwa kuenda kwa wachungaji au waganga. Na matatizo yako palepale.Una uhakika hajajiunga na kakikundi ka kilokole?
Chunguza vizuri huenda amejiunga na kikundi fulani cha wanamaombi wanaoamini kila changamoto ni kurogwa.
Nakwambia maana mimi nina sister yeye kila mtu kwake ni mchawi kuanzia jirani, ndugu, wakwe kila mtu isipokuwa hao wana maombi wenzake.
Kila failure yake ni wachawi wanamroga.
Maombi yake ni ya kushambuliwa wachawi tu.
Nimefurahi kusikia umzima wa afya.Njema tu namshukuru Mungu kwa kweli
Mbona wanawake huwa wanawakimbia wanaume pindi wakiingia kwenye changamoto??Mpe upendo mwenzio. Utamuumiza sana ukimuacha. Huyo anakupenda ila anahitaji msaada wa kisaikolojia. Msaidie mwenzio,
be a man and hold that inconveniences with dignity and patience as a man, don't be like a boy to run away from disturbances
Akiwa kwako au akiwa kwenu/kwao wote mke na mume.Arudi kwao atibiwe,sijasema umwache.....mlitoa kwao mzima yote yametokea akiwa kwako na njia zote umemtumia imeshindikana...mrudishe home atakaa sawa,
Defensive mechanism baada ya kuhisi kupwaya eneo Fulani hasa kwenye uzazi!miaka 20 halafu watoto wawili!!?yaani mlipanga au ilitokea bahati mbaya!?Yaani inasikitisha na inahitaji uvumilivu,Tumeowana kama miaka 20 iliyopita tuna mtoto mmoja na mmoja alifariki.
Kama miaka 4 iliyopita hivi ndivyo mwenzangu alipoanza kupitia changamoto za kuchanganyikiwa, anaweza akaazisha zogo bila sababu kunituhumu namroga au mimi malaya,kila mtu kwake ni mchawi,yaani yeye ni mtu wa kulalamika tu, tuachane nimpe taraka na mambo chungu nzima
Anaweza anzisha zogo sehemu yoyote ile iwe kwenye gari sokoni au sehemu yoyote ile
Kwa kweli inahitaji moyo ukitegemea wakati namuowa alikuwa vizuri tu
Mkuu, tenda wema nenda zako. 80% ya wanawake hawana shukrani. Huyo unaweza mtendea wema, akapona kisha akakuacha akipiga pesa ndefu.Nampenda kwa kweli na huwa namuonyesha upendo wa hari ya juu sana,kumnunulia zawadi kumtoa out na vitu vingi ili kumpunguza mawazo,sababu naamini anayopitia hata mimi siku moja ninaweza kuja kuyapitia endapo nitamtendea vibaya basi na mimi nitakuja tendewa vibaya
Mkuu, umeingia kwenye akili yangu saa ngapi kuwaza kama mimi?? If it was the man who is in trouble, huyo mwanamke angekimbia..Swali la kujiuliza ni kwamba if the roles were reversed huyo mwanamke angemvumilia mshikaji?
Mimi ningemuacha mkuu. 80% ya hao watu ni wapumbavu sana.Usije kumuacha kisa ana matatizo..
Ngoja siku mkeo apige pesa ndefu kisha akikumbie au akutukane mbele ya kadamnasi ndipo akili zitakapokukaa sawa.Acha kulinganisha mwanaume na mwanamke, mwanaume ni kichwa cha familia hatakiwi kushindana na mwanamke.
Je umefanya jitihada gani hadi sasa kuhakikisha anapata tiba na kuwa sawa?Kama miaka 4 iliyopita hivi ndivyo mwenzangu alipoanza kupitia changamoto za kuchanganyikiwa
Tunajikazaga kisabuni wakati wenzetu yakitutokea kidogo tu wanatuachaMkuu, umeingia kwenye akili yangu saa ngapi kuwaza kama mimi?? If it was the man who is in trouble, huyo mwanamke angekimbia..
Mimi sina huruma na 80% ya wanawake kwa maana ni wapumbavu..Yaani ilianza kama utani familia yake ikaniambia nimpeleke kwa waganga,kutokana na imani yangu nikawakatalia,baadaye nikampeleka kwa dada yake maana hana baba wala mama,kibao kikanigeukia wakasema mganga kasema mimi ndiye ninayemloga, sijawahi kuloga hata kuku, mimi ni mfanyabiashara shughuli zangu nategemea ubunifu na akili yangu aliyonipa Mwenyezi Mungu,kaka zake wakaingilia kati ndiyo wakampeleka mloganzira,maana mimi siishi Tanzania,
Lakini kuna wakati akianza matatizo yake anasema hata mwanaye wa kumzaa aliyemaliza form four mwaka huu anamroga, sasa sijui ni mapepo au vipi ingawa najitaidi sana uvumilivu yaani ni mtihani mzito, unamuuguza mtu anayekutuhumu wewe mchawi inaitaji upendo wa hali juu sana