Nashauri safari za mabasi kutembea saa 24 zisitishwe, vifo vitamaliza watu

Nashauri safari za mabasi kutembea saa 24 zisitishwe, vifo vitamaliza watu

Gari lingekua lako ungefanya service ukifika dar na ukifika moro unafanya ungeweza. Mbona unaongea vitu vya ajabu sana.
Gari hizo zina ratba yake ya service sio kila siku. Unadhani service ni kuweka mafuta.
Unajua ifike mahali wana jf kama hujui uliza.. Gari hujawahi miliki unaanza leta stry za service every return day. Daah
Watanzania wanaendeshwa na hisia kuliko akili
 
serikali ya kufanya tathmini ukaiamini ni hii hii ya akina tulia ya ccm au unazungumzia serikali nyingine!!!

siasa zinatumika juu ya vichwa vya wajinga kuamua hatma ya maisha yao.

wadau wa usalama barabarani wanapendekeza gari za abiria zisitembee usiku,anakuja mtu aliyeacha kupanda bus miaka 15 iliyopita anakwambia sio uamuzi salama kiuchumi,uchumi wa ugoko!!!
wenzenu wanapotaja uchumi wanataja na barabara 6 zinazotenganishwa na ukuta 3/3,nyie moja mpaka chokaa katika [emoji29][emoji29]
Acha kelele zako,
Leta takwimu zinazoonyesha basi za abiria kusafiri mchana ni salama zaidi kuliko usiku.
Leta idadi ya ajali zilizotokea usiku dhidi ya zile za mchana. Vinginevyo wewe na wenzako wa aina yako ni wa kupuuzwa tu.
 
Ila kwetu inahitaji uangalizi na mafunzo ya hali ya juu kwa madereva
Ulaya kupata license ya bus au lorry sio mchezo inaweza kufika mpaka 12m ya bongo
Mimi nilichukua kwa 10m ya kitanzania na nilisoma haswa
Maswali 900 lazima ukariri
Mtihani maswali ni 100 kutoka hayo 900 na lazima upasi zaidi ya 70 %
Unatoka umenolewa haswa
Changamoto ni vihiyo na wajinga kuwa wengi katika jamii na vivyo hivyo kwenye mamlaka za usimamizi na utoaji leseni.
Matajiri wenye magari kwa sababu ya ujinga wa jumla wanawakabidhi vijana wapuuzi waliopitishwa na mamlaka bila weledi, magari ya thamani kubwa na maisha ya abiria.
Watu wengi huangamia kwa kukosa maarifa na weledi katika taifa kwa ujumla.
 
hamna shida amkeni tu,ila msisahau barabara zenu ni vichochoro,hata taa hakuna.

wenzenu wanaamka huku wanawajibika,nyinyi mnaamka huku mnapiga siasa tu.
Suluhisho ni kupanua barabara sasa sio kuwafanya watu wasifanye kazi usiku.
 
Kama hakuna data zinazoonesha ajali za usiku ni nyingi kuliko za mchana basi, hii hoja haina mashiko.

Tupende kutafuta data kwanza. Huu ni uchumi,kazi za watu.
Huwezi amini usiku abiria ni wengi sana
 
Nakubaliana na wewe.

Licha ya ajali za barabarani hata usalama wa watu kwenda stend saa kumi za usiku pia haupo.

Nilienda kwetu huko kuuliza bus la kurudi dsm naambiwa yanapita saa kumi za alfajiri.

Bahati tu nilikuwa na namba ya taxi, sijui kama nitaenda tena huko.
Kama unapotokea kuna vibaka sana basi panda gari za saa mbili asubuhi, sio lazima kusafiri na linaloanza safari saa kumi usiku.
 
mtu anatoa ushauri safari zisitishwe wanatokea wanywa mbege, ulanzi na konyagi huko kelele nyingi hatutaki wewe acha sijui nzuri sijui fwee fwee,
kwa nini miaka yote safari hua zinazuiwa? na wanaruhusu tena,
hata mimi nashauri uthibiti uongezeke hakuna asiyejua hawa madereva wa masafa ukiacha speed kali wanaendesha hovyo kweli kweli peke yao ndo wanawahi wanakoenda

na wahuni wamepandisha nauli hivi wafute kabisa safari za usiku nyambafu.
 
Achana nao Mkuu! Serikali imefanya vizuri kuruhusu safari za usiku.
Kama wao wanaona shida kusafiri usiku wasafiri mida walioizoea.
Wengine wanapenda kulakula wakiwa safarini. Wakiona mayai lete, wakiona mahindi lete, wakiona miguu ya kuku shida.
Sasa safari za usiku hazina mambo hay
o.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Tujifunze kuleta mawazo ya kuboresha, sio kufungia na kusitisha tu. Labda pia uje na takwimu za ku-support hoja yako

Mchana mabasi yanasafiri mangapi? Ajali zake ziko ngapi? Vifo vingapi? halafu fananisha na usiku pia.

