Nashauri somo la physics liwe option kuanzia form one, mathematics liwe option pia

Means?,maadam mtoto wako anajua coding, watoto wa kindendeule huku lingusenguse wasijue coding, upumbavu huu
Anachoongelea mkuu ni tu-base kwenye quality(ubora) sio Quantity(wingi) wanafunzi wa michepuo ya sayansi wapo
wengi kweli na huwa zinajaa kila mwaka shule za sayansi tena kwa miaka ya sasa bila kuwa na B-flat kwenda mfano PCB ni kimbembe
lakini huko kwenye kada ya afya nini kimeongezeka!? jibu ni hakuna.
Ndio wenye akili wanaangalia quality tuwe na watu wachache ambao watukuwa mathink tank kwenye sayansi kuleta
evolution mpya, wale wakawaida waende wakaajiliwe huko
 
Tatizo ni serikali kuamua beba mizigo ya watu wajinga na wapumbavu.

Ingeacha wajinga waendelee kuwepo kuliko kuwa na wahitimu wengi wasio elewa kitu
Mkuu sio wajinga sema wanakalama zao ambazo mifumo ya elimu imezificha
mfano wanamichezo, wabunifu nk. elimu ikiwa inclusive ikaweza kutambua vipaji vyao wangali
watoto wanaweza kuwa lulu kwa taifa tunaona brazil inategemea mpira kwa kiwango kikubwa
na waliuendeleza na umewatoa.
Maywether hajui kusoma wala kuandika(kwa definition yako ni mjinga) lakini hakuna profesa anayemzid kwa mefanikio tukija kwenye pesa
pengine toka ulimwengu uanze
 
Ushauri wako ni sawa na kusema mtu akidaiwa deni, ajifungie Ndani ili asionekane.
Mimi napingana na wewe kwa Asilimia 100% Tatizo la msingi hapa ni miundo msingi ya kufundisha hayo masomo.
Nikupe changamoto kidogo ukafanyie utafiti; tafuta wastani/idadi ya waalimu wa shule za msingi wanaofundisha somo la hesabu, walio pata ufaulu wa angau D ya Hesabu kidato cha nne; Ukisha pata majibu, rudi tena hapa kutoa ufafanuzi kuwa TUNAVUNA TULICHO KIPANDA!!!
Mimi siwalaumu kabisa waalimu, kwani wanajitoa ilikuziba pengo la walimu wa hesabu....
 
Nchi haiwezi endelea kwa kukata mauno, kupigana, kucheza mpira.

Nchi inaendelea kwa kuzalisha mali.
Nchi zote hupimwa kwa GDP
 
Nchi haiwezi endelea kwa kukata mauno, kupigana, kucheza mpira.

Nchi inaendelea kwa kuzalisha mali.
Nchi zote hupimwa kwa GDP
Nimesema tu-invest kwa wale wanayoyaweza na kuyapenda masomo husika nimekutolea
mfano Elias Kihombo nini amefanya licha ya kuwa amebarikiwa uwezo mkubwa katika hayo masomo
ya sayansi, ninachoongelea ni isssu ya quality(ubora) sio quantity(wingi/idadi)
Tuwe na wanasansi kweli kweli kutoka kwenye damu kama kin Eistein, Newton, Tesla wale
wengine wenye mahaba na mambo mengine na wenyewe wapewe fursa kuonyesha uwezo wao
bila shaka kila mwisho wa wiki unaangalia mpira ligi ya england na sio kusoma majarida ya wanasayansi japo
kila siku utamia vitu hivyo maana yake kila kitu tukipe umhimu unaostahili
 
Solution yako ni hipi kama mdau wa elimu? Zigo tumuangushie nani? Hali inazidi kua mbaya sana, watoto haswa shule hizi za kata uwezo ni mdogo sana.
Nimesoma PCB pale Old Moshi high school, masomo ya sayansi ili yawe rahisi yanahitaji kufundishwa kwa practical zaidi. Mimi niliipenda sayansi hapo Old Moshi, tofauti na O level kwa sababu wale walimu (physics tulikuwa na Mwl Mrusi, Chemistry Mwl mmarekani na Biology mtanzania from UDSM) ilikuwa full practice. Yule Mrusi alikuwa ni full engeneer, alifufua mpaka magari ya shule yaliyokuwa yamekufa... Alikuwa na vifaa kibao vya kufundishia.. Sijui mambo ya speed of light, sound waves, kinetics, velocities etc.. Hii mambo ya kukariri tuu newton's law of motion, archemedes principles etc haisaidii kabisa kwa sababu Kiingereza ni tatizo kubwa sana kwenye shule zetu.
 
Tatizo ni serikali kuamua beba mizigo ya watu wajinga na wapumbavu.

Ingeacha wajinga waendelee kuwepo kuliko kuwa na wahitimu wengi wasio elewa kitu
Basic education ni kwa watu wote. Wenye uelewa mzuri na wasio na uelewa wa kutosha. Haya ni maazimio ya dunia na Sisi ni signatory wa hizo protocol.
 
Ni kuyawekea mkakati kabambe tu masomo hayo. Kwa nini iwe Tanzania tu na sio nchi zingine?! Unataka kusema nchi zingine wana akili kuliko Watanzania? Mungu alituumba wote na akili sawa, isipokuwa kuna mahala tumelega!
Tuanzie na namna tunavyowapata walimu wetu, je mfumo huo unatoa walimu competent kwenye sayansi?
 
Akili kubwa sana, comment bora ya kuanzia Mwaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…