Napitia changamoto kubwa, mke wangu anachanganyikiwa!

Napitia changamoto kubwa, mke wangu anachanganyikiwa!

Kipato kipo vizuri tu,ila inaitaji moyo sana,mfano anaweza kukuchenjia ndani ya basi akakunyan'ganya simu kukutuhumu unachati na wanawake na likawa zogo kubwa, au mko nyumbani ukachelewa kurudi sababu ya mihangaiko akaanzisha zogo,kuna wakati kama binadamu huwa najikuta nashindwa kuvumilia,
Wahisha mirembe haraka sana.

Hizo ni dalili za ukichaa kabisa.

Angalia asijeanza kukudhuru
 
Kanisani huko watamchanganya kabisaaa mi nadhani ampeleke kwao ili tiba zikatafutiwe huko.
Huu ushauri si rafiki kwa maisha ya waTz walio wengi.

Ndoa wameishi miaka 20, wadhani wazazi wao watakuwa na umri gani kwa sasa na uwezo wao kiuchumi upoje?

Kumpeleka kwao ni kama kwenda kumdump na hali inaweza kuwa mbaya zaidi.

Hapo cha kufanya ni mume ampeleke mkewe kwenye hospitali zinazoshughulika na magonjwa ya akili period
 
Kuna jamaa huku jirani kwetu nae anapitia hali kama hyo ana watoto watano wakubwa tu

Ila yeye mkewe hana zogo ila ana mtuhumu jamaa anamroga,kuna wakat watoto wote na mama yao huondoka na kumuacha jamaa peke yake
Yaani watoto huwa wanalishwa sumu mbaya sana na mama zao,sembuse wakiwa wa kiume yanakuwaga poyoyo kwelikweli
 
Yaani inasikitisha na inahitaji uvumilivu,Tumeowana kama miaka 20 iliyopita tuna mtoto mmoja na mmoja alifariki.

Kama miaka 4 iliyopita hivi ndivyo mwenzangu alipoanza kupitia changamoto za kuchanganyikiwa, anaweza akaazisha zogo bila sababu kunituhumu namroga au mimi malaya,kila mtu kwake ni mchawi,yaani yeye ni mtu wa kulalamika tu, tuachane nimpe taraka na mambo chungu nzima
Anaweza anzisha zogo sehemu yoyote ile iwe kwenye gari sokoni au sehemu yoyote ile
Kwa kweli inahitaji moyo ukitegemea wakati namuowa alikuwa vizuri tu

Pole sana boss. Mambo ya duniani ni mengi. Nendeni kanisani (kwa waliookoka) muamue kumpa Yesu maisha yenu. Naona shetani ana nia ya kuisambaratisha ndoa yenu. Usikubali.

YESU NI BWANA&MWOKOZI
 
Mkuu kwanini umesema anachanganyikiwa? Kwenye uzi wako hujaonesha kama ana dalili za kuchanganyikiwa. Kukutuhumu umalaya, kumtuhumu kila mtu mchawi, kudai talaka, kuanzisha timbwili pasi na kujali mpo wapi hizo sio dalili za kuchanganyikiwa, unless useme viashiria vingine. Hivyo viashiria mbona wanawake wengi sana wanavyo mkuu? Mkuu kwa ulivyovisema, mkeo ni mzima ila tu anataka talaka, labda useme kiashiria kingine sio hivyo ulivyovitaja.
Ahaha. Usikute kwel manzi kamchoka mwamba.
Unachanganyikiwa mpaka unawaza talaka?
Talaka huwa inawazwa intentionally baada ya kufikiri kwa kina na ushauri ukatafuatwa.
Awe makini jamaa
 
Yaani inasikitisha na inahitaji uvumilivu,Tumeowana kama miaka 20 iliyopita tuna mtoto mmoja na mmoja alifariki.

Kama miaka 4 iliyopita hivi ndivyo mwenzangu alipoanza kupitia changamoto za kuchanganyikiwa, anaweza akaazisha zogo bila sababu kunituhumu namroga au mimi malaya,kila mtu kwake ni mchawi,yaani yeye ni mtu wa kulalamika tu, tuachane nimpe taraka na mambo chungu nzima
Anaweza anzisha zogo sehemu yoyote ile iwe kwenye gari sokoni au sehemu yoyote ile
Kwa kweli inahitaji moyo ukitegemea wakati namuowa alikuwa vizuri tu
Nendeni kwenye maombi, halafu hawezi kukusingingizia tu kuhusu umalaya, Kuna mapicha picha kayaona acha umalaya
 
Dasasa Ft Harmonize

Hata iwe mapenzi yamekwisha
Kumbuka Kuna mazoea🎶
Eeh Eeehh Baby uuuuhh
Mazoeaa🎶
Hata kama mapenzi yanakwisha
Yanabaki mazoea🎶
Eeh Eeehh uuuhh Baby eeeeh
Mazoea🎶