Halafu tutazame pia faida na hasara kwa uchumi, risk ni sehemu ya maisha.
 
Haina uhusiano na kusafiri usiku. Miaka yote ajali zinatokea gari zinasafiri mchana mbona hushauri nazo zisitishwe?
Kwema wakuu?

Kwa Hali ilivyo usalama barabarani nyakati za usiku ni mdogo madereva hawazingatii sheria barabarani wakati wa usiku maana hamna polisi. Malori nayo ndio mida Yao ya kukimbia so ajali ni nyingi mno. Madereva pia usiku wanasinzia barabarani sababu ya uchovu.

Kuna siku nimesafiri na basi la Frester kwenda Dar es Salaam, kufika Morogoro usiku kama saa nane, dereva anataka kugonga semi za mafuta sababu anaovetake pia hamna polisi barabarani.

Hivyo hivyo gari la Abood juzi tumetoka Dar dereva anaendesha kwa kasi pia tulilipanda pale mbezi saa kumi na moja alfajiri gari haikufanyiwa service maana ilikuwa inatoka mkoani na watu wanashuka pale Mbezi na sisi tunapanda sababu hawana muda wa service.

Chonde chonde serikali sitisheni hizi safari
 
Achana nao Mkuu! Serikali imefanya vizuri kuruhusu safari za usiku.
Kama wao wanaona shida kusafiri usiku wasafiri mida walioizoea.
Wengine wanapenda kulakula wakiwa safarini. Wakiona mayai lete, wakiona mahindi lete, wakiona miguu ya kuku shida.
Sasa safari za usiku hazina mambo hay
o.
na kwasasa usiku kuna abiria wengi sana,kama umewahi safiri usiku utakua shahidi.
 
Kwema wakuu?

Kwa Hali ilivyo usalama barabarani nyakati za usiku ni mdogo madereva hawazingatii sheria barabarani wakati wa usiku maana hamna polisi. Malori nayo ndio mida Yao ya kukimbia so ajali ni nyingi mno. Madereva pia usiku wanasinzia barabarani sababu ya uchovu.

Kuna siku nimesafiri na basi la Frester kwenda Dar es Salaam, kufika Morogoro usiku kama saa nane, dereva anataka kugonga semi za mafuta sababu anaovetake pia hamna polisi barabarani.

Hivyo hivyo gari la Abood juzi tumetoka Dar dereva anaendesha kwa kasi pia tulilipanda pale mbezi saa kumi na moja alfajiri gari haikufanyiwa service maana ilikuwa inatoka mkoani na watu wanashuka pale Mbezi na sisi tunapanda sababu hawana muda wa service.

Chonde chonde serikali sitisheni hizi safari
Kuna ukweli usiku ni muda wa kulala hata kama ulipumzika vipi, kuendesha labda yawe mayahudi mawili anaetoa gari ikifika saa nane usiku anampa mwingune aliyepumzika kwa kujiegesha pale chini.


Kingine gari za isamilo ni mbovu mno hazifanyiwi service mapema kuna moja juzi nilikuwa inatoka mwanza yaanj nilikuwa inasimama barabarani inafanyiwa service wanamwaga oil mule abiria wanasubiri tu zaidi ya mara moja
 
gari ni mashine mkuu,inapofanya kazi masaa zaidi ya mawili ikiwa na mzigo inahitajika service wacha ujuaji sana.

service sio lazima ubadili filter pump hata ukaguzi tu kuikagua mifumo kama iko OK ni dalili ya kuwa makini na uwekezaji wako,sio usalama wa abiria pekee.

gari inatembea masaa 12 inafika point B anabadilishwa dereva na tingo peke yake😄😄,uliishaona ndege namna inavyofanya kazi mkuu???
tajiri mwenye magari akiona ulichoandika hatakuelewa.
Hapo umetoa elimu sahihi katika uwanja usio sahihi.

Jf ya sasa imejaa wabishi wasiokuwa na uelewa.
 
Nakubaliana nawe kwenye ishu ya kujikagua hasa breki na matairi kabla ya kugeuka baada ya kusafiri safari ndefu..ila safari za usiku ni salama kabisa kwa sababu magari yanaenda kwa ratiba ya muda mfano gari linaloenda mwanza linapangiwa mda wa kufika dodoma, singida,nzega, shinyanga nk sasa hapo akiwahi sana kabla ya muda kuna sheria zinafuatwa...wanaheshimu muda siku hizi. Kuhusu kupata ajali zaidi usiku labda kama unatakwimu halisi toka polisi ila ajali hata mchana zipo nyingi sana.
 
Back
Top Bottom