Usiwadanganye wenzio...
Shida ni moja...
Wanawake, hasa msipojiangalia, kipindi kile cha usichana - kipindi cha kuchanua vyema kama ua waridi na kila nyuki msituni kutamani kulichavusha - huwa kinapita haraka sana. Miaka 35 huko wengi wameshaanza kuchakaa wakati huku mtaani ndo kwanza wasichana kibao wanayaanza maisha. Ni kanuni ya supply and demand. Supply ni kubwa, demand ni kidogo hasa kipindi hiki ambapo vijana wengi hawataki kuoa (mapema)
Halafu mwanamke akifika 35 huko hajapata mtoto wake wa kwanza, probability ya kupata changamoto za uzazi inaongezeka sana...ikiwemo kuzaa watoto wenye matatizo...
Kwa hiyo usiwadanganye. Acha waolewe kabla hawajavuka 30 maana wakivuka hapo changamoto ni nyingi sana. Na kwa kizazi hiki cha sasa hakuna guarantee kuwa hata wakivuka 30 huko ndo watakuwa wamekomaa na kuwa wake wema. Kama ni pasua kichwa ni pasua kichwa tu hata umuoe akiwa 40s+. Nina mifano dhahiri!
Kwa ujumla tu haya mambo hayana fomyula.