VERSE: 2

Nakunywa pombe nilewe sababu ni wewe, silewi zinanipaliaaaa 🎶🎶

ooohhh
uuuhhhu Uuuuh
Umenipatia🎶

Oooohh uuuhhhu
Unanijulia🎶🎶
 
Yaani ni yule mtu mnaweza kushinda naye vizuri tu,lakini anachokiwaza yeye anachukulia kama ni kweli umekifanya na ndipo anapoanza kuongea au kulalamika kwa sauti
Pole. Au ni menopause? Hii nayo inatusumbua wanawake wa kuanzia 45+
 
Kwanini wafrika tunapenda waza waswala ya Imani imani(Dini au waganga) wakati hilo swala liko wazi ni matatizo ya akili .

Huo muda anahangaika na wachungaji ambao hawatamsaidia kitu angetakiwa ahangaike na hospitali za akili aweze tatuliwa changamoto yake.

Tatizo mtu anakuwa na tatizo la akili(ukichaa) hatupendi kukubali tunaamini linatibika tuu kawaida kumbe hapana.

Mtu akiambiwa mpeleke mgonjwa MIREMBE anahisi kama anamdhalilisha mgonjwa kumbe ndo sehemu sahihi.
Mkuu ni kweli kuna uwezekano akawa ana matatizo ya akili.
Lakini hayo matatizo ya akili yamegawanyika aina nyingi.
Kuna ambao unasababishwa na utumiaji wa madawa ya kulevya/bangi,kuna mwingine unasababishwa Stress/depression na kuna mwingine unasababishwa na kurogwa hio ipo wala usipinge na kujifanya wewe ni mzungu.
Kuna jamaa mmoja namfahamu anatumia dawa za hospitali kwa miaka 20 na hajapona wewe unadhani itakuwa ni kitu gani kama sio kurogwa?
Cha msingi tumshauri mtoa mada ajaribu kotekote hatuwezi kujua ni wapi atakapopata unafuu.
 
Yaani ni yule mtu mnaweza kushinda naye vizuri tu,lakini anachokiwaza yeye anachukulia kama ni kweli umekifanya na ndipo anapoanza kuongea au kulalamika kwa sauti
Mkuu nicheki pm nikushauri kitu nimeshakutana na watu wengi wa aina hiyo najua kinachomsibu.
 
jamiii yoyote yenye imani kali juu ya mambo ya kiroho huwa ina matatizo

maana makanisani mahubiri yamejaa stori za kurogwa na stori shetani. na wakienda kwa mganga napo wanajazwa ujinga wa kurogwa na majini

hivyo wanaamini ni kweli
Na hiyo familia ni watu wa kusali,wote baba mama na watoto ni wahudhuriaji wazuri wa hospital
 
Yaani inasikitisha na inahitaji uvumilivu,Tumeowana kama miaka 20 iliyopita tuna mtoto mmoja na mmoja alifariki.

Kama miaka 4 iliyopita hivi ndivyo mwenzangu alipoanza kupitia changamoto za kuchanganyikiwa, anaweza akaazisha zogo bila sababu kunituhumu namroga au mimi malaya,kila mtu kwake ni mchawi,yaani yeye ni mtu wa kulalamika tu, tuachane nimpe taraka na mambo chungu nzima
Anaweza anzisha zogo sehemu yoyote ile iwe kwenye gari sokoni au sehemu yoyote ile
Kwa kweli inahitaji moyo ukitegemea wakati namuowa alikuwa vizuri tu
Kwanza pole,hayo ni matokeo ya kitu ambacho anakitaka kwa udi na uvumba sasa hakipati,ndio anazusha hizo tabia,kuwa mpole na tafuta mwanasaikolojia akusaidie
 
Wak
Kwanini wafrika tunapenda waza waswala ya Imani imani(Dini au waganga) wakati hilo swala liko wazi ni matatizo ya akili .

Huo muda anahangaika na wachungaji ambao hawatamsaidia kitu angetakiwa ahangaike na hospitali za akili aweze tatuliwa changamoto yake.

Tatizo mtu anakuwa na tatizo la akili(ukichaa) hatupendi kukubali tunaamini linatibika tuu kawaida kumbe hapana.

Mtu akiambiwa mpeleke mgonjwa MIREMBE anahisi kama anamdhalilisha mgonjwa kumbe ndo sehemu sahihi.

Sometimes ni Mambo ya kiimani kwenye baadhi ya Koo.

Kuna baba yetu mdg alikua na hili tatizo la kuchanganyikiwa, lkn historia inasema kuna babu yao alikua mganga by the time anafariki alimpendekeza yeye atakuja kurith hyo mikoba yake ambapo muhusika alikataa ndo yakaanza kumuandama na kumchanganya from time to time till death.
 
Back
Top Bottom