Hivi karibuni, wanasayansi kutoka NASA wamedaiwa kwenda mwezini kutalii na kupiga picha kupitia misheni ya
Artemis II, na hatimaye kurudi Duniani. Jambo hili, kama mwanasayansi, nalipongeza sana. Asiyefurahi kwa kidogo hata kikubwa hawezi kupewa; nimefurahi kupata picha kuanzia tukio linaanza mpaka lilipofika hapa.
Lakini, pongezi hizi zinakuja na mashaka mazito. Ikiwa tuliweza kufika na kutua mwezini miaka 60 iliyopita na teknolojia ya "analog," kwanini leo, tukiwa na teknolojia ya hali ya juu kuliko wakati wowote, tushindwe kwenda, kutua, na kutuonyesha kila kitu
mubashara (LIVE) bila chenga? Kwanini tunapewa picha za vipande vipande badala ya video inayotiririka kuanzia kuondoka mpaka kutua? na kipi kinawazuia wasiende mwezini wakatembee na kuweka bendera kama wenzao wa Apollo?
Baada ya chombo cha Artemis kuanza safari yake kuelekea mwezini, picha na video zilizotumwa zimezua maswali mengi kuliko majibu. Video hizi zinaonyesha Dunia ikiwa imetulia tuli (
Still). Tangu tarehe 2 mpaka leo, picha zinaonyesha upande ule ule wa bara la Afrika kana kwamba Dunia imeganda.
Hii imenileta maka kwenye maswali makuu ya kimantiki:
- Kasi ya Ajabu Iko Wapi? Tuliaminishwa na kufundishwa tangu shule ya msingi kuwa Dunia inazunguka kwenye mhimili wake kwa kasi ya zaidi ya kilomita 1,600 kwa saa. Kwa kasi hiyo, ndani ya saa chache tu tulipaswa kuona mabara yakipishana na sura ya Dunia ikibadilika kwa haraka. Lakini kwenye video ya NASA, Dunia haisogei, haizunguki, wala haina dalili yoyote ya mwendo.
- Mawingu Yaliyoganda: Tunajua kuwa angahewa ina upepo na mifumo ya hali ya hewa inayobadilika kila sekunde. Inakuwaje kwenye video hizi mawingu yanaonekana yakiwa yameganda mahali pale pale kwa muda mrefu? Je, ni kweli haya ni mawingu ya asili au ni picha tu ya kutengeneza iliyowekwa nyuma ya chombo?
- Mvuto wa Centrifugal (Centrifugal) : Sayansi inasema kitu kinachozunguka kwa kasi lazima kirishe vitu nje au kionyeshe mabadiliko ya umbo (bulge). Mbona hapa tunaona duara kamilifu lililotulia kama picha ya ukutani?
Kama mwanasayansi, nakubali maendeleo, lakini siwezi kukubali maswali bila majibu. Ikiwa picha zinatuonyesha Dunia imetulia, na macho yetu hayaoni mzunguko ule wa kilomita 1,600 kwa saa, basi kuna mambo mawili: Ama
tulidanganywa kuhusu kasi ya mzunguko wa Dunia tangu awali, au picha tunazopewa na NASA si za kweli (CGI).
View attachment 3568900
hii ni viddeo ya leo ya nasa ambayo upande huo wa Afrika unafanana kama video ya Nasa ya kwanza kipindi wanatoka duniani..
View attachment 3568902View attachment 3568903View attachment 3568904