Nashauri somo la physics liwe option kuanzia form one, mathematics liwe option pia

Pia kwa kuwa umesema wewe haina maana kwamba uko sahihi.
 
Somo la hesabu ndiyo linatakiwa kuwa msingi wa kwenda chuo chochote hata vya ufundi unesi , kilimo ,biashara, hata kujiunga mageshi pia
Ni kweli, wayasome sasa wanayoyaweza kupunguza zero, kuna haja gani kuwalazimisha watoto kitu ambacho hawana uwezo nacho?
 
Pia kwa kuwa umesema wewe haina maana kwamba uko sahihi.
Hakuna sehemu nimedai niko sahihi, ila ukienda ground utauona usahihi wangu
mfano Diamond, Messi, Samta, mo dewji, bakhresa, kishimba, JK, Sa100, Mohammed Ali, Gandhi, wale wafalme wa saudia na Qatar.
nachoongea wasome wale tu watakao apply hivyo vitu kwenye maisha yao ya kila siku mfano scientist.
mwisho kabisa tufanye research ya kweli nini kifanyike haya ni maoni tu japo naamini ni ya kweli
 
Ni kweli umeongea, watu wa mwanza wanamfahamu mkandawile na Michael na wengineo hawa walifanya mambo magumu tuyaone mepesi kwa sababu ya content walizokua nazo, nadhani wale walikua nondo vile kwa sababu tuition ziliwapa pesa sana, Michael mnyama alipelekwa shule ya taqwa but alifukuzwa kwa matokeo mabovu, unaweza ukanijibu kwanini?...shida ni wanafunzi? Au ni system mbovu ya kuendesha shule? Ukubali au ukatae Mathematics au physcs sio kwa ajili ya kila Mwanafunzi kuna wanafunzi wengine hata ufanyaje, wengine wanazaliwa given uwezo wa kuchaji kichwani unakuepo.
 
Hawa wataelewa kweli hayo masomo

Ova
Your browser is not able to display this video.
 
Hatuwezi kuwa taifa zima la coding, itafikia wakati coders watakuwa obsolete
Nadhani hoja hapa ilikuwa kuachana na mfumo wa wanafunzi kufundishwa kwa kukariri, hii kitu inaua sana uwezo wa wanafunzi ku reason in logical way... Sisi wa zamani tulikuwa na ule ufundishwaji wa kujenga hoja. Mitihani multiple choices ilikuwa only one section out of 4 or 5 sections. Ukisikia vile visa vya Msafiri ana kondoo, majani na mbwa mwitu na akafika mtoni ambako alitakiwa avushe kitu kimoja kimoja yote ilikuwa inalenga kufikiri na kupasua bongo..
 
Hayo unayo tamani yawe option ndio masomo yanayotawàla dunia,ila kwa kuwa mvivu,kwako yawe option ila kwa maslahi ya taifa yawe lazima hata itolewe ruzuku kuyaenzi na kuyaendeleza,🤔
Mkuu Mimi nimetoa wazo tu kwa ajili ya kupunguza F, ninaona ndio maana zunguka shule zote kipindi hiki wanaochagua physcs form 3 ni wangapi? Wengi wanakimbia saaana
 
Kwa uwelewa wangu mdogo naona mitaala ya masomo ya sayansi hasa physics iboreshe kuenda na na usasa zaidi na kufundishwa katika lugha raisi zaidi kwa hivi vidato vya chini, Mambo ni mengi sana kwa muda mchache huku kukiwa hakuna vifaa vya maabara kufanyia practical katika mashule zaidi imekuwa anayeweza kukariri zaidi ndiye mshindi huku wengine wakiwa hawaelewi....
Ili kuto wavunja moyo wanaotaka kuyachukua maana yakiogopwa sana tutakuwa na tatizo kubwa la wataalamu katika nyanja mbalimbali za sayansi.
Mimi ni mhanga wa Physics A level....Kuna vitu na maswali ya practical ndo nmekuja kuyaona kwa mara ya kwanza kwenye mtihani wa taifa.
 
Tuanzie na namna tunavyowapata walimu wetu, je mfumo huo unatoa walimu competent kwenye sayansi?
Mkuu, walimu wanaofundisha ordinary secondary level ni diploma holders, hawa walifaulu somo la mathematics na hivyo kuruhusiwa kusoma level ya diploma. Sio sahihi kabisa kusema kwamba hawa walimu hawajuwi mathematics, vinginevyo walidanganya kwenye matokeo ya mitihani yao! Tukumbuke walimu hawa walipatikana kutokana na mchakato madhubuti baada ya matokeo kutoka kwenye mamlaka inayothibitisha uwezo wa ki - elimu kwa mtu husika. Hawa sio wengine bali ni NECTA - ni chombo tunachokiamini sana kwa secta ya elimu hapa nchini kwetu. Sasa ukisema tusiwaamini hawa walimu wetu, ni sawa na kusema tusikiamini hiki chombo chetu! Je, ni sahihi? Hapana, bado chombo chetu kinafanya vizuri, tatizo lipo kwa wahusika wenyewe!
 
Tatizo ni serikali kuamua beba mizigo ya watu wajinga na wapumbavu.

Ingeacha wajinga waendelee kuwepo kuliko kuwa na wahitimu wengi wasio elewa kitu
Nakubaliana na wewe, hasa hasa kuanzia primary maana kuna cases mtoto unasikia kafaulu lakini kuandika na kusoma vizuri hajui... Angalia sasa hivi nguvu kubwa ni kujenga majengo lakini hatusikii maboresho ya walimu. Ilitakiwa wale waliofaulu vizuri Universities ndiyo wawe walimu na walipwe vizuri.
 
Mi pia nimepitia mfumo wa zamani wa kuandika na kufanya hesabu Darasa la 7, nini kilitokea hadi ikawa hivi ilivyo leo hatujui.

Ila elimu yetu imekufa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…