NASA mbona haieleweki kuhusu kupeleka watu mwezini?

Sasa wewe na hiyo elimu yako ya secular mbona imekufanya kuwa mjinga zaidi ? Kama hata kuhoji juu ya habari za anga unashindwa, na unatoka kirua mbele na kunadi uongo huu, wewe ndiyo mjinga zaidi.

Hao wata shutumiwa kwa kukudanganya wewe na huenda wewe hukuwaelewa ila kwa maarifa na utambuzi wa mambo huwezi kuwafikia.

Akili mmepewa bure zitumieni aisee.
 
A
Ndugu leta facts zinazoprove uwepo wa uzio na sio imani kama ulibyojibu

Unataka facts gani labda ? Hiyo niliyo ni facts. Sasa wewe utuonyeshe nani aliwahi kwenda mwezini na uonyeshe ukweli wa hizo habari.
 
Kabla ya atmosphere,? 😁 Hapo tunatoka na kuingia karbu kila siku
 
Ndugu leta facts zinazoprove uwepo wa uzio na sio imani kama ulibyojibu
Unajua mpaka muda huu hamjaleta facts hata mona kuhusu hii kadhia ? Zaidi ya stori na kudhihaki watu.

Facts tumeleta sisi, kwamba huwezi kupasua anga mpaka kwa idhini ya Mola na hiyo idhini haijatolewa ndiyo maana NASA wanaendelea maigizo yao huko Area 51. Kila wakitoa habari zao wenye akili na kufikiria kiundani wanaona dosari.
 
Mimi sijasapoti inshu ya NASA kufika huko....lakini pia sikubaliani na wewe kwamba sababu ni uzio kama unavyodai kwa sababu hoja yako ime base zaidi kwenye imani which is intangible..
 
Mimi sijasapoti inshu ya NASA kufika huko....lakini pia sikubaliani na wewe kwamba sababu ni uzio kama unavyodai kwa sababu hoja yako ime base zaidi kwenye imani which is intangible..
Njaa ni tangible au kinyume chake ? Ila unakubali uwepo wake sababu kuna ishara za kuwepo hilo. Yaani siyo mpaka uone bali unapata jibu kwa kinyume chake.

Dini (Hapa naongelea Uislamu, sijui kuhusu dini nyingine) inatoa muongozo na kusema ya kweli, kitendo cha wao kushindwa kufika huko ni ishara na ni uthibitisho ya kuwa hilo haliwezekani. Sasa wanacho fanya ni maigizo na kuwadanganya watu kwa picha bunifu.
 
Heheheee
Mdili namada iliopo jukwaani achana na huyo jirani yako
Mana yeye kafeli tayari sababu hata aya yamwanzo kabisa imeshuka ikalazimisha ama kusisitiza kuhusiana na kusoma
Haijataja elimu ipi ila elimu zote inatakiwa uzisome kwafaida yako najamii kwaujumla
Iqraa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nasema ndio naamini watu walikwenda mwezini.
Wewe ndio unatakiwa uthibitishe kwamba hakuna mtu aliyekwenda mwezini.
 
"Kitendo cha wao kusema wanaenda kuangalia kama kuna usalama wa kupeleka tena binadamu siku zijazo ni kauli tosha kusema hawajawahi kupeleka binadamu mwezini."

Neno kama kuna usalama umelitafsiri vp mpaka ulitumie katika hitimisho lako?
 
Usalama wa spacecraft itself plus data collection. and the safety of specified environment if it's suitable enough for human activities and residential usage.
Kitu ambacho hawakufanya miaka 53 nyuma.
 
Mimi nasema ndio naamini watu walikwenda mwezini.
Wewe ndio unatakiwa uthibitishe kwamba hakuna mtu aliyekwenda mwezini.
Wewe unao ushahidi kuonyesha mtu alienda mwezini ?

Jukumu la kuthubitisha sio kwangu tu hata wewe ni jukumu lako. Mimi nimeshakupa kanuni ya ujumla su jibu la ujumla kwalo limeshakata, kwamba si tu wanadamu bali mpaka majini hawawezi kuvuka hilo anga na kukaribia hiyo mbingu ya kwanza.

Mmewekewa aya huko mwanzo, sasa ili ionekane aya ni ya uongo wekeni ushahidi wa kweli kuonyesha kuna mtu au kuna watu walikwenda mwezini. Sasa msituletee stori za vijiweni sisi tunataka uhalisia (facts).
 
Wao NASA kama NASA specifically wanapata faida gani kukuongopea wewe?
 
Wao NASA kama NASA specifically wanapata faida gani kukuongopea wewe?
Swali zuri, ushawahi kujiuliza kwanini wanaongopa ?

Kwao faida wanapata kubwa sana, katika kujiweka katika sehemu ambayo si yao hii ni faida yaani kusifiwa na kufanya waogopwe na kutukuzwa.
 
Unajua maana ya "imani"?
Mimi nimeshakwambia ndio naamini watu walikwenda mwezini.
Sasa wewe unataka uthibitisho au ushahidi gani?

Kazi iliyobaki ni wewe kuthibitisha kwamba hakuna mtu alikwenda mwezini na kwanini.
 
Swali zuri, ushawahi kujiuliza kwanini wanaongopa ?

Kwao faida wanapata kubwa sana, katika kujiweka katika sehemu ambayo si yao hii ni faida yaani kusifiwa na kufanya waogopwe na kutukuzwa.
Mimi nimeshajiuliza kwanini waongope na jibu nililopata ni hakuna faida yoyote watakayopata wakiongopa.

Sasa niambie point ipo wapi hapo kwenye kusifiwa, kuogopwa na kutukuzwa kama unavyosema na kunawafaidisha vipi NASA developmentally, Physically, Economically na Scientifically?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…