Nashauri safari za mabasi kutembea saa 24 zisitishwe, vifo vitamaliza watu

Magari ya usiku kutokea Moshi niliyopanda yanatembea 80kms sijaona linalokimbia zaidi hivyo ni mwendo salama kabisa kwa usiku.
Labda ungeshauri wamiliki wa mabasi wahakikishe, wanaoendesha usiku ni wale wasio na upungufu wa nguvu za macho (uoni hafifu); kwani hilo ndilo laweza kuwa tatizo
 
Spidi za gari zimewekwa zifikiwe hizo 80 ndogo sana Kwa safari ndefu

Dereva aongeze mwendo
 
kama uliambiwa saa 7-8 unasinzia sababu ya kuvimbiwa,vipi usiku ambao kiasili ni muda wa kulala kabisa!!!
Fanya utafiti kama pia unasafiri na gari ya abiria (sio binafsi) mida gani abilia wanaacha kupiga stories na wanasinzia.
 
mtu anafanya kosa bongo analipishwa 30k😁😁😁.

hakuna kitu tuko serious.
yani hata ukikuta dereva analalamika,basi ni kwa kutoa 30 sio kujuta kwa janga alilotaka kusababisha.
Na ajali hazitaisha maisha yote na watu wataendelea kufa bila hata malipo
Mtu anawasha mziki mkubwa hata gari ikiwa inatoa sauti ya ajabu wao hawana Habari
Anakuja kushutuka gari linawaka moto

Halafu kuna wapumbavu wanafurahia kelele za mziki sijui huwa hawana mziki makwao
Ajali nyingi ni uzembe na wengine walevi

Kuna siku traffic police katusimamisha kamkuta dereva kalewa vibaya
Akamwambia yaani wewe una matatizo
Oyaa konda njoo uendeshe
Yaani simple utakuta jamaa amekula hela zake sana mpaka anamuogopa mlevi ila hajali maisha ya watu 60
 
Hata toyo hajawahi kumiliki huyu mpuuzi
 
Nakubaliana na wewe.

Licha ya ajali za barabarani hata usalama wa watu kwenda stend saa kumi za usiku pia haupo.

Nilienda kwetu huko kuuliza bus la kurudi dsm naambiwa yanapita saa kumi za alfajiri.

Bahati tu nilikuwa na namba ya taxi, sijui kama nitaenda tena huko.
 

Wabongo tunapenda majungu sana….sijui tuna shida gani….hebu weka record ya hizo ajari zilizotokea usiku..
 
Msiturudishe kwenye maisha ya ujima ndugu, safari za usiku zimekuwa msaada mkubwa sana kwa wananchi, hivi ninavyoongea nineingia Arusha nashiriki kikao hapa Tanroads jioni nageuza,

Katika nchi zilizoendelea safari zinatakiwa ziwe masaa 24, dunia imebadilika sana
 
kuna watu mnapenda nchi iwe gizani,safari za siku ni nzuri mfano juzi nilitakiwa niende mbeya na kurudi nilifankisha kwa ajili ya mabus ya jioni. Na kwa sasa abiria wapo wengi sana wa usiku kuliko mchana. Ninachoona changamoto zitatuliwe na si kusitisha huduma.
 
Wabongo tunapenda majungu sana….sijui tuna shida gani….hebu weka record ya hizo ajari zilizotokea usiku..
Achana nao Mkuu! Serikali imefanya vizuri kuruhusu safari za usiku.
Kama wao wanaona shida kusafiri usiku wasafiri mida walioizoea.
Wengine wanapenda kulakula wakiwa safarini. Wakiona mayai lete, wakiona mahindi lete, wakiona miguu ya kuku shida.
Sasa safari za usiku hazina mambo hay
o.
 
Gari hifanyiwi service kila siku. Inafanyiwa kila baada ya kutembea kilometa kadhaa, mara nyingi kila baada ya kilometa 3000 mpaka 10,000 kutegemea na hali ya chombo husika. Hata ndege, inatoka Dar, inafika Dubai inashusha abiria na inageuka baada ya muda mfupi haifanyiwi service muda huo huo.
Suala la ajali pia linahusu sana oversight ya polisi na LATRA. Ni sheria kwamba kila basi linaloenda mbali shurti liwe na madereva wawili wanaopokezana. Kwa hio LATRA hasa ndio inatakiwa wahalikishe hilo linazongatiwa
 
Kama hakuna data zinazoonesha ajali za usiku ni nyingi kuliko za mchana basi, hii hoja haina mashiko.

Tupende kutafuta data kwanza. Huu ni uchumi,kazi za watu.
Sahihi
 
TATIZO KUBWA ZAIDI Dereva kuendesha gari zaidi ya 1,000km peke yake.
Hii ni hatari kubwa.

Last week nimetoka mpanda na bus la AN CLASSIC, saa 12 kamili asubuhi hadi Dar saa 8 usiku, aliendesha Dereva mmoja, umbali wa km 1,188, hii ni hatari kubwa mnoo
 
Basi la Baraka liliua watu 14 na ajali ilitokea jua linaiangazia hiyo ajali, na zipo ajali nyingi zimetokea huku jua likishuhudia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…