Nchi hii ina chembechembe za udini toka awamu ya kwanza tena nyie msiokuwa waislamu ndio mna chuki zaidi
Lakini cha ajabu wapiga kura wengi ni wale wanasema wanabaguliwa na wengi ndio hao hao wanaowapa madaraka hao waliowabagua tangu hiyo unayosema awamu ya kwanza.
Lakini Tanzania hatukuanza kutawaliwa na awamu ya kwanza.
Watawala walianza tangu Ujima wakaja Waarabu ,Wareno,Wajerumani, Waingereza na sasa tunatawaliwa tena kama wakati wa ujima na wale tunaofanana nao.
Lakini wakati wote huo watawala wanatawala kwa kuweka mbele Maslahi yao. Enzi za ujima palikua na watawala na viongozi wa dini zetu za asili. Hawajawahi kuchangamana hao watu zaidi ya kila mmoja kumtumia mwenzake kwa manufaa yake.
Wakati wote ardhi ya mtu mweusi imekua na wageni kutoka nje.
Waarabu walitawala karibu Afika nzima na dunia nzima.
Lakini bado binadam hakukosa malalamiko. Wachache walinufaika lakini wengi waliumizwa ndio maana walipokuja Wale wa magharibi watu waliwaunga mkono na kuwatoa waarabu kwenye utawala. Hata hao wa wazungu nao waliwanufaisha wachache na wengi wakaumia. Wakaja wakina Tundu Lisu wa wakati huo waliowapinga watawala dhalimu na kuwatoa wazungu . Lakini bado walionufaika ni wachache wengi wakabaki hohehahe mpaka Leo.
Kifupi Ukisikia serikali inasema haina dini ujue haina dini kweli kweli. Wanachojua ni maslahi yao tuu. Mtu akikuambia hana dini ujue haamini katika kutenda mema na haki anachojua ni kulinda kile anachoona kinamnufaisha yeye kama binadam ikiwemo madaraka yake.
Ma ndicho kinachofanyika. Wakigundua kuwa waislam wamewakubali na kuwakumbatia watajipendekeza kwa wakristo na kujifanya kuwa ni zamu yao na wanawafurahisha . Wakigundua kuwa Wakristo wqmewaelewa basi watajipendekeza kwa waislam ili waonekane kuwa wanawasidia na kuwajali. Lakini ukweli ni kuwa ni kakundi ka watu wachache sana wenye akili na ujanja mwingi wanaoangalia maslahi yao.
Wajanja wachache wanatumia chama kushika dola ya nchi na kumimina fedha kwenye mifuko yao. Dini kwao sio ishu wakishashika dola.
Kwa hiyo kusema kuwa labda watawala wanapendelea dini Fulani sio kweli . Wanachoangalia ni kucheza na akili za waumini.
Wakijua kuwa dini zinaona kuwa tabia Fulani ni dhambi kubwa basi watajifanya wanaichukia na kupambana nayo ili wapate kura na kushika madaraka yao na kula bata. Wakati huo huo hawaoni kuwa ni dhambi kula rushwa, kupindua na kutamka idadi ya kura za uongo na kumpa ushindi asiyeshinda.
Hawajui kuwa Serikali ndiyo inayotakiwa kutoa sadaka ya Fungu la kumi la mapato ya serikali kwenye dini na sio serikali kujaribu kuchukua kule kwenye miradi ya dini.
Hata hizo Jezi tusikurupuke kulaumu serikali bila kujua nani aliyeweka order ya kuzitengeneza . Huenda ni wachina wenyewe na wapiga kamari Wa Sport pesa ambao hawajui hata masuala ya Msalaba.
Ndio maana hata hizo jezi ukiuliza vizuri utagundua kuwa waliozinunua hawakua hata wale wanaoukubali msalaba.
Sent using
Jamii Forums mobile